Chadema Mwanza inahesabu siku za uhai wake trust me.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Mwanza inahesabu siku za uhai wake trust me....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by security guard, Aug 30, 2012.

 1. s

  security guard JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 80
  MFADHILI MKUU WA CHADEMA SENGEREMA AHAMIA CCM
  MLEZI na Mfadhili Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jimbo la Sengerema, mkoani Mwanza, Bw. Alex Manji, ametangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  Bw. Manji ambaye hivi karibuni alitangaza kuwania ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA, katika Uchaguzi Mkuu ujao, alifikia uamuzi huo kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Jumuiya ya Wazazi wa CCM, wilayani hapa, uliofanyia jana.

  Alisema hajashawishiwa na mtu kukihama chama hicho bali amebaini kuwa kuendelea kukaa huko ni sawa na kupoteza muda wake kwani CCM ndio chama kilichomlea tangu utoto wake.

  “Nimeamua kurudi nyumbani CCM kwa hiari yangu, nitakuwa bega kwa bega na wanachama wote kuhakikisha tunaisambaratisha CHADEMA hapa Sengerema.

  “Ninaijua vizuri CHADEMA kwa sababu nimekuwa mdhamini wao mkuu katika jimbo hili,’’ alisema Bw. Manji ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Nyampulukano.

  Katika mkutano huo, Bw. Manji alipewa kadi yenye namba 0136371 iliyotolewa Novemba 5,2010, na mgeni rasmi Kamanda wa Vijana wa CCM wilayani hapa, Bw. William Ngeleja, ambaye alisema uamuzi aliochukua ni wa busara na unastahili kupongezwa.

  Akizungumzia uchaguzi huo, Mbunge wa jimbo hilo, Bw. William Ngeleja, aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuchagua viongozi ambao watasaidia kuimarisha chama katika Uchaguzi Mkuu ujao.

  “Ndugu wajumbe, naomba tuwe makini tunapochagua viongozi ambao watakuwa msingi imara wa chama chetu huko tunakokwenda ili tuendelee kuwatumikia wananchi,” alisema.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Bw. Jaji Tasinga, aliwataka wajumbe wa mkutano huo wajitokeze kwa wingi kutoa maoni yao kwenye tume ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya.
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi,CHADEMA HAIMTEGEMEI MTU MMOJA.
   
 3. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chadema ipo imara hata kama akiondoka wilbroad Slaa!!Kwanza huyu mwenyewe alikua amekaa kwenye ncha ya msumari maana hata jina lake hastahili kuwa chadema et Manji!!Fisadi wapi na wapi na chadema?Alihama Shitambala itakua manji na pia kumbuka chadema haihitaji kuwa hata na wanachama ila wakati wa uchaguzi ndo utaijua kama inakubalika au haikubaliki Uliza igunga Chezea M4C wewe
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa, inategemea koo tofauti kama akina Mbowe, Mtei, Ndesamburo, Lema, malizia...
   
 5. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Jina lake tu utata ALEX halafu ubini uwe MANJI fulu maigizo.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  .....Arfi, Safari, Marando, Mbilinyi, Wenje, Msigwa, Zitto nk. Hivi nyie watu wa Nepi ni lazima mlete uharo hapa ili mjihakikishie posho zenu? kweli ufisadi hauwezi kuisha chini ya magambaz!!!
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mbona Mzee wa mipasho umemsahau?
   
 8. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenena vema sana, Mangamba akili zao ni fupi sana, wakati Chadema inajegwa kwa moyo ya collective mass (umma) ccm inajengwa individuals (Mfadhili) fulani fulani matokei yake wanabaki kuwatukuza
  Naamini huyo manji alikuwa anakitu anavizia chadema sasa hajakipita na huenda amehaidiwa huko alikokimbilia.
   
 9. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Sababu nyingine, eti chama kilichomlea, ngoja akafie huko.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ah yes!! Mzee wa mipasho J.S. Wote hao niliotaja imethibitishwa wanatoka Mkoa wa Kili!!!! Magambaz mnachekesha kweli!!! You are sinking fast!!!
   
 11. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Bora aondoke alikuwa anafikiri CDM wanalea mafisadi? Alikuwa anamiliki mafuso akafikiri CDM watakuwa wanayakodi kubebea watu Kama ilivyo ccm Kumbe watu wanaenda kwenye Mikutano wenyewe. amerudi ccm ili awakodishie aliula wa chuya CDM
   
 12. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  NYIE WAPUUZI KWELI IVI ATI MANJI WA UKO SENGEREMA NDO MFADHILI WA CDM? AWA MAPANDIKIZI TU FRM CCM WAMESHINDWA KUFIT CDM, USICHEZE NA M4C, MFADHILI WA CDM NI WANANCHI NA C UYO MANJ WENU, AFTERALL ANA KURA MOJA TU WAKAT TNAVUNA MAMIA YA WANACCM KUINGIA CDM KILA KUKICHa
   
 13. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa taarifa yako mtu anayehama CDM kurudi CCM hana jipya kwa waTz. Mtu akitoka cdm akaenda TLP au cuf tutamfikiria!
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  JS ndio nani? Josephine Slaa?
   
 15. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Oil chafu?
   
 16. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu bado haujawa na hoja hata yenye viashiria kua cdm itayumba Mwanza!kwani huyo Manji ndio kabeba wana Cdm wote Mwanza?angalia kauli na hata jina lake utajua kua ni mtu hasiye jitambua,kauli kama C.c.m ndio imenilea na ilo jina lake eti Alex "Manji" utajua tu ni mtu mwenye iq ya aina gani,CDM wanataka wawakilishi wa wananchi wawe smart kwa maana ya upeo,sasa huyo bwana "Manji" ameshajua hatopitishwa na Cdm 2015 kugombea ubunge ndio maana kaona bora arejee kwy vilaza wenzake maana watamfikiria!
   
 17. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #17
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hakuna mwanasiasa aliyekuwa upinzani akarudi ccm akaendelea kuwa mwanasiasa !
   
 18. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sio oil chafu bali ni Ecoli=kinyesi
   
 19. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Kweli? Vipi kuhusu Tyson, Lusinde, Malima na Kitwanga?
   
 20. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Sera za CDM JF tumezizoea.
   
Loading...