CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Flyover Dar, Uwanja chato, Mambo yote Dar na Chato, mmmh labda akijenga flyover Tunduru, kondoa au Nanjilinji atawashawishi, Wale wa vijijini waliokuwa wanatumiwa pesa na ndugu mjini sasa huko vijijini hawana kitu hata mbolea watu wa mjini hawatumi pesa, Deal zimekata
unajua watu hawaambiwa mambo mengi mabaya yanayo fanyika, siasa sasa hivi imekua ya upande umoja tu. ukisimama na kuongea kinyume unafungwa. ata hao wanaojiunga ccm, hawana alternative. ni uwoga tu. ila kwa sasa hivi mambo ni mabaya. jiulize kwa nini walitaka kumua Tundu Lisu ? wengi wana kimbilia ccm kwa sababu yakutafuta fursa na kujilinda.
 
Petro E. Mselewa, na mimi nakubaliana na wewe kwamba Team Lowassa ndiyo inayousumbua uongozi wa CHADEMA, na ndio walio wengi hata humu JF. Lugha yao ni moja tu ya kupinga kila kitu kwa kebehi, dharau, lawama, lialia, uzushi, nk kwa kila aina ya lugha chafu.

Viongozi wa CHADEMA Team Lowassa, watambue kuwa Lowassa aliwaandaa angie Ikulu kwa kutumia migongo yao, kupitia tikiti ya CCM, kwa kuwa alikuwa amejekwisha jenga mizizi na mtandao wa ufisadi. CCM ililiona hilo, ikamkata na genge lake.

Viongozi wa CHADEMA Asilia wanalijua hilo ila walimpokea Lowassa kama mtaji wao kisiasa. Na hakika wamevuna siyo tu majimbo zaidi bungeni, pia wanaongoza halmashauri kubwa nchini.

Tofauti ya makundi haya mawili unaonekana sasa kwa jinsi ya utendaji wa Serikali ya CCM inayongozwa na Rais Magufuli, akitambua kuwa nguvu yake ni Watanzania wenyewe. Inapambana na kundi/genge la mafisadi chini ya Lowassa, na wakati ule ule ikiendesha mabadiliko ya kiuchumi, moja ya agenda kuu za CHADEMA asilia.

Team Lowassa, wengi humu, kila lifanyalwo na Magufuli kwao ni mwimba. Wanasahau kuwa matatizo anayopambana nayo Rais Magufuli mengi yamefanyika wakati wa awamu zilizopita, ambazo Sumaye na Lowassa walikuwa Mawaziri Wakuu. Baadhi ya matatizo hayo:
1) Kesi za kimataifa, ambazo leo zinapelekea mali za Taifa kukamatwa.
2) Mikataba mibovu ya usimamizi wa maliasili ya nchi.
3) Ukwepaji kodi na matumizi mabaya na mali ya umma.
4) Urasmu na uzembe Serikalini na Taasisi zake
5) Na mengine mengineyo anayopambana nayo.

Kila lililo na mwanzo lina mwisho. CHADEMA Asilia wakati ndio huu, ngoeni mizizi yote ya Team Lowassa!

nk: Vijana Mnyika, Lissu, na Msigwa unganeni na wazee akina Mwesigwa na Safari kwa kazi hiyo ya kuleta mabadiliko ndani ya CHADEMA au kuiondoa Team Lowassa. Tayari Katambi na Kafulila wameungana na Mkumbo kuonesha mlango, japo walipaswa kufanya mageuzi ndani. Tatizo alikimbiwi ila hukabiliwa. Tatizo lichukuliwe kama changamoto, mwishowe ni fursa ya mabadiliko.

umepotosha sana.
hasa hilo la mikataba. mkataba unaosunbua huko ulaya kwasaaa ni makosa ya magufuli personaly.
na hii bomoa bomoa ya leo na zile kuuza nyumba za serekali siku yaja watalipa tu.
 
umepotosha sana.
hasa hilo la mikataba. mkataba unaosunbua huko ulaya kwasaaa ni makosa ya magufuli personaly.
na hii bomoa bomoa ya leo na zile kuuza nyumba za serekali siku yaja watalipa tu.
Amepotosha sana tena, Kimsingi jamaa anafanya utumbo mwingi tu. na kwa kua ame silence upinzani, hakuna mtu anayejua. wengi tu wamepotezwa. ata hao wanao hamia ni uwoga wa kupotezwa na kufuatiliwa. Kumbuka ata Mugabe alishangiliwa but one day waliomshangilia ndo waliomuondoa madarakani
 
unajua watu hawaambiwa mambo mengi mabaya yanayo fanyika, siasa sasa hivi imekua ya upande umoja tu. ukisimama na kuongea kinyume unafungwa. ata hao wanaojiunga ccm, hawana alternative. ni uwoga tu. ila kwa sasa hivi mambo ni mabaya. jiulize kwa nini walitaka kumua Tundu Lisu ? wengi wana kimbilia ccm kwa sababu yakutafuta fursa na kujilinda.

Kwanini unasema walitaka kumuua Tundu Lissu?

Kwani hakuna mhuni au mtu yoyote yule ambae hakupendezwa na tabia ya Tundu Lissu (ya kumdhihaki raisi wa nchi mbele ya umma) na ambae anaweza kutaka kumuua Tundu Lissu?

Kama ni kuuwawa tu, Tundu Lissu asingekuwa hai leo angelengwa kichwani tu na akafa palepale.

Nadhani wale "assailants" walikuwa na lengo la kumpa onyo.

