Tatizo kubwa ni kuwafunga mdomo CHADEMA kuzungumzia na kukemea ufisadi. Sasa CCM inajifanya ndiyo inayopambana na ufisadi kutokana na CHADEMA kuzibwa mdomo.
CCM wamefanikiwa kutengeneza wapinzani from within ili kupunguza nguvu ya upinzani wa nje ambao ni uncontrollable ....wanazi wa Chadema wanapenda kushangilia kila mwenye hoja kinyume na serikali na kuwapa umaarufu wa bure badala ya kujua hoja ni ipi na msimamo wa chama ni upi ili upande wowote hata kama ni serikali wakiwa na hoja ambayo ni agenda yao wanaungana nao ....haiwezekani mkawa mnapinga agenda zote za serikali ....ipo siku nchi itavamiwa na mtaipinga serikali kutuma jeshi dhidi ya wavamizi ...
Kwaiyo mpka leo hujui kama chama kimeyumba kuondoka slaa poleUmekosea mayalla adui mkuu wa upinzani ni FISIEM Hawa wengine ni wamekumbwa na mifadhaiko hawawezi na hawatoweza kuiyumbisha cdm. Kaondoka kigogo slaa je umekionaje chama kimeyumba?
Chama hakiwezi kuendelea kwa kununua wanachama ona fisiem wanavohangaika kaondoka Nyalandu tazama idadi ya wanaowarubuni imefikia ngapiii... ukipata jibu hapo ndo ujue Nyalandu ananguvu ya idadi hiyo wanayonunua mpaka ifikie idadi YA MAUMIVU YA KUKIMBIWA na MH. NYALANDU nnaimani NYALANDU atakuwa mbali na hawatomfikia.
watambue kuwa kila kichwa watakachofika bei ndio sawa na gharama ya kumrudisha NYALANDU kama fisiem watammaind.
at first place.CHADEMA haikupaswa kamwe kuanza kujilinda kuhusu tuhuma za ufisadi.Technically ni kosa kubwa sana..labda Lowassa ndiyo hawezi kujibu hoja ya ufisadi, lakini sioni kwanini wana cdm wengine washindwe.
at first place.CHADEMA haikupaswa kamwe kuanza kujilinda kuhusu tuhuma za ufisadi.Technically ni kosa kubwa sana
Never, unataka kusema tanzania hii kuna anayeyaona hayo, never, ni njaa zinawasukuma kuondoka. Mbaya katika Tanzania hii ni Lowasa, Fisadi kuliko wote ni Lowasa (kama kweli tuhuma ni ya kweli). Nakuapia kama hawatapata wilaya na mikoa, watarudi Chadema. Usilete shallow analysis, hawa wanahama baada ya Magufuli kusema atahakikisha anaua upinzani. Njia moja wapo ni kuwanunua (madiwani), sasa anaona wenye njaa kama Kafulila, atawapa vyeo.... etc. Petro, akiwapa vyeo utasemaje? Time will tell. Yule binti tayari ni waziri, na akina kafulila and Co. Ltd wanategemea watafanyiwa hivyo.
..kweli cdm walifanya makosa kumfanya Lowassa mgombea wao.
..hoja yangu ni kwamba ndani ya ccm kuna mafisadi kibao. Lakini ccm wana ujasiri wa kuishambulia cdm kwa hoja ya ufisadi.
..katika mazingira hayo, cdm nao hawapaswi kuwa na kigugumizi kuwashambulia ccm kwa ufisadi.
NB.
..ccm hawapingi rushwa hata kidogo. Na ushahidi ni jinsi walivyowahonga madiwani wa cdm Arusha.
CCM ilikuja na sera gani mbadala? Unaangalia weak point ya mpinzani wako unamgonga hapo hapo. matukio ya kuvunja haki za binadamu ni muhimu sana kupata wanachama na kuungwa mkono.......................Mkuu, "with all due respect" upinzani wa Chadema hauna nguvu sana kwa sasa maana yale yote walokuwa wakiyapigania, serikali chini ya CCM ndiyo inayatekeleza.
Chadema waache kutumia matukio kama sera zao na mikakati ya kutaka kugombea kuingia Ikulu.
Waanze upya kwa kuhakikisha wabunge wanaonekana wanafanya kazi waliyochaguliwa kuifanya.
Waje na sera mbadala na zionekane ni sera zipi ambazo zinakuwa ni zaidi ya zile zinazotekelezwa sasa na CCM na serikali yake.
