CHADEMA NA m4c na PROJECTORS..KAMPENI HALISIA KABISA

theHAVARD_product

JF-Expert Member
May 4, 2012
289
191
​Nadhani imefika mahala CHADEMA ikatumia njia nyigine kufikia watu..Walianza na Choper,na walifanikiwa sana katika hili mwaka 2005,2010 na hata 2015 itazidi kuwasaidia,na hasa baada ya sasa kumiliki Choper NNE!

Katika SIASA za Afrika ambapo JAMII kubwa ni UNEDUCATED kufikia watu wengi na kwa uzuri zaidi yahitaji UBUNIFU wa hali ya juu.



Kuna wananchi bado wako 50/50 Wameichoka CCM na bado hawaamini UPINZANI utaleta ukombozi/mapinduzi ya kimaendeleo katika nchi hii! Unaongelea kuhusu watu kunufaika na MADINI yao,ila watu hao hawajui kunufaika na madini kupoje!! kadhalika,Unaongelea kuhusu watu kunufaika na GESI yao,ila watu hao hawajui kunufaika na gesi kupoje!!

Nazungumzi jamii za chini kabisa,
1)Unaongelea kuhusu stand ya VUMBI na Wanafunzi kusomea Chini GEITA na Kama watu wanaona PICHA kwenye projector HAMASA inazidi kuongezeka zaidi!

2)Unazungumzia kuhusu AMBULANCE vibajaji ambavyo vimekufa (HAZIFANYI KAZI) ukiwa na picha Unaeleweka maradufu!

3)Unazungumzia kuhusu MADAWATI na MADARASA yaliyobomoka kutokana na UFISADI unaeleweka zaidi.

4)Unazungumzia kuhusu UBOVU wa BARABARA unaotokana UFISADI unaeleweka zaidi.

5)Unazungumzia POWERTILER feki zinavyotesa wananchi. unaeleweka vizuri mno.

JE PROJECTORS ZITATUMIKAJE?

kama mkutano unaanza saa 8 mpaka saa12,ukipata nusu /saa zima mwisho wa mkutano kuonesha watu mambo yanayojiri KUTOKANA na CCM si mbaya.. Wataelimika na kujionea zaidi. Kuna watu hawafuatilii hata vyombo vya Habari!

Nadhani,majuzi tu Mbunge wa Musoma mjini(mh.Nyerere) ametoa seti za Tv sokoni ili watu wafuatilie yanayojiri katika taarifa za habari.Watu wako bize zaidi katika kutafuta Mkate,na hili linawanyima hata fursa ya kufuatilia mambo ya nchi yao. Na hili ni janga,Janga kabisa.

kuna watu waliwahi kushauri kuhusu kuwepo CHADEMATv,hii ni silaha kubwa sana,inahitajika ASAP! Ukiianza kufuatilia tangu mtirirko wa Mauaji ya Morogoro,Iringa na hata kipindi kile Arusha nasita kuelewa kwanini haipo!
Kama Mmeshindwa kuhusu CHADEMATv jaribuni na hichi Basi.kinachotakiwa ni mtirirko wa Documentaries zinazoelezea hali halisi ya Maisha ya WaTanzania wasionufaika na RASIMALI Zao.


 
Mkuu ushauri wako ni mzuri sana naongezea muda kama mkutano ni saa nane kuanzia saa sita zianze kuonyeshwa documendary kwenye projector kwa masaa kama mawili wakati wageni na watu wanasubiriwa kuhudhuria mkutano bila kusahau vipeperushi vyenye ujumbe mbalimbali unaohusu ukombozi wa nchi hii vigawiwe kwa wananchi lazima sasa mambo yaende kisasa humu jamvini tulisha lisemea sana jambo la afisa habari kutuwekea update na picha mikutano inapokuwa inaendelea hasa hizi operation maalum watu wanataka kujua chama kinavyofanya shughuli zake.
 
