ostrichegg
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 12,048
- 6,199
Usipayuke sana nenda kasome kwanza taratibu mpya za chama chenu cha ndio. CCM ina mwenyewe.Mkuu tayari wana wagombea ubunge wao ,orodha anayo mwenyekiti Mbowe kim Il Sung kama humlambi viatu sahau ubunge kupitia Chadema,akina Sepetunga nao sijui tayari wameshatumikishwa ,Chadema ina mwenyewe ,wengine wote ni akina pangu pakavu tia mchuzi
Msalimie wa sanamu ya Diamond.Wabunge wenyewe kama kubenea wanaongelea shanga bungeni mnategemea nini
2005 CCM 80%, 2010 CCM 61%, 2015 CCM 54%, 2020 CCM .....load..Wenyewe wanasema "Chadema wana gain kila uchaguzi." Na pia hawana "hofu they will make it."
Ninaambatanisha ushahidi toka kwa Waterloo hapa chini.
Haya, shauri yako.2005 CCM 80%, 2010 CCM 61%, 2015 CCM 54%, 2020 CCM .....load..
NB. Haya ni matokeo baada ya kamati za ufundi za ccm ikiwepo tume ya taifa ya uchaguzi.
Umesema vizuri kabisa. Magufuli aliteua makada kushika nafasi za ukurugenzi wa Halmashauri ukifika uchaguzi akatangazwa ambaye hajashinda wataanza kulalamika eti wasimamizi ni makada. Wakati mwingine sielewi huu upinzani. Uchaguzi ujao A kutoka upinzani anashinda anatangazwa B wa CCM sasa andamana kumjaribu hapo ndo utajua.Sijui hawa jamaa wana mkakati gani na uchaguzi mkuu wa 2020 hususan kwenye upande wa wabunge.
Kulialia kuhusu sheria mbaya hakutobadilisha sheria mbaya kuwa sheria nzuri.
CHADEMA kama kweli wapo serious basi wangeanza sasa kuwaandaa watu wa kugombea ubunge kwenye majimbo yote ya Tanzania.
Mambo ya kuwaachia wagombea wa CCM wapite bila kupingwa halafu mnakuja kulialia baadaye kuwa eti sheria ni mbaya na mnamwomba Magufuli abadili sheria [wakati Magufuli hatungi hizo sheria] ni utoto wa kisiasa.
Anzeni sasa kuwa groom wagombea ubunge na muweke wagombea wenye sifa kwenye kila jimbo.
Msipoweka wagombea mnakosa kabisa hata nafasi ya kushinda. Uchaguzi ulopita kuna majimbo hamkuwa na wagombea ubunge. Aibu.
Msiwaze urais tu. Bunge nalo ni la msingi.
nakupa heko kwa huo moyo wa chumaHatutishiki maana hizi dalili zinaletwa na vijana wa Lumumba. Adui yako muombee njaa.
Chadema inachana mawimbi tusikimbiane tu hapa hiyo 2020
Asantenakupa heko kwa huo moyo wa chuma
Bunge lipi? Bunge la wengi wape. Hovyo! Wewe CHADEMA iache tu. Pilipili usoila yakuwashia nini?Sijui hawa jamaa wana mkakati gani na uchaguzi mkuu wa 2020 hususan kwenye upande wa wabunge.
Kulialia kuhusu sheria mbaya hakutobadilisha sheria mbaya kuwa sheria nzuri.
CHADEMA kama kweli wapo serious basi wangeanza sasa kuwaandaa watu wa kugombea ubunge kwenye majimbo yote ya Tanzania.
Mambo ya kuwaachia wagombea wa CCM wapite bila kupingwa halafu mnakuja kulialia baadaye kuwa eti sheria ni mbaya na mnamwomba Magufuli abadili sheria [wakati Magufuli hatungi hizo sheria] ni utoto wa kisiasa.
Anzeni sasa kuwa groom wagombea ubunge na muweke wagombea wenye sifa kwenye kila jimbo.
Msipoweka wagombea mnakosa kabisa hata nafasi ya kushinda. Uchaguzi ulopita kuna majimbo hamkuwa na wagombea ubunge. Aibu.
Msiwaze urais tu. Bunge nalo ni la msingi.
Mi navyoona mambo yanavyokwenda, hakuna wa kuitoa CCM madarakani... labda CCM ipasuke vipande viwili.
Wamemiliki kila kitu kinachoweza kuwapa ushindi wa haki au wa wizi.
Kwa mfumo huu, CDM na ndugu zao wote, watasubiri sana kuwatoa hawa wezi madarakani.
2005 CCM 80%, 2010 CCM 61%, 2015 CCM 54%, 2020 CCM .....load..
NB. Haya ni matokeo baada ya kamati za ufundi za ccm ikiwepo tume ya taifa ya uchaguzi.
Hii ni challenge na wapinzani wasipodai katiba mpya 2020 kuna uwezekano tusipate hta diwani mmoja nchi nzimaUmesema vizuri kabisa. Magufuli aliteua makada kushika nafasi za ukurugenzi wa Halmashauri ukifika uchaguzi akatangazwa ambaye hajashinda wataanza kulalamika eti wasimamizi ni makada. Wakati mwingine sielewi huu upinzani. Uchaguzi ujao A kutoka upinzani anashinda anatangazwa B wa CCM sasa andamana kumjaribu hapo ndo utajua.
