Mazindu Msambule
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 7,508
- 6,891
TBC inaheshimika sana duniani, haipo tayari kumualika mtu kama Mh. Lema ambaye anaonekana wazi kabisa kwamba uwezo wake wa kufikiri ni mdogo na malezi yake ya utotoni hayakuwa mazuri.
Mkuu sio kweli.Nakutolea mfano mdogo tu hapa Lindi tupo analojia bado na wakazi wengi wanatumia antena ndogo maarufu kama chadema na wanakamata TBC tu.TBC ni mali ya watanzania wote na Chadema ni chama cha wananchi.Tuna kila sababu ya kulisemea hili.Haina athari kwa kuwa wananchi wengi wanaoiunga mkono CHADEMA ni hohe hahe (wasio na hela ya king'amuzi) na baadhi ya watu ambao hawana hata umeme....wanategemea zaidi magazeti...
Wanaoangalia TBC wengi ni wale wazee wa dar es salaam.
inaonekana cdm ikibahatisha wakachukua madaraka,mkuu wa TBC na watangazaji wote watakula vitanzi,peeeeeeeeeooooopleeeee?sidiemu wameibaikoti tibisii
Chadema wana vita na Ccm,
Tbc ni Ccm
vita ya Ccm ni ya Tbc pia, wewe hujui hilo? Watakucheka watu!
Kwani wewe sio mtanzania?Muelekeo wetu kama nchi tunataka kuona mageuzi makubwa katika nyanja za kiuchumi,kijamii na kisiasa hususani maeneo ya kilimo,madini, utawala bora,uhuru wa vyombo vya habari,ukuaji wa demokrasia na nk na hatimaye kufikia malengo ya millenia.Kwani mnaenda wapi...?
Mkuu umenena vema.Tunahitaji kuwa na uelewa wa ziada na kujiongeza zaidi! CCM wana bifu na CHADEM lakini TBC ni mali yetu watanzania wote na tusipolionesha hilo kwa sauti moja, basi watakuja kujimilikisha kama walivyojimilikisha viwanja vyote vya michezo wakati tulibeba zege sote na wengine kukamatiwa kuku wetu kwa nguvu. Ipo siku hata mawe yatatoa ushahidi.
Nasikitishwa sana kuona wabunge wa CHADEMA hawashiriki katika mijadala inayoendeshwa na television ya taifa (TBC) hususani vile vipindi vya asubuhi.
Sifurahishwi kwa sababu kuna watanzania wengi wana access na station hii na wanahitaji sana michango murua kutoka kwa wabunge machachari wa CHADEMA.
Niwaulize enyi viongozi wa CHADEMA,je mna mgogoro na TBC na nyinyi TBC je mna mgogoro na CHADEMA?Na kama jibu ni ndiyo kwanini msikae mkayamaliza?Hamuwatendei haki watanzania kwa kweli.
Jirekebisheni.
Mmmmmh!Hii nchi yangu kila kitu siasa sasa.Tutafika kweli?
TBC inaheshimika sana duniani, haipo tayari kumualika mtu kama Mh. Lema ambaye anaonekana wazi kabisa kwamba uwezo wake wa kufikiri ni mdogo na malezi yake ya utotoni hayakuwa mazuri.
Mmmmmmh..Je kususa ndio solution?Kujirekebisha kwa TBC ni kwa vigezo gani?Huenda ulikuwa safarini na pia unakaa mbali na vyombo vinginevyo vya habari isipokuwa TBC na washirika wake. Hii ni kwa sababu CHADEMA walipofanya mkutano wao wa uongozi baada ya rabsha zilizotokana na kuzuiwa kwa mkutano wao na kuuwawa kwa Mwangosi, waliitangaza TBC kama janga la taifa na kutangaza kuisusia rasmi ikiwa ni pamoja na kuwataka wapenzi wake na wananchi kwa ujumla kuisusia. Taarifa hizi zilitolewa na vyombo mbalimbali vya habari, ila sina hakika kama TBC na washirika wake walizitoa. Kwa bahati mbaya, kwa kuwa wewe ni mshirika mzuri wa TBC ndio sababu huenda hukupata nafasi ya kufahamu lililokuwa nje ya box. Kwa msingi huo basi, sitegemei kiongozi yeyote wa CDM kushiriki katika jambo lolote lifanywalo na TBC hadi pale chombo hicho kitakapojirekebisha na kuwa cha kitaifa na sio kipeperushi cha CCM (maneno ya Mbowe).
Bahati mbaya, binafsi nilikuwa sinaga mpango kabisa na TBC kama nisivyojua kama RTD bado ipo hewani (Niliachana navyo tokea maigizo ya Mzee Jongo na Jangala).
Ndiyo umeandika nini hapo?!sidiemu wameibaikoti tibisii
Nasikitishwa sana kuona wabunge wa CHADEMA hawashiriki katika mijadala inayoendeshwa na television ya taifa (TBC) hususani vile vipindi vya asubuhi.
Sifurahishwi kwa sababu kuna watanzania wengi wana access na station hii na wanahitaji sana michango murua kutoka kwa wabunge machachari wa CHADEMA.
Niwaulize enyi viongozi wa CHADEMA,je mna mgogoro na TBC na nyinyi TBC je mna mgogoro na CHADEMA?Na kama jibu ni ndiyo kwanini msikae mkayamaliza?Hamuwatendei haki watanzania kwa kweli.
Jirekebisheni.
Thibitisha kwamba inaheshimika duniani..vyombo vinavyo heshimika duniani vinatambulika...SABC, CCTV, BBC, RT, CNN, Al Jazeera, Citizen!! Hakuna chombo chochote cha habari ndani ya bongo hii kinajulikana huko nje!!TBC inaheshimika sana duniani, haipo tayari kumualika mtu kama Mh. Lema ambaye anaonekana wazi kabisa kwamba uwezo wake wa kufikiri ni mdogo na malezi yake ya utotoni hayakuwa mazuri.
Tokea TBC wamfukuze kazi Tido Mhando, kwa maagizo ya ofisi ya Lumumba,eti kwa kosa la kuandika balanced stories, hiyo stesheni, badala ya kujiita televisheni ya Taifa, jina ambalo linawastahili ni waitwe TBCCM!!TBC imekuwa kama radio ya chama,na haiaminiki kwa sababu imekuwa ikieneza propaganda na kusahau jukumu lake la kuelimisha wananchi.Watu wengi hawaisikilizi siku hizi.