Mkuu, haya yanayoendelea yanatokea ndani ya CHADEMA. Ni makosa makubwa kwa CHADEMA kudhani kuwa kila baya linalotokea ndani ya chama chao linatokana na ushawishi au mkono wa ccm
Ni lini ulishawahi kuwa na nia njema na CHADEMA hadi maoni yako yachukuliwe serious kiasi hicho wakati siku zote umeonyesha chuki ya hali ya juu dhidi ya CHADEMA?Acha hila
Karibu vyama vyote vya siasa nchini hususani vile vikubwa vimekuwa vikitumia hoja ya VIKAO HALALI VYA CHAMA kama njia ya kubana wanachama wake kutoa maoni; au labda kwa usahihi, kuwazuia kueleza maovu ya chama. Katika hili, CHADEMA ndo sio wastahimilivu hata kidogo; heri ya CCM wanavumulia wanachama wao katika kile kinachoitwa kutoa habari za chama bila kupitia viako halali vya chama. Kwa bahati mbaya kabisa, wana-CHADEMA wa kawaida nao wameingia kwenye mtego huu, kwamba inapotokea mwana-CHADEMA ameeleza mambo yanayowachukiza viongozi nje ya utaratibu wa kawaida; wana-CHADEMA hawa wa kawaida watakuja juu na kumtuhumu mwenzao kwa kumuita majina mbalimbali ya hovyo hovyo!
Wapenzi, wanachama na mashabiki wa kawaida wa vyama vya kisiasa nadhani wanatakiwa kuamka na kugundua kwamba hiki kinachoitwa kwamba ni VIKAO HALALI VYA CHAMA ni ghiriba tu za viongozi wa vyama hivi ya kutaka yale mabaya ya vyama yasisemwe! Hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA kwa hakika kina jina la kuvutia na ndio maana hata wale wapenzi na wanachama wa kawaida nao wamekuwa wakiimba nyimbo hizi za VIKAO HALALI VYA CHAMA! Hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA ni kama kile kingine kinachoitwa UTAWALA BORA ambao Watanzania wengi tumekuwa tukiupigia upatu bila kufahamu kwamba UTAWALA BORA ni kichaka cha maovu ya viongozi na watendaji mbalimbali! Utawala Bora hauwezi kuwa na manufaaa kwa wananchi ikiwa unakuwa practiced kwenye jamii isiyo na maadili kama ya kwetu!
Sasa turudi kwenye hiki kinachoitwa kwamba VIKAO HALALI VYA CHAMA!! Hivi leo hii tuseme kuna mwanachama ana uhakika kabisa kwamba (say) Dr. Slaa au Freeman Mbowe amefanya ABC; tena jambo la fedheha kabisa! Hivi kweli mwanachama huyo anaweza kuwa na Ujasiri wa kusimama mbele ya VIKAO HALALI VYA CHAMA na kutamka waziwazi maovu hayo? Kama atakuwa na huo ujasiri, ni wanachama wangapi wanaweza kuwa na huo ujasiri wa kumchana LIVE mwenyekiti au katibu wa chama ambao tayari wamesha-prove kwamba hawana uvumilivu dhidi ya maoni hasi!
Kwa upande wangu, sina tatizo na hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA lakini nadhani ni busara watu tukaangalia ni nani wanapaswa kuachiwa kuimba nyimbo hizo! Mwacheni Mbowe, mwacheni Dr. Slaa au watu wengine kama hao waimbe hizo nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA kwani kutofanya hivyo ni kuhatarisha nafasi zao kwenye chama! Sitaki kuamini kwamba kutahatarisha uhai wa chama unless kama tunataka kusema CHADEMA ni MBOWE au SLAA! Wakati sioni tatizo kwa akina Mbowe kuimba nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA lakini kwa mpenzi, shabiki na mwanachama wa kawaida ambae wala hajui hata viatu anavyovaa Dr. Slaa ni rangi gani au vile vya Mbowe; basi kuimba nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA ni uzuzu! Ni uzuzu kwa sababu whether you like it or not; kamwe hutaweza kufahamu ukweli mchungu unaokihusu chama chako kupitia hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA unless if youre prepared whether for bad or worse, wewe na chama chako tu kama ilivyo kwa Waislamu au Wakristo na dini zao!!
Hawa watu na wanachama wa kawaida nadhani ingekuwa ni busara zaidi kujadili contents za tuhuma kuliko kungangana na VIKAO HALALI VYA CHAMA ambavyo hata wao wenyewe hawahudhurii! Hili ambalo kwa wana-CHADEMA wanajidanganya kwamba eti ni kutowafumbia macho wasaliti ni ujinga mtupu, sana sana lina-prove ni jinsi gani UONGOZI WA CHADEMA unavyoandamwa na vivuli vya uoga! Swali la VIKAO HALALI VYA CHAMA linatumika kama njia ya kuwaziba watu midomo! Ni ajabu CCM iliyojaa ma-conservatives angalau inavumilia maoni makali ya wananchama wao yanayotolewa dhidi ya chama chao na wakati mwingine dhidi ya viongozi! Hivi ni nani asiyejua kwamba Nape na Samuel Sitta walikuwa on transit kuelekea CCJ? Hata hivyo waliwavumulia . itakuwa ni ujinga kudhani kwamba uongozi wa juu wa chama na serikali hawakufahamu harakati hizo za akina Sitta!
