CHADEMA na Lowassa, Homa ya CCM

CHADEMA na Lowassa, Homa ya CCM

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,602
Reaction score
830,313
Tunaendea kwenye uchaguzi mkuu nchi mwishoni mwa mwaka huu kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu
Tunafanya hivyo kwakuwa tunaamini katika demokrasia na uongozi wa kisiasa.

Ni kwa muktadha huo ndio tunapata vyama vya siasa vitakavyopambana ili kushinda uchaguzi na hatimaye kuchukua madaraka ya nchi na kuongoza.

Tuna vyama vingi vya siasa, lakini vilivyo hai na mwelekeo wa kupambana kwenye sanduku la kura ni CHADEMA/UKAWA na ccm! Hapa ndio kuna mtifuano.

CCM kimekuwa chama tawala tangu Uhuru, kikafanya mazuri mengi mwanzoni lakini kadiri kilivyozidi kuwa kikongwe kikasahau misingi yake na kupoteza dira kabisa, kimebaki kuwa chama butu kisichoweza kuwa na sauti yoyote ya kukemea na kusimama kwenye misingi kwa watu wake! Lakini ndani yake kukiwa na watu wenye uwezo wa kufanya hivyo japo wanakosa nafasi.

Sasa uchaguzi unapokaribia ndio kinazinduka na kuanza kujitutumua ilihali kishachelewa mno! Rushwa imetamalaki, huduma za jamii zimedumaa, watendaji wamefubaa na mifumo ya uongozi na utawala bora vimeparaganyika kabisa, kila mtu anaangalia anapata nini kwenye nini.

Kuna hawa watu wawili ambao at least wana uelekeo wa kuirudisha nchi kwenye mstari wake, kuirudisha mifumo kwenye utaratibu wake, kuleta uwajibikaji serikalini na kila mahali.

Watu hawa wawili CHADEMA/ UKAWA NA LOWASSA ndio homa ya ccm kwasasa wanamfahamu vyema Lowassa hacheki na nyani na wanajua atafanya nini akiingia ikulu, ataleta kilio kikubwa kwa wengi, ana nguvu uwezo na uthubutu wa kufanya hivyo.

CHADEMA hawatofautiani na Lowassa watafanya kama atakavyofanya Lowassa kuirudisha nchi kwenye mstari, CHADEMA inajulikana vyema kwa ccm hawana utani wala mchezo na wanataka kuithibitishia dunia na wanaccm kuwa wanaweza hapa kutakuwa na kilio.

Kwahiyo kwasasa CCM imebanwa kotekote haijui ideal na CHADEMA au Lowassa hakuna mwenye afadhali mboga moto, ugali moto!
Chama Tawala kiko njiapanda.
 
Mpwa Mshana umenena maneno ambayo ni ya kweli kuna mzee m1 hapa wa chama tawala anasema usungiz hawapati hivi wameitwa wajumbe wote wanatakiwa dodoma mwisho wa mwezi kujadili mstakabali wao ila ngona ngumu hela hawana yani balaaa M4C tutaendeleza mapambano
 
Kazi kweli kweli umenena kwl unajua ccm hawataki kumuweka lowassa kwa sababu wanajua wakimuweka akishinda kwa mfano atatibua dili zao nyingi na chama hakina pesa wapo njia panda wanatapatapa
 
Lowasa yupi unazungumzia huyu fisadi au mwingine.
 
Lowasa na wizi wake amuongoze nani wewe.
 
Tunaendea kwenye uchaguzi mkuu nchi mwishoni mwa mwaka huu kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu
Tunafanya hivyo kwakuwa tunaamini katika demokrasia na uongozi wa kisiasa.

Ni kwa muktadha huo ndio tunapata vyama vya siasa vitakavyopambana ili kushinda uchaguzi na hatimaye kuchukua madaraka ya nchi na kuongoza.

Tuna vyama vingi vya siasa, lakini vilivyo hai na mwelekeo wa kupambana kwenye sanduku la kura ni CHADEMA/UKAWA na ccm! Hapa ndio kuna mtifuano.

CCM kimekuwa chama tawala tangu Uhuru, kikafanya mazuri mengi mwanzoni lakini kadiri kilivyozidi kuwa kikongwe kikasahau misingi yake na kupoteza dira kabisa, kimebaki kuwa chama butu kisichoweza kuwa na sauti yoyote ya kukemea na kusimama kwenye misingi kwa watu wake! Lakini ndani yake kukiwa na watu wenye uwezo wa kufanya hivyo japo wanakosa nafasi.

