Wenye tamaa wameitumia sana chadema. Siyo kweli kwamba unaweza kuhama vyama tu kama vile ni club ya mpira ama ngoma ya mdundiko! Vyama vinajengwa kwa falsafa nk. Ni mambo mengi yanayomfanya mtu kuwa mwananchama wa chama Fulani, especially vya kisiasa! Kuna kada wa ccm aligusia hilo, na mimi nakubaliana na baadhi ya hoja zake. Hata Dr. Slaa nilishangazwa sana na hatua yake!Nikaweza kuconclude moja kwa moja kuwa wengi wameitumia chadema kwa maslahi yao binafsi…Hilo nina ushahidi nalo wa mojakwa moja, wengi waliotoka chadema, wameenda kupewa vyeo!Siyo tu Dr.Mihogo, pale yule Shonza, Mwampamba na hawa wengine wa juzi hapa kina Mwita!
Kuna sehemu ambazo ilikuwa hata kama ukiweka jiwe, almuradi ni chadema litapita.Kuna waliotake advantage ya hiyo kitu ili tu wapate kura za wananchi, lakini ndani ya mioyo yao ni mafisi wanafiki na walafi wa madaraka! Stori utakazosikia wakipiga ni kiasi gani cha pesa watapata wakigombea either udiwani au ubunge!
Wajinga wengine utasikia eti “Ilipangwa toka tumboni aitwe muheshimiwa”, huyu ni mpumbavu ambaye alikuwa akimtetea yule Mwita aliyejitoa halafu akapewa cheo na jiwe! CDM sijui mtajipanga vipi kuwatambuwa hao watu ambao ni sawa na mafisi wenye ngozi ya kondoo? Ili msirudie makossa?Mimi nadhani mlishaanza vibaya! Mliwafuatiliza sana ccm, na kwasababu kulikuwa na upepo wa wananchi kuwapenda, mkajisahau, mkaachia hadi mafisi ndani yenye tamaa tu za madaraka!
Wameitumia chadema kwasababu ninaamini wasingeweza kupata nafasi walizonazo wala kukubalika na wananchi kama wangeenda kwa gia ya ccm! Kwanza wasingepata hata hiyo nafasi ya kugombea chochote ndani ya ccm, ccm ina wenye bhan! Kupewa kwao nafasi baada ya kujindoa chadema, kunaonyesha wazi kuwa walikuwa ndani ya chama kwa maslahi yao binafsi kama vile uongozi, pesa nk. Pia inaoyesha ilikuwa ni "Quid pro quo", yani ni makubaliano ya kutoa kitu flani ili upewe kitu flani, nipe nikupe... Hakuna mzalendo hata mmoja! Dr. Slaa ambaye ndo nilikuwa nikimuamini Zaidi kwa uzalendo, ndiye aliyenithibitishia hoja yangu kabisa! Kapewa ubalozi katulia tulii! Ndo hapo sasa uyajiuliza nia yake haswa kwa Taifa ilikuwa ipi? Lakini chadema ni taaisi imara kabisa!
Kwanini nasema ni taasisi imara?
Baada ya misukosuko yote, kuanzia mkuu wa nchi kuminya demokrasia ikiwa ni pamoja na kuwakataza chadema na upizani kwa ujumla wasifanye shghuli za kisiasa hadi wakati wa uchaguzi, na wakati wao wakiendelea na siasa ni jambo la ajabu sana! Hata rais Obama alizungumzia hilo jambo la kuminya demokrasia kwa kuwaweka wapinzania ndani au kuwakataza kufanya shughuli za kisiasa, huku wakidai kwamba kuna uchaguzi huru na demokrasia! Uongo mtupu! Pamoja na hayo yote, chadema haijafa!
Baada ya kuona ndoto yao ya chadema kufa haijatimia, eti wanajifanya sasa wao ndo washauri wakuu wa kusema eti mwenyekiti hafai! Kama mngeweza kuiuwa chadema ndo mngekuja na hiyo hoja, mmeshindwa, sasa ni kama mnaomba poo kiaina!
Hata Urusi, wananchi wake ilikuwa wamuondoe Putin madarakani, shida ilikuja pale wananchi walipoona marekani wanafurahia na kuendelea kuwashauri kuwa Putin hafai kuendelea kuiongoza URUSI!!Wakaona hadi yule mama Clinton akiwasapoti hao wanaonyanyaswa na Putin! Pamoja na kwamba waliona ni kweli Putin ni dikteta, bado walikuwa na mashaka kwasababu marekani nao wanamuona Putin kuwa ni mbaya, walikataa kukubalina na adui yao! Sasa kwanini nyie magamba mnataka wanachama wa cdm wakubaline na ujinga wenu eti kuwa Mbowe hafai kuongoza chadema?
Hayohayo yameshatokea kule Iran! Wale wananchi wamechoshwa na mahayatollah, lakini shida ni mmarekani, haijalishi uzuri wa jambo lile au manufaa yake kwa hao wananchi, kama linasapotiwa na adui wako, hilo ni jambo la kutizama kwa jicho la tatu! Halafu humu wasiojielewa, au wenye kumbukumbu fupi, wanaleta hoja za kuwa Mbowe ajiuzulu.Mimi naona ni kama wajinga waliobobea kwenye ujinga wao!