dolevaby
JF-Expert Member
- Aug 25, 2013
- 12,956
- 9,482
Membe hana ushawishi wowote zaidi ya wapiga Kura wachache pale Mtama na wengi wao kule ni ccm kumbuka Nape atagombea piaHuu muungano kwenye kura za urais na mgombea urais ndipo penye walakini.
Kiukweli kwangu Membe sioni influence yake kabisa ukiacha hiyo mikoa ya kusini, sasa kipi bora;
(a) Kumsimamisha Membe asaidie wagombea ubunge mikoa ya kusini ambayo hatuna uhakika kama kweli ana hiyo influence?
Au
(b) Chadema imsimamishe mgombea urais wake ambae inaamini anaungwa mkono na kundi kubwa la watu Tanzania nzima kwa ujumla, na sio kanda fulani pekee?
Mleta mada umejaribu kusisitiza kwenye umoja ni vizuri, lakini pia tuangalie kwa jicho la pili nguvu za wagombea hasa wa Urais kutoka vyama vyote viwili, tusilazimishe tu bora fulani ana jina basi apewe hiyo nafasi, napenda hapa tutazame zaidi nguvu/uungwaji mkono wa wagombea wa hivyo vyama viwili.