100% nakubaliana na huu ushauri,cdm fanyieni haraka huu ushauri.nimeamini watu wanaipenda cdm kwa moyo wote.ubarikiwe sana mtoa mada
 
Mi nakubaliana na mtoa mada mimi wazo langu cdm wangekuwa na hizo projecter zitakazo onesha picha za weekness ya ccm,na kumbukumbu ya mwl maneno yale makali makali yale ya mwl ya kuhusisha na kitu cha sasa hivi mana yule mzee alikuwa anaongelea future wakati mwingine,naona ingekuwa cku moja kabla ya mkutano wa cdm ili wana nchi usususani vijijini watapata mwanga jamani mana hawa ndio wanaohumia sana yani hadi sometimes huwa nawaoneaga huluwa sana.
 
Kampeni zitakua za kisasa zaidi, wananchi kuelimishwa zaidi na ushindani wa kisiasa kuendelezwa zaidi katika kila chamaa cha siasa kote nchini BILA HATA YA MTU MMOJA KUTAFUTA NJIA ZA MKATO KWA KUTUMIA MIZENGWE NA MAZOEA YALE YA ZAMANI.

Kama ni fedha, wananchi tujiaanda kuzipata KWA MAGUNIA TUKIHONGWA NA WALE WANA-USWISI WA KULE CCM lakini kura yako ya kujikomboa ni kwa CHADEMA hadi kieleweke safari hii.
 
Kampeni zitakua za kisasa zaidi, wananchi kuelimishwa zaidi na ushindani wa kisiasa kuendelezwa zaidi katika kila chamaa cha siasa kote nchini BILA HATA YA MTU MMOJA KUTAFUTA NJIA ZA MKATO KWA KUTUMIA MIZENGWE NA MAZOEA YALE YA ZAMANI.

Kama ni fedha, wananchi tujiaanda kuzipata KWA MAGUNIA TUKIHONGWA NA WALE WANA-USWISI WA KULE CCM lakini kura yako ya kujikomboa ni kwa CHADEMA hadi kieleweke safari hii.
Hii nayo itazidisha CHANAGAMOTO kwa MAGAMBA,hakutakuwa na Shule za Nyasi
 
Ushauri wa msingi kabisa kwa kuongezea, hata vile vipndi vya bunge wachukue waedit na kuwaonyesha jinsi magamba wanavyotetea ufisadi na ushenzi na kuonyesha jinsi wapambanaji (CDM) wanavyowapigania wananchi........2015 hawa magamba sijui magome watoke wakafie mbali.
 
Projectrs mchana haiwezekani, watu hawataona labuda muda ubadilishwe use usiku
kuna projectors zinapiga hata mchana..zinategemea na luminous,,siku hizi kuna hadi projector zenye luminous 5000! ukiona ambazo mchana hafifu ujue luminous ni ndogo. Hata hivo hata ukiwa na yenye luminous 1500 ukianza sa12 si haba!
 
Pls CDM hembu njooni hapa mtoe maoni yenu kuhusu hili suala tunalojadili, watu wanaumiza vichwa jinsi ya kuwatoa hawa magamba madarakani, mnyika wewe ndio mtu wa uenezi nini maoni yako khs hili.
 
Kutokana na umuhimu wa kuwafikishia ujumbe mahususi wa UKOMBOZI kwa Wananchi haswa wale wa vijijini, hata kama projector itakuwa ngumu, napenda kuongezea kuwa iwepo fursa ya kuwaekea ''VIDEO'' itakayowafanya wakusanyike mapema ili waiangalie,... Lakini iwe imekusanya matukio muhimu kama hayo yaliyosemwa hapo juu....!! Naunga mkono Hoja!
 
Wazo zuri sana cha msingi hapa aje kiongozi wa chama ikiwezeka hata kwa kuchangia tupo tayari zipatikane projector za kutosha.
 
Back
Top Bottom