Mnazunguka sana shida ni katiba kwa 2015 tulikuwa na uwezo kupata wabunge wengi sana hta hao 45 walipita kwa nguvu ya umma tu tusingeambulia hata mmojaMambo kama haya CDM hawapendi kuambiwa, hauna ofisi za kueleweka na resources zinatumika ovyo kununuliwa Tshirt za 120,000/Tsh unategemea nini?
Unataka kuingia Ikulu huku ukiwa na wabunge 40, ni wazi hata ikitokea miujiza ukaingia Ikulu, waziri mkuu na Spika bado watatoka CCM sababu ndio watakuwa na wabunge wengi bungeni, na wao ndio wataamua wamuondoe lini Rais sababu uwezo na nguvu hizo wanazo.
Shida rasimu ya warioba na ilizuiwa na magamba ssa mlitaka wapinzani wafanyeje??? Washikw mitutu??? Hata kma tutamsimaisha magufuli wenu kma mgombea wa UKAWA 2020 hawezi shinda nakuhakikishia!!! Shida ya upinzani sio sera wala ofisi shida ni TUME ....... mana hta 2015 tulikuwa na kila kitu cha kutuwezesha kushinda ila tukaanguka sembuse 2020?? Shida sio ofisi sijui nini mambo yote rasimu ya warioba ambayo ilizuiwa na maccm wenzioMzee Mwanakijiji hawa watu hawasaidiki tena kwa sasa, Majimbo mengi walishinda kutokana na kura za chuki dhidi ya CCM na si ubora wa wagombea wao, ila upepo umeshabadilika, EL alikuwa na pesa ndefu ya kufanya hamasa na amsha amsha, kwa 2020 hakuna mfanyabiashara atakayeweka pesa yake kwa EL au CDM sababu ni wazi hawana uwezo tena wa kumtoa Magu.
Hayawezekanu bila katiba mpya...... hta tusimamishe malaika huwezi fikisha wabunge 100 ccm anakuangalia tu!!! Tusidanganyane hapa....... kelele ziwe tume huru na rasimu ya warioba ila ofisi sijui wagombea hata tukiwapata bado hawawezi tangazwa mshindiNi mara nyingi sana Chadema wamekuwa wanapewa ushauri wa kuimarisha majimbo ya uchaguzi kama vile kuwa na ofisi za maana kwenye kata, tarafa, wilaya na mikoa, hata na makao makuu yenyewe.
Kukiwa na ofisi za maana na zikasimamiwa na watu makini inakuwa ni rahisi kazi za chama kuendelea kufanyika hata kama siyo vipindi vya uchaguzi, na ni katika harakati za namna hii unaweza ukaspoti potentials kwenye nafasi kama wenyeviti wa vijiji, madiwani na wabunge. Siyo kusubiria kina Bulaya, Lembeli na CCM washindwe ndo wahamie kugombea kupitia CDM.
Na hili likifanyika ki-ufasaha ni rahisi kuongeza idadi kubwa ya wabunge ambao wanaweza kuleta impact hata kwenye kuzipitisha hizo sheria.
Mpaka tutakapokuwa na idadi ya wabunge pinzani yenye kumiliki kura bungeni ndipo tutaweza kuufikiria Urais, maana kwa hii katiba ambayo refa ni wa CCM, kamisaa na vibendera ni CCM, uwanja ni wa CCM hatuwezi kushinda mechi ya fainali.
..kwa maoni yako unadhani ni fikra/jambo gani ambalo CDM wanatakiwa kupambana nalo sasa hivi?
..my observation ni kwamba Mzee haamini ktk demokrasia ya vyama vingi. Haamini ktk uhuru wa mawazo. Hapendi uhuru wa wananchi kukusanyika freely au kuji express kwa njia ya maandamano.
Upinzani wa Tanazania nao inabidi wawe creative aisee. La sivyo watakuwa ni wapinzani daima na hawatokuja kushika madaraka...iwe bungeni au ikulu.
Rasimu ya Warioba ilitokana na mchakato haramu ulioanzishwa ndani ya CCM. Ilikuwaje wapinzani walidandia kitu amabcho kilikuwa wazi - kwa baadhi yetu - kuwa hakiendi popote?Shida rasimu ya warioba na ilizuiwa na magamba ssa mlitaka wapinzani wafanyeje??? Washikw mitutu??? Hata kma tutamsimaisha magufuli wenu kma mgombea wa UKAWA 2020 hawezi shinda nakuhakikishia!!! Shida ya upinzani sio sera wala ofisi shida ni TUME ....... mana hta 2015 tulikuwa na kila kitu cha kutuwezesha kushinda ila tukaanguka sembuse 2020?? Shida sio ofisi sijui nini mambo yote rasimu ya warioba ambayo ilizuiwa na maccm wenzio
Mkuu upinzani ulidai katiba 2010 na kikwete hakuwa ameweka kwenye ilani ya ccm!! Ssa huo mchakato vp ulikuwa wa ccm?? Mbona tume ya warioba ilikuwa imejaa wazalendo wa akina kabudi polepole (kabla ya uteuzi) baregu ramadhan n.k na walifanya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi ssa ulitaka wapinzani wasiunge mkono wakato tume ilikuwa huru kabisa!!!!Rasimu ya Warioba ilitokana na mchakato haramu ulioanzishwa ndani ya CCM. Ilikuwaje wapinzani walidandia kitu amabcho kilikuwa wazi - kwa baadhi yetu - kuwa hakiendi popote?