Kuna Columnist mmoja kwenye gazeti la Raia Mwema anajiita MSOMAJI RAIA! Huyu jamaa huwa anaiponda wazi wazi serikali ya Kikwette! Na kwenye baadhi ya makala zake; huwa anamponda hata JK mwenyewe! Lakini whats so interesting, MSOMAJI RAIA ni wa ndani katika serikali ya Kikwete; namfahamu! Sasa ikiwa mtu wa kawaida kama mimi nafahamu whos MSOMAJI RAIA, itakuja kuwa KIkwette mwenyewe ambae amezungukwa na wana-intelejensia kadhaa kila Idara?! Hata hivyo, Kikwete anamvumilia MSOMAJI RAIA!
Huku Uswahilini kuna tabia Fulani imezoeleka kabisa! Unakuta mzazi analetewa mashitaka kwamba kijana wake amedokowa/ameiba mahali, au labda nyumba ya mtaa wa pili. Ni kawaida kukuta wazazi wanakuja juu, mithili ya moto wa kifuu kwamba mtoto wao anasingiziwa; KATU HAWEZI KUWA MWIZI. Wapo wanaofikia kusema hizo ni chuki tu utafikiri mzazi husika huwa anatembea na mwanae kila mahali! Siku wanakuja kutanabahi, anakuja kusikia kwamba Mwanao yupo Jela au kapigwa moto! Wazazi wa aina hii ndo mashabiki wengi wa CHADEMA walivyo! Wakati si Dr. Slaa wala Mbowe wana sifa za kuwa Malaika lakini wapenzi na mashabiki wa CHADEMA wanataka kufanya kama hawa watu ni MALAIKA ambao tunaambiwa huwa hawafanyi makosa!
Lililo wazi ni kwamba, mwanadamu pekee asiyefanya makosa ni MAITI! Youll never be free of mistakes unless if youre dead!
Kwa wanaojua hulka za akina Slaa na Mbowe hawezi kujiuliza maswali mengi kuhusu alichosema Mwigamba.Mkuu naona hoja yako ni ya kinadhalia zaidi, ingekuwa vizuri ungeweka na ka_substance kidogo,,, mfano ungetuweka bayana kuwa kwa mtazamo wako hili sakata la Mwigamba halikustahili kufuata VIKAO HALALI YA CHAMA kwa kuwa alichosema kwa mtazamo wako ni halali. Hapa namaanisha kuwa uhalali wa hoja yako utakuwepo tu kama alichosema Mwigamba ni cha kweli.
Maoni yangu ni kuwa kama mtu ana ushahidi wa kitu anachotaka kusema ni bora aseme hadharani bila kufuata vikao halali vya chama kwa kuwa ukweli huweka kila mtu huru. Siungi mkono mtu uko kikaoni na wenzako ambako ndio fursa ya kuwananga hapo hapo lakini unatumia jina bandia kutoa tuhuma unazodhani ni halali kwako. Utawala bora unakiukwa kama anayetekeleza utawala bora hafuati misingi ya uwazi.
Na ndivyo inavyostahili kipindi hiki kuliko wakati wowote.Marafiki wa maadui zetu na mifumo yao hawatapata nafasi.
Majenerali wakuu hawabadilishwi katikati ya vita
Kama CCM mna uchungu sana wachukueni mnaowataka wakagombee huko kwenu.Msitupangie aina ya silaha za kuwapiga nazo ninyi.
Mtaishia kulalama tu na kupoteza muda.Hampati kitu.So, go home
Ben hivi kwa nini unadhani mimi naichukia CHADEMA????!!Sio mara ya kwanza kusema haya hapa!!!
Kwa kumbukumbu tu mimi sijawahi,sio na wala siwezi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa ili niwe neutral na objective kuwakosoa,kushauri na kuwapongeza wote pale inastahili!!!!
Wewe umesoma na unajua criticisms huwa zinaenda kwa theory yenye mashiko ili kuiboresha, no body bothers to criticize a weak theory!!!! Kwa mtazamo huo jua kuwa we lie down critiques sababu nyie ndio second giant nchini!!!
Hebu jaribu siku moja kuwa msomaji tu humu jukwaan meanwhile umwambie afisa habari afanye yeye.hii kazi unayoifanya for that single day!!!!
Kama utajiridhisha yote yanayoandikwa humu ni hila,ujinga,upumbavu na uzandiki juu ya Chadema zibeni masikio na pamba muendelee na shughuli zenu!!!