Usitaje sera kama haki ya kufanya mikutano au kubomolewa nyumba zilizo ndani ya hifadhi ya barabara, hizo siyo sera bali ni hoja ambazo kamwe hazitasikilizwa na wananchi ambao huchambua hoja hizo.
Kama mwananchi anaona barabara inapaswa kupanuliwa kupitia ndani ya hifadhi yake na ni kweli amejenga ndani ya hifadhi basi ni lazima nyumba hiyo ivunjwe na apishe bila kutegemea kulipwa fidia yoyote.
Unapotaja sera Chadema ina sera zipi kuhusu Uchumi, viwanda, teknolojia, miundombinu, ajira, elimu, kilimo na kadhalika.
Unakuja na sera mbadala au "alternatives" unaweka wazi wananchi wanapima inagwa hakuna guarantee ya kuzikiubali kama zile zilizopo zinatekelezwa kwa kasi ya ajabu.
Mkishundwa kwenye uchaguzi mnapika sera zingine na zingine na hata baadae mnapata zile sera ambazo zinauzika kwa wapiga kura na huenda mkashinda uchaguzi.
Leo hii karibu nusu ya wabunge wa upinzani hawaenekani majimboni kwao, na hii ni kasoro kubwa sana kimkakati kwa Chadema ambayo ndiyo inawagharimu.
Pili, Dr Slaa ndiye alikuwa katibu mkuu wenu makini sana na hoja yake kwamba hawezi kula matapishi kwa kumkaribisha Edward Lowasa Chadema ni ya kuizingatia sana.
Vinginevyo ntaendelea kuamini kuwa Edward Lowasa, Fredirick Sumaye na mzee Kingunge Ngombale Mwiru wamehamia Chadema kukidhoofisha zaidi kuliko kukiimarisha.
Wakimaliza kazi hiyo basi mwenyekiti Mbowe atakuwa na wakati mgumu sana.
Naamini hayati Mwalimu Nyerere hakutaka kabisa vyama vya siasa lakini kwa kuwa hakuona faida ya kuendelea kuvikatalia akaamua kuvuruhusu mwaka 1992 na wengi hapa akiwemo Pasco tuliona huo ujio wa hivi vyama.
Lakini alifanya hivo kwa malengo kwamba ni lazima vyama hivi huko mbele visiwe na meno makali na hata vikiota meno makali basi wapo mafundi ya kuyapunguza.
Ndiyo maana Chadema inapaswa kuwa makini na utaratibu wake wa kukaribisha wanachama wapya hasa wale wanaohamia kutoka CCM ambao hakuna ushahidi kama wamerusisha kadi za vyama vyao.
Je, tunajua kama profesa Kitila Mkumbo au, bwana Katambi na wenzao kama walirudisha kadi za CCM walizokuwa nazo kabla hawajahamia Chadema kutoka CCM?
Jibu ni hapana.
Kama kweli Chadema ilitaka kuimarika kikwelikweli basi Freeman Mbiwe alipaswa kumpisha Edward Lowasa awe mwenyekiti wa chama ambapo angalau angeweka usawa katika majukwaa kama mtu "mzito" ingawa bado asingeweza kujisafisha na tuhuma za ufisadi.
Nafikiri utanielewa hapo.
Kwa mtazamo wangu naona CHADEMA wajitafakari..warudi kwenye drawing board
Unajua kwenye hizi siasa unahitaji Differentiation
Bila kuwa na tofauti na CCM ...Utashindwa kusema bora mimi CHADEMA kuliko wale CCM
CC
CCM ilikuja na sera gani mbadala? Unaangalia weak point ya mpinzani wako unamgonga hapo hapo. matukio ya kuvunja haki za binadamu ni muhimu sana kupata wanachama na kuungwa mkono.......................
"Off course", sera za CCM ni zilezile lakini zilikuwa hazitekelezwi kwa vitendo na wananchi tukaona na badala yake tunafahamu kilichokuwa kinafanyika.
Sera hizohizo na ilani ya uchaguzi ileile ya mwaka 2015 ndizo zinazofanyiwa kazi kwa sasa na serikali ya awamu ya tanoi chini ya raisi John Magufuli.
Na hilo halina ubishi kwani tunashuhudia utekelezwaji wake.
..kwa hapa naomba msaada.
..najua kuna ilani ya ccm.
..lakini sera za ccm ni zipi ?
..pia sina uhakika kama ccm wana itikadi tena.
..majuzi nilimsikia mbunge wa ccm akilalamika kuwa serekali ya Magufuli inataka kuirudisha nchi kwenye "ujamaa"!!
Cc The Valiant