CHADEMA NA m4c na PROJECTORS..KAMPENI HALISIA KABISA

Nimatumaini yangu kuwa Mnyika na wengine wantusikia.

Kila njia zitumike kwa ajili yakuwafikia watu. Chadema inaweza kuanza nakutoa mikanda ya cd kuhusu mambo yamsingi na kufunza watu nakuzigawa bure au kwa pesa kidogo. Katika cd hizi au video wazungumzie mada mbali mbali kama uchumi wa nchi, sera za chama na utekelezaji wake katika kumkomboa mwananchi wa kawaida. Jambo hili ndilo lililofanywa na Hayatola Komein wa Iran kuleta mapinduzi angali akiwa exile. Pia wanaokumbuka jinsi mtikila alivyokuwa anawafikia watanzania wengi kupitia kanda zake alizokuwa akizitoa.
 
napingana na mtoa mada kwa aina ya mkakati anaoshauri kutumiwa na chama. mimi nadhani hatuna haja ya kuwaaminisha watu hali halisi ya nchi hii, kiuchumi, kijamii na kadhalika kwani wenyewe ni mashahidi tosha wa kinachoendelea katiika maeneo yao- viwango wa shule za msingi, sek ondari za kata vituo vya afya, zahanati, upatikanaji wa maji safi na salama, umeme disel , gas, gharama za maisha katika vyakula,usafiri, rushwa za aina zote kutaja kwa uchache tu.
Mimi nadhani muelekeo wa chdm kuwafikia wananchi wengi wa vijijini bado ni mkakati mzuri. ila mikakati ieleze kwa mapana jinsi ambavyo serikali ya chdm itakavyoweza kukabiliana na hizi changamoto zinazojitokeza leo. ni kwa namna gani na sera gani za ndani na nje ya nchi zitakavyoweza kuwasaidia wananchi kuondokana na umasikini, ieleze wazi wazi jinsi kilimo kinavyoweza kukuza uchumi wa nchi hasa kwa watu walio vijijini ambao ndiyo wengi na tena masikini. tatizo la vijana, utumiaji na ulinzi wa rasilimani za taifa, je uwekezaji nje umekuwa na tija ya kutosasha kuleta maendeleo ya watanzania. jingine ni kwa jinsi gani chdm kinavyoweza kulinda amani , usalama, haki, udugu, umoja na mshikamano. (kulinda katiba ya nchi kwa manufaa ya wote)
 
wazo naunga mkono 100 kwa 100 ,
viongozi chadema mpo humu jukwaani?
Tunataka sikia maoni yenu kwenye hoja hii.
 
Back
Top Bottom