Hivi ni kiko gani halali cha chama kilichompa Ben Saanane kazi ua uspy wa chama?
Chadema haiendeshwi kwa vikao wala katiba. Inaendeshwa kwa utashi wa wale walioianzisha.
KIkwete anaiongoza CCM kwa mkono wa Muwa muunge mkono.Dr.W.Slaa na Freeman A. Mbowe wanaiendesha Chadema kwa mkono wa chuma.
Critics hukosoa kwa hoja.Tumekua humu JF siku nyingi na kukosoana kwa hoja.Wewe unaweka mipasho na hatred attitude.Unachoandika humu mara nyingi ni hate speech!
Mkuu wangu kama ungenisoma vizuri ugegundua kwamba mimi siku-base suala la Samson Mwigamba bali nilichoangalia sana ni hii tabia ya viongozi wetu kutumia visingizio kama Katiba, Vikao Halali vya Chama and the like kama DEFENSIVE MECHANISM! HIZI ni ghiriba tu ambazo zimeenezwa kwenye Nyanja mbambali za jamii tangu enzi na enzi lakini lengo kuu likiwa ni kuwaziba midomo wana-jamii. Ni ghiriba ambazo zipo karne kwa karne, hazipo kwenye siasa pekee! Ghiliba za aina hii zipo kwenye masuala ya dini hadi kimila! Muislamu akihoji sana mambo ya dini yake ataambiwa anakufuru, Mkristo akihoji sana ataambiwa amepandwa na mapepo; na kama ni Mlokole ataambiwa "Ashindwe kwa Jina la Yesu!" Full ujanja ujanja kila mahali. Na hakuna shaka kabisa kwamba ni jamii yenye kuzing'amua ghiriba kama hizi tu ndizo pekee zinakuwa zenye ustawi bora! Akheri ya dini, tumeyakuta, tumeghiribiwa na tumeufyata! Sote hivi sasa tunaogopa kukufuru tusije kuchomwa moto wa milele! Enzi za utoto wetu ilikuwa tunaambiwa kwamba ukitaka kufahamu jinsi moto wa Jahanamu unavyovuma, basi ziba masikio yako kwa kutumia viganja vya mkono; INATISHA AISEE! Halafu ndo uambiwe utatupwa humo milele!Mkuu naona hoja yako ni ya kinadhalia zaidi, ingekuwa vizuri ungeweka na ka_substance kidogo,,, mfano ungetuweka bayana kuwa kwa mtazamo wako hili sakata la Mwigamba halikustahili kufuata VIKAO HALALI YA CHAMA kwa kuwa alichosema kwa mtazamo wako ni halali. Hapa namaanisha kuwa uhalali wa hoja yako utakuwepo tu kama alichosema Mwigamba ni cha kweli.
Maoni yangu ni kuwa kama mtu ana ushahidi wa kitu anachotaka kusema ni bora aseme hadharani bila kufuata vikao halali vya chama kwa kuwa ukweli huweka kila mtu huru. Siungi mkono mtu uko kikaoni na wenzako ambako ndio fursa ya kuwananga hapo hapo lakini unatumia jina bandia kutoa tuhuma unazodhani ni halali kwako. Utawala bora unakiukwa kama anayetekeleza utawala bora hafuati misingi ya uwazi.
Hapo kwenye RED ni moja ya hoja ambazo huwa zinaniacha hoi sana; "kuna mkono wa CCM!" Kila linalotokea, ni lazima waihusishe CCM as if wanachama na viongozi wa CHADEMA can easily be manipulated or placed a price on top of their integrity!! Kama ulivyosema, hiyo nayo ni aina nyingine ya kuziba watu midomo coz' mtu ukifunguka lazima uonekane umenunuliwa na CCM hata kama hakuna kitu kama hicho!Mkuu bora umeliona hili. Hapa kuna uwezekano mkubwa viongozi wakuu wa CHADEMA wanatumia falsafa ya kusema "kuna mkono wa CCM" ili kuweza kuficha maovu yao na kuwafunga mdomo wale ambao hawapendi mienendo yao.
mkuu tumeona unawamudu vyema ndo maana tunakuacha upambane nao hao buku 7 FC, kiongozi wao Ritz sijui kakimbilia wapi.
Ni kifungu Kipi nilichokiuka kikatiba?Mbona tangu nimekua JF hujawahi kuuliza kama mimi ni msemaji wa CHADEMA?Acheni woga.I'm here to stay.Siendi popote na nitaendeleza mapambano hata kama hamtaki
Ulitaka aisemee CCM chama cha ufisadi na rushwa?Mkuu, nimetafuta kitufe cha Like sijakiona. Hakina unastahili like yangu na umeongea jambo la maana sana. Yaani siku hizi Ben Saanane ndo amekuwa msemaji wa CHADEMA! Na haya anayojibu yamepitia vikao halali vya chama? Je haya ayasemayo Ben Saanane hayapingani na katiba ya chama?