Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoani Mwanza kupitia Viongozi wa Chadema wilaya ya Ilemela wamesema mtu anayeitwa Robert Gwanchele aliyetoa taarifa ya kupinga maamuzi ya Kamati kuu jana siyo kiongozi ndani ya chama na kwamba amefanya hivyo kwa kutumiwa na watu ambao ni wapinzani wa Chadema.
Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Ilemela, Damas Kimenyi na Katibu Froling Rwela, wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti walisema Gwanchele siyo kiongozi ndani ya chama na hata cheo cha Mwenyekiti wa Vijana Kanda ya Ziwa Magharibu hakipo ndani ya chama.
Walisema Gwanchele alikuwa Katibu wa Chadema kata ya Nyamanolo lakini alivuliwa wadhifa huo mwaka 2011 baada ya kubainika alikuwa akitumiwa kukihujumu chama na hivyo kubakia kuwa mwanachama wa kawaida.
"Ndani ya chama Mwenyekiti wa Kanda ya Ziwa Magharibi ambaye ni Peter Mekele, Katibu ni Renatus Bujiko, kwa hiyo cheo cha Mwenyekiti wa Vijana wa Kanda ya Ziwa Magharibi hakipo katika Chadema, taarifa aliyoitoa anatumiwa na CCM," walisema.
Viongozi hao walisema kuwa Chadema wilaya ya Ilemela na mkoa wa Mwanza kwa ujumla ilishatoa taarifa ya kuunga mkono uamuzi uliotolewa na Kamati Kuu ya kuwavua nyadhifa Zitto na Dk. Mkumbo.
Zitto na Dk. Mkumbo walivuliwa nyadhifa zao wiki iliyopita kwa kile kilichodaiwa wamekisaliti chama kwa kuandaa 'Waraka wa Mabadiliko mwaka 2013' ambao ulilenga kuandaa mtandao wa ushindi kwenye uchaguzi wa ndani ya chama mwakani.
Source:Nipashe Jumatatu.

Wana JF mambo?. Muda mfupi uliopita, viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakishirikiana na viongozi wa chama ngazi ya Kanda ya Ziwa Magharibi na Taifa kwa ujumla, wametoa tamko kali la kukanusha taarifa zilizoitwa za 'kipuuzi na kihuni', zilizotolewa jana na Robert Gwanchele kuzuia Mbowe na Dk. Slaa wasikanyage Mwanza!.
Katika tamko hilo lenye ukurasa mmoja, limesainiwa na mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Nyamagana, Nestory Sukari pamoja na katibu wa chama wilaya hiyo, Fred Lukanga, linasema: "Waliotangaza zuio hilo, Chama hakiwatambui". Pia wamejibu maswali ya waandishi waliotaka kujua Gwanchele ni nani ndani ya Chadema, ambapo mwenyekiti wa chama Nyamagana, Sukari alisema: "Kwanza Chadema haina kitengo wala nafasi ya uongozi wa Vijana ngazi ya Kanda ya Ziwa, wala Umoja wa Matawi Mkoa wa Mwanza. Waliotoa tamko hilo ni wahuni.
Katibu wa Mbunge wa Nyamagana, Robert Mwinamila naye akaongeza kwa kusema: "Hao vijana waliotoa tamko jana yawezekana ni wagonjwa wa akili, na wanapaswa kupelekwa hospitali ya Mirembe wakapimwe akili. Unapoona mtu mwenye kichaa anaanguka anguka ovyo, anatakiwa awahishwe haraka hospitalini, maana ipo siku ataangukia moto". Ila Chadema kimeapa kuchukuwa hatua za kisheria dhidi ya Gwanchele maana amejiita ni kiongozi wa Chama wakati akijua siyo kweli na alishahamia chama cha ADC. Tamko halisi nitawaleteeni muda si mrefu waungwana!.