Siyo lazima chama cha upinzani kiitwe CHADEMA, chochote kinaweza kuwa chama cha upinzani ili mradi tu hakina viongozi wapenda madaraka, madikteta, wafuja mali za chama, wanaorusha ngumi pale wanapoambiwa ukweli.
::::::::::::::::::::::::
Hii inanikumbusha enzi za NCCR
Mageuzi ilianza hivi hivi.
Ni wazi kabisa CCM haijazoea
kukabiliana na upinzani mkubwa /
mkali kwa mwongo mmoja(vipindi
viwili vya uchaguzi).Mwaka 1995
NCCR Mageuzi waliisumbua sana CCM
walichofanya ni kuisambaratisha
kabla ya uchaguzi wa mwaka
2000.Mwaka 2010 Dr Slaa wa CDM
aliwasumbua sana wasingependa
kuingia uchaguzi wa mwaka 2015 huku
CDM wakizidi kujitanua kila uchao
wakijua wazi watakuwa na mgombea
mpya asikuwa na nguvu za kidola
ambaye anaweza kupambana na mgombea
mwenye rekodi nzuri na mwenye mtaji
mkubwa wa kura za mwaka 2010.CCM
wanajua wazi baada ya uchaguzi mkuu
uliopita CDM haikulala bali
walianzisha programs maalum M4C
ambayo ilihakikisha inawafikia
wapiga kura wengi kabla ya uchaguzi
mkuu ujao.
CDM wakiweza kushinda mtihani ulio
mbele yao ni wazi uchaguzi mkuu
ujao itabidi CCM wajiandae kwa
kumweka mgombea mwenye rekodi nzuri
ya uadilifu.CCM isingependa
kuchagua mgombea mzuri kwasababu ya
kitisho cha CDM kuzidi kujiongezea
umaharufu.Warasimu wa CCM
wangependa kumchagua mgombea
atakayelinda uchafu (maslahi) wao
ili linaweza kuepukwa iwapo CDM
itasambaratishwa.
Kwa afya na ustawi wa taifa letu
tusikubali CDM ikasambaratishwa
itatuchukua miaka mingine 15 kujenga
upinzani mwingine wenye nguvu huku
tukiwaachia walafi/wezi wakitafuna
na kutuibia rasilimali
zetu.Tusisahau Mzee Mkapa
alivyofanya baada ya kusambaratika
kwa NCCR Mageuzi.Mabenk yaliuzwa
kwa bei ya kutupa,madini,mashirika
ya umma,EPA,Meremeta zote
zilisababishwa na ukosefu wa
upinzani wa maana ulioanza
kujengeka enzi hizo.