CHADEMA na ACT Wazalendo tujuzane maana ya haki

Mtyela Kasanda

JF-Expert Member
Oct 13, 2018
554
818
Nyuzi nyingi humu zinaomba haki, na ukisoma zaidi ni haki ya wabunge wa upinzani kuchaguliwa. Sasa haki maana yake nini? CCM hawana haki ya kuchaguliwa? Kwanini isiwe CCM ambao wana wanachama wengi kwa ujumla kuzidi wapinzani wote kwa pamoja?

Au haki imepata maana mpya, maana ya kuchagua wapinzani tu bila CCM?

Kama mgombea wa upinzani ni mgombea ubunge na baadala ya kupiga kampeni kwenye jimbo lake (Zitto Kabwe) anatembea nchi nzima kunadi wagombea wengine ingekuwa ajabu ashinde yeye dhidi ya mgombea anaefanya kampeni jimboni masaa 24, au ni haki ya mpinzani kushinda kwakua yeye ni mpinzani tu?
 
Yafuatayo siyo haki:

1. Kuengua wagombea wa upinzani ili ccm wapite bila kupingwa i.e wabunge wa NEC

2. Wagombea wa upinzani kukamatwa siku ya kurudisha form ili muda upite na wakose sifa za kugombea!

3. Wakurugenzi kugoma kuapisha mawakala wa upinzani na kwingine kuzikimbia ofisi ili wasiwepo kabisa na hivyo upinzani kukosa mawakala!

4. Kuzuia au kwaondoa mawakala wa upinzani kwenye vituo vya kupigia kura!

5. NEC kumfungia Lissu wakati huo huo kumuacha JPM ambaye amekiuka kanuni nyingi za uchaguzi wakati wa kampeni ikiwemo kutoa pesa akiwa majukwaani kwa ajili ya miradi,hii ni rushwa!

6.Udanganyifu kwenye majumuisho kura,haiingii akilini majimbo mawili tofauti JPM apate kura hizo hizo na Lissu apate kura hizo hizo!

Hayo siyo haki ndani ya uchaguzi!

Nje ya uchaguzi:
  • Akina Nusrat Henje ni zaidi ya miezi minne wako mahabusu bila dhamana kwa kuimba "Mungu ibariki Chadema",wakati huo huo Uvccm wanapeta tu japo na wao waliimba "Mungu mbariki Magufuli"!Hapo hakuna haki bali uonevu wa wazi!
  • Siyo haki kwa CCM kufanya siasa peke yake wakati vyama vingine vikifungwa pingu kwa miaka 5!
Nk
 
Kuchaguliwa kwenyewe kwa wabunge wa ccm.

Screenshot_20201101-101529.jpg
 
Nijuavyo mimi maana ya haki ni VIONGOZI wa upinzani kukaa madarakani kwa muda mrefu bila ya kuwapa haki wengine nao waongoze. Kuna viongozi wameng'ang"ania madaraka tokea mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa hapa nchini Tz.
 
Nyuzi nyingi humu zinaomba haki, na ukisoma zaidi ni haki ya wabunge wa upinzani kuchaguliwa. Sasa haki maana yake nini? CCM hawana haki ya kuchaguliwa? Kwanini isiwe CCM ambao wana wanachama wengi kwa ujumla kuzidi wapinzani wote kwa pamoja?

Au haki imepata maana mpya, maana ya kuchagua wapinzani tu bila CCM?

Kama mgombea wa upinzani ni mgombea ubunge na baadala ya kupiga kampeni kwenye jimbo lake (Zitto Kabwe) anatembea nchi nzima kunadi wagombea wengine ingekua ajabu ashinde yeye dhidi ya mgombea anaefanya kampeni jimboni masaa 24, au ni haki ya mpinzani kushinda kwakua yeye ni mpinzani tu?
Huenda hata wao hawajua wanacho kidai
 
Jifunze Kenya

Back
Top Bottom