CHADEMA mtamkumbuka Zitto na Slaa, CUF hawataisahau CHADEMA

Haya ndugu zangu, uchaguzi umeisha. Tuungane kuijenga ACT, ndio kimbilio lilobaki kwetu wapenda mabadiliko. Magufuli 2015 tumempa kwa sababu hatukuwa na mbadala. 2020 is for Zitto, shime tuungane kwa nguvu moja tujiandae kwa uchaguzi ujao.

Ha! ha! ha! unachekesha sana. Sasa kwa taarifa yako ACT itabidi ingojee miaka 20 ijayo ndipo ianze kufurukuta. Wewe unadhani kujenga chama ni lele mama? Mmesimamisha wagombea zaidi ya 200, mmepata kiti kimoja tu cha ubunge. Nenda pole, safari bado ni ndeeeefu sana.
 
Data zako unazipata wapi? so far CHADEMA wamepata majimbo mengi kuliko 2010 ... CUF wamefanya Vema sana na sasa wanachukua Zanzibar Rasmi ... Tanganyika inakuja kwa kasi ya ajabu
 
ila zito ni kiboko aiseevkachukua jimbo na madiwani kibaoo

kachukulia wapi hizo ward ? ni kwao kigoma ningeona yupo vizuri kama hata yule mbunge aliye mfuata kapata pia......na ameshinda kwa kura kidogo tu elfu 30 kati ya kula elfu 90 nafikiri
 
Mpaka sasa matokeo ya kweli yanaonyesha Lowassa anaongoza akifuatiwa na Magufuli.
 
We uko wapi huoni majimbo wanayoshinda CHADEMA,CUF yalivyo mengi tena mikoa yote
 
Haya ndugu zangu, uchaguzi umeisha. Tuungane kuijenga ACT, ndio kimbilio lilobaki kwetu wapenda mabadiliko. Magufuli 2015 tumempa kwa sababu hatukuwa na mbadala. 2020 is for Zitto, shime tuungane kwa nguvu moja tujiandae kwa uchaguzi ujao.

Act ikishakuwa tishio itaandamwa hadi ipotee kwenye siasa za TZ na kama unabisha vuta subira
 
hayo majimbo sio kwamba CUF walikuwa hawashindi bali ccm walikuwa wanaiba!

Cuf wametwaa viti 7 bara kwa mara ya kwanza ...sasa wamefaidika na ushirikiano. Tena kikiwemo kiti kikubwa cha Tanga mjini na mtwara mjini....
 
Kwa mwenendo wa matokeo rasmi viti vya ubunge tayari CHADEMA yaelekea kupoteza viti vingi vya ubunge pamoja na udiwani hii inaonyesha wazi umahiri wa Zitto kabwe na Dr. Slaa walivyofanya kazi kubwa kwa kutumia upeo wao mkubwa wa ushawishi wa kisiasa kuipa mafanikio makubwa CHADEMA katika uchaguzi uliopita 2010 na kujizolea majimbo mengi ya ubunge na udiwani.

Lakini kama ilivyo chadema ya akina Mbowe inamalengo yake maalumu kwa watu maalumu.na ktk kuelekea kutimiza malengo yake huwatumia wale political genius kama kijiko cha jikoni Kuwavusha point A kwenda point B baadaye huwajengea zengwe ili iwafukuze au waj iengue wenyewe na wakati mwingine huisiwa kutumika hata njia za kimafya ili kuwaweka pembeni kama ilivyo jiri kwa Chacha wangwe, Dr.Kaburu, Zitto kabwe, hatimaye Dr. Slaa hawa kila mmoja alipewa sehemu yake ya kazi na wamiliki wa CHADEMA pasi na wawo kujitambua. wakisaidiwa pembeni na vuvuzela akina Tundulisu na Mnyika. ili kusafisha njia mtoto wao Mbowe aingie Ikulu kirahisi. Kazi hiyo waliifanya na Slaa akawafikisha ktk geti la Ikulu.

Master plan akaona itakua ni vigumu sana kumuengua slaa kama atafanikiwa kuingia ikulu kwa sababu mzizi wake ktk chama ni wahatari kwa hiyo hapa kuvuka kuingia ikulu lazima apatikane mtu ambaye anaushawishi wa kisiasa lakini hana mzizi ktk chama ili tukisha ingia ikulu iwe rahisi kumuosha kwa bahti isiyotegemewa akapatikana Luwasa tena akawa ni jiwe moja kwa ndege wawili,kwanza ni fimbo ya kumfukuzia Dr,slaa pili ni lift ya kuwaingiza ikulu.tatu kuachia nafasi ni rahisi mno kwa mujibu wa afya yake.

Cuf nawo wakazuguushwa ukuti ukuti bila kujua wakatumika kama petroli ya kuchochea gari la kuipeleka Chadema ikulu bila wawo kutanabahi kuwa kwa mchezo huo baada ya uchaguzi watakufa kifo cha mende mbendembende miguu juu. nafasi yao ya 3 huku bara inachukuliwa na ACT Wazalendo, HEKO ZITTO.

Hii ndio move waliocheza Chadema's master mind. kwa bahati mbaya mkanda umeungua ikulu hakuingiliki na uwakilishi mkubwa wa ubunge na udiwani umetoweka.

Move kama hii Jems hardly chess huiita THE WAY THE COOKIE CRUMBLES. Kwa wale wasomi wa zamani wa novel wanajua.

Sasa hivi cdm wameshapata majimbo zaidi ya 30 wewe bado unatumika na Nape.
 
Ha! ha! ha! unachekesha sana. Sasa kwa taarifa yako ACT itabidi ingojee miaka 20 ijayo ndipo ianze kufurukuta. Wewe unadhani kujenga chama ni lele mama? Mmesimamisha wagombea zaidi ya 200, mmepata kiti kimoja tu cha ubunge. Nenda pole, safari bado ni ndeeeefu sana.

hao 200 wamtokea wapi? kuna vijiji vya moshi mgombea wa ACT anapata kura 600?? unaona kitu kidogo?

ndio mnanyimwa nchi kwa akili kama hizi.....hutaki mabadiliko kisa eti kujenga kunachukua miaka mingi??

CCM nao wanasema kuwapa upinzani nchi bado sana..............

yaani chuki inakupofusha
 
Back
Top Bottom