Sasa uchaguzi unapokaribia ndio kinazinduka na kuanza kujitutumua ilihali kishachelewa mno! Rushwa imetamalaki, huduma za jamii zimedumaa, watendaji wamefubaa na mifumo ya uongozi na utawala bora vimeparaganyika kabisa, kila mtu anaangalia anapata nini kwenye nini.

Kuna hawa watu wawili ambao at least wana uelekeo wa kuirudisha nchi kwenye mstari wake, kuirudisha mifumo kwenye utaratibu wake, kuleta uwajibikaji serikalini na kila mahali.

Watu hawa wawili CHADEMA/ UKAWA NA LOWASSA ndio homa ya ccm kwasasa wanamfahamu vyema Lowassa hacheki na nyani na wanajua atafanya nini akiingia ikulu, ataleta kilio kikubwa kwa wengi, ana nguvu uwezo na uthubutu wa kufanya hivyo.

CHADEMA hawatofautiani na Lowassa watafanya kama atakavyofanya Lowassa kuirudisha nchi kwenye mstari, CHADEMA inajulikana vyema kwa ccm hawana utani wala mchezo na wanataka kuithibitishia dunia na wanaccm kuwa wanaweza hapa kutakuwa na kilio.

Kwahiyo kwasasa CCM imebanwa kotekote haijui ideal na CHADEMA au Lowassa hakuna mwenye afadhali mboga moto, ugali moto!
Chama Tawala kiko njiapanda.

Mkuu kamati ya ccm ipo faragha kwa sasa, ikiwa na ajenda moja tu, kumjadili lowassa ni jinsi gani wataweza kutompitisha katika kinyanganyiro cha uteuzi wa chama katika nafasi ya urais.
 
Kwani Lowasa na CCM ni vitu viwili tofauti? Kusema kuwa CHADEMA hawana tofauti na Lowassa ni kunifanya nianze kufikiria upya wa kumpa kura yangu Octoba 2015!
 
Lowassa huyu huyu fisadi, Hebu kuweni serious jamani!

Lowasa yupi unazungumzia huyu fisadi au mwingine.

Ndiye anayesikika sasa hivi ndani ya chama, na ana kundi kubwa sana ndani yake! Na hakuna mwenye uwezo kwasasa wa kumnyooshea hata kidole, kimsingi wanamgwaya na hata wakitaka kumtaja lazima waangalie kushoto na kulia mbele na nyuma
 
Nafikir lowasa n tishio kwa nn wanataka wampinge ili hali ss wananch ndo tunachagua?hatutak kuchaguliwa mtu ss sio watoto
 
Kwani Lowasa na CCM ni vitu viwili tofauti? Kusema kuwa CHADEMA hawana tofauti na Lowassa ni kunifanya nianze kufikiria upya wa kumpa kura yangu Octoba 2015!
soma vizuri,nadhani hujaelewa...
 
Mkuu kamati ya ccm ipo faragha kwa sasa, ikiwa na ajenda moja tu, kumjadili lowassa ni jinsi gani wataweza kutompitisha katika kinyanganyiro cha uteuzi wa chama katika nafasi ya urais.

Wamechelewa mno keshajikits mno maamuzi yoyote ya kutompitisha ni janga na kumpitisha pia ni janga inahitajika nguvu ya ziada kujipanga mno na kuvumilia uchungu mwingi kutokana na madhara yatakayofuatia kutoteuliwa kwake
 
Hii kufananisha utendaji mbovu wa kazi wa Lowasa na CHADEMA mimi nalipinga kabisa .Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ukiona mtu anatumia gharama nyingi kusaka madaraka hafai kuwa kiongozi anatakiwa kuogopwa kama ukoma au Ebola .hapo utakuwa umejifunza kitu huu ni mtamazamo wangu .
 
Nafikir lowasa n tishio kwa nn wanataka wampinge ili hali ss wananch ndo tunachagua?hatutak kuchaguliwa mtu ss sio watoto
una ndoto Lowasa atakuja kuwa raisi wa tanzania .utaota sana ikulu wanaingia watu waadilifu .
 
Back
Top Bottom