Nchi hii bana full usanii tu, hakuna cha CCM wala CDM, wote wachumia tumbo tu.
Hiyo picha ya ofisi binafsi haija nishangaza sana, lakini unaijua makao makuu ya CDM?
Inatia aibu kiukweli, wanapata ruzuku mamilioni yote yanaishia kwa kundi la wafanyabiashara kwa kigezo cha kuendesha shughuli za chama, shughuli za chama hata ofisi ya maana wanashindwa kujenga.
Wapo bize kulipana mishahara mikubwa tena yenye kila harufu ya ufisadi, eti mshahara kidogo kisha marupu rupu kibao ilimradi tu kukwepa kulipia kodi(rabish) kweli nyani haoni kundule.Leo hii mapato ya Slaa ni ufisadi mwingine na kwa wenye akili timamu ni kufidia ubunge alio uachia ilikugombea uraisi
Ni rahisi sana kuiona CDM mkombozi ikiwa nje ya madaraka kwa sababu CCM imepoteza dira kabisa, nikama nchi imewashinda, na mkombozi unayeweza "kumdhania" kwa sasa ni CDM, lakini CDM pia kuna tatizo pale, tatizo ambalo hatuwezi kuliona kwakuwa CCM imetukinai,imepoteza matumaini yetu.
Mleta mada Pengine marehemu Chacha Wangwe ndio hichi alikuwa anapigania, ruzuku zipelekwe mikoani na kisha wilayani kujenga chama(ikiwemo ofisi), akaishia kujenga bifu zito na "wenye chama"
Kimsingi kama unaupeo wa kufikiri hatua kadhaa mbele utaona tofauti kati ya CCM na CDM ni kuwa kimoja kipo madarakani(kwenye neema) na kingine kinapigania kuingia kwenye neema.
Siamini tena ukombozi wa kweli kupitia hivi vyama vyetu, labda bila kujali nani kashinda tukiwa na uwiano unaoendana wa wabunge wa upinzani na wamadarakani na wagombea binafsi na bunge likipewa meno walau tunaweza fika tuendako
LAKINI KWA SASA WOTE NI FULL USANII TU