Kwanini mnapenda kujenga nadharia zisizo na ushahidi?

Una uhakika gani kama walotaka kumuua Tundu Lissu ni CCM?
 
Ahsante kwa hoja chokonozi. nianzie na hilo la ukomo wa uongozi. sidhani kwamba linaweza kutusaidia sana kwa hivi sasa. chama imara ni sharti kiwe na misingi imara, kiwe na "constituency", kuwe na watu hasa waliokereketwa na waliokula yamini kukilinda. hawa ndio wapate wafuasi. ni baada ya chama kujijenga sana kwa muda mrefu, ndio unaweza kuleta hizo taratibu za kutegemea demokrasia. lakini hata hivyo ni lazima kuwe na utaratibu tofauti wa kusimamia wale wanaoingia katika chekeche. katika mazingira ya sasa, ambapo CCM chama dola kinatumia kila mbinu, huwezi kusema tu eti tutegemee demokrasia
God bless you for your good writing and short analysis
 
Mkuu Pascal Mayalla mara nyingi huwa unatoa fact, ila leo umesema kweli tupu no.4, 6 na 14. Ujio wa Lowasa ndani ya CDM ni kuzima uzalendo na kukaribisha ukurasa mpya wa kuwatetea mafisadi....

* Kama list of shame iliyowekwa hadharani na CDM ni kweli iliwezekanaje Lowasa kuwa mgombea wetu....
*Nilizungusha sana mikono ila kama ndiye mgombea wetu tena..nitatafakari wa kumpa kura yangu...sintaenda CCM maana sintaweza kushindana na dhamira yangu...

**Wazalendo wa CDM watakuwa wanajitafakari tulipojikwaa ili tusije anguka**
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, hivyo ni kawaida, ukifanya ukosoaji wowote kuihusu Chadema humu jf, utanyooshewa vidole kuwa wewe ni CCM. Nafanya ukosoaji wangu constructively, truthfully with objectivity, impartiality and balancing, hivyo nawashauri Chadema, wawe tayari kupokea na kuuzingatia ushauri wowote, hata kama ushauri huo unatoka kwa kichaa au kwa shetani, ili kujitafakari na kujitathinini, kama inajidhania imesimama, na uiangalie isianguke. CHADEMA msipuuzie ushauri hata kama ni kutoka kwa shetani!, S ...

Utangulizi
Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa Chadema, na unatolewa na mtazamaji wa muda mrefu wa mchezo wa siasa nchini Tanzania, ambaye ameangalia tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Tanzania, uchaguzi wa jimbo la Kwahani, 1994, uchaguzi mkuu wa 1995, 2000, 2005, 2010, na 2015. Ushauri wenyewe ni kuhusu hii hama hama ya wanachama na viongozi wa Chadema kuhamia CCM. Naishauri Chadema Wajitafakari!, Wasiwabeze Wanaohama Kama Wafanyavyo CCM, Wanaohama Chadema, Wana Hoja za Msingi, Chadema Wanadhani Adui Yao Mkuu Anaowanya Kushindwa Kwenda Ikulu ni CCM, Kiukweli Adui Mkuu wa Chadema Sio CCM, Nitawatajia Adui Mkuu wa Chadema, na Mwisho Nitawapa Ushauri Chadema Wafanye Nini, Waweze Kuingia Ikulu 2025 Magufuli atakapomaliza and only if Magufuli atamaliza 2025!, kwa sababu haya ninayoshauri, kwa uchaguzi wa 2020, saa hizi tayari ni too little too late, na Magufuli ni just too powerful kiasi kwanza hakutakuwa na uchaguzi wa rais 2020, uchaguzi wa rais wa 2020 utakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, lakini mshindi tayari ni Magufuli, hivyo wote watakaompinga Magufuli 2020, itakuwa ni kujifurahisha tuu, hivyo Chadema Watake Wasitake, Lazima Wabadilike, Vinginevyo...its the end of the road kwa Chadema, tunarudi kwenye nchi ya Chama Kimoja.

Why Chadema?
Tanzania japo tuna vyama vya siasa zaidi ya 22, lakini vyama vikubwa ni CCM, Chadema na CUF, by now CUF is already a gone case, hivyo tunapozungumzia upinzani Tanzania, tunazungumzia Chadema. Kifo cha CUF hichoo... chaja! Upinzani kubaki CHADEMA pekee ...

Justification ya Kuikosoa Chadema kwa Mtu Ambaye Sii Mwanachama.
Mashabiki na manazi wa Chadema humu jukwaani, ukifanya ukosoaji wa Chadema, au kutoa ushauri wowote kuhusu Chadema, watakubeza unashauri kama nani?. Kwa sababu Chadema ni public party paid by taxpayers money, then the taxpayers have the right to know the conduct of their tax, hivyo Watanzania wote wana right kujua mambo yote ya Chadema, public na private, ni haki yao kwa sababu kinaendeshwa kwa kodi zao!.

Kwanini Uishauri Chadema, Kwa Wao Wenyewe Hawajioni na Kujishauri?.
Ushauri huu nautoa kwa dhana kuwa Viongozi wa Chadema, wanachama wao, wafuasi wao, washabiki wao na manazi wa Chadema humu jf, wote ni pro Chadema, wako ndani ya box la Chadema, hivyo wanaweza wasiwe na uwezo wa kuona nje ya box, soso tulioko nje ya box ambao ni watazamaji, tunaweza kuwa tunaiona Chadema vizuri