CHADEMA, mliamini katika ubatili. Ile ndiyo CCM ya Magufuli!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Nasisambaza pole kwa Mbowe, Mnyika, Lowassa,Lissu na Msigwa kwa 'vipigo' walivyopokea katika uchaguzi mdogo wa Madiwani. Tena wamepigwa nyumbani kwao,yaani, katika majimbo yao. Poleni sana CHADEMA mlioamini katika ubatili.

Yaani kwa akili zenu mliamini kabisa kuwa katika Kata ambazo Madiwani wenu walijiuzulu 'kwa kumuunga mkono Rais Magufuli' mtashinda? Mshinde ili Madiwani 'wanunuliwe' tena na tena? Hakukuwa na nafasi ya mchezo wa kuigiza kama huo. Lazima CCM iibuke kidedea!

Ukiachilia mbali Kata ambazo Madiwani wake walifariki au kufungwa jela, isingewezekana kwa kata ambazo Madiwani wake walijiuzulu zirerejee kwenu wapinzani hasa CHADEMA. Halafu, CCM lazima ipendwe kanda zote na sehemu zote za Tanzania. Ni lazima!

Hizo ni rasharasha, mvua kamili ni 2020. Ile ndiyo CCM katika ubora wake. Unabembelezwa, ukikataa unaelekezwa!

Kujenga hoja bila ya bunduki na kamatakamata itapendeza!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kibiti, Pwani)
 
Bora umeongea ukweli.Naona sasa hivi hata kichwa huinui kwa jinsi uanvyoona haya na vibaya.Yule kijana wako naona kakupiga maswali na madongo mpaka umemfukuza jana arudi chuoni.

Nasikia umemtishia ati unamnyima ADA na vinginevyo utamtupa Sentro ya Stasheni pale.

Yote tisa Hongereni kwa kushindwa kwa kishindo
 
Nasisambaza pole kwa Mbowe, Mnyika, Lowassa,Lissu na Msigwa kwa 'vipigo' walivyopokea katika uchaguzi mdogo wa Madiwani. Tena wamepigwa nyumbani kwao,yaani, katika majimbo yao. Poleni sana CHADEMA mlioamini katika ubatili.

Yaani kwa akili zenu mliamini kabisa kuwa katika Kata ambazo Madiwani wenu walijiuzulu 'kwa kumuunga mkono Rais Magufuli' mtashinda? Mshinde ili Madiwani 'wanunuliwe' tena na tena? Hakukuwa na nafasi ya mchezo wa kuigiza kama huo. Lazima CCM iibuke kidedea!

Ukiachilia mbali Kata ambazo Madiwani wake walifariki au kufungwa jela, isingewezekana kwa kata ambazo Madiwani wake walijiuzulu zirerejee kwenu wapinzani hasa CHADEMA. Halafu, CCM lazima ipendwe kanda zote na sehemu zote za Tanzania. Ni lazima!

Hizo ni rasharasha, mvua kamili ni 2020. Ile ndiyo CCM katika ubora wake. Unabembelezwa, ukikataa unaelekezwa!

Kujenga hoja bila ya bunduki na kamatakamata itapendeza!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kibiti, Pwani)
Uchaguzi ulitawaliwa na vurugu, mawakala wa cdm walipigwa na kuamrishwa kutoka nje kwenye vituo vya kuhesabu kura...
Magu aliwaambia wakurugenzi kuwa anawapa magari,halafu asikie wakitangaza kuwa ccm imeshindwa..
Hivi kweli kwa kauli hiyo ni kwa nini wizi usifanyike?
Huu siyo uchaguzi, na wala hakuna mpenda demokrasia na mwenye akili timamu hata mmoja atakeyeshangilia eti ushindi wa ccm...
Ccm imetumia mabavu ili ionekane inapendwa, ila ukweli ni kuwa haipendwi ni wizi tu!
 
Huwa siwaelewi vyama vya upinzani vinaikubaliaje Tume ya uchaguzi kuwatumia wakurugenzi wa halmashauri kama wasimamizi wakuu wa uchaguzi wakati wote ni makada wa chama shindani?
Ni hivi lazima mshindwe tu na mtashindwa zaidi hadi hapo mtakapo kataa huu upuuzi wa NEC
 
Uchaguzi ulitawaliwa na vurugu, mawakala wa cdm walipigwa na kuamrishwa kutoka nje kwenye vituo vya kuhesabu kura...
Magu aliwaambia wakurugenzi kuwa anawapa magari,halafu asikie wakitangaza kuwa ccm imeshindwa..
Hivi kweli kwa kauli hiyo ni kwa nini wizi usifanyike?
Huu siyo uchaguzi, na wala hakuna mpenda demokrasia na mwenye akili timamu hata mmoja atakeyeshangilia eti ushindi wa ccm...
Ccm imetumia mabavu ili ionekane inapendwa, ila ukweli ni kuwa haipendwi ni wizi tu!
Mkuu mfia maji haishiwi kutapatapa....kama unavielelezo Kamili nakushauri uende mahakamani ukashtaki naamini haki itapatikana
 
Matusi yanatoka wapi aisee Mbona mimi sijakutukana....huna point bora ukae kimya tu. Kuliko kujidhalilisha ivo
Wewe una point gani?
Kwa nini usingepita kimya kimya...?
Kuna tusi kubwa nlilokutukana zaidi ya huu uhuni wenu mliofanya...?
Sioni ajabu kujidhalilisha kwa kukuita zwazwa...wewe ni zwazwa tu!
ab282743d4d896e39f6920e2c5a42eb8.jpg
 
Chadema msipokuwa na plan B msitegemee kuchukua nchi kirahisi, wenzenu hawahitaji hoja tena ila ni mwendo wa utemi tu... Kubweka hakuwezi kuwasaidia tena Chadema maana CCM wenye dola wameamua kutumia mbinu ya ubabe maana wanajua watanzania ni waoga..

Ni vizuri tukaamua tu kuachana na siasa na kusiwepo na vyama kama hatuna plan B zaidi ya hii ya kubweka kama mambwa koko bila madhara.

PLAN B IKO WAPI MAKAMANDA KAMA TUNAJUA KABISA TUNAONEWA NA DHAHIRI WENYE NCHI NDIO WAMEAMUA HIVYO KUYAFANYA HAYA MCHANA??
 
Hii ni rasharasha, kwa hiyo 2020 mtaingia na vifaru vituo vya kuhesabia kura? Maana hii tu mmeingia na visu, nondo huku mkilindwa na polisi
 
Aliyoyasema Lissu yanaonekana; kila mpinzani ni adui; hatuna tofauti na Rwanda; Uganda na Burundi ; dhambi ya ubaguzi aliyotabiri Mwalimu sasa imetimia; tumegawanyika tayari.
 
Back
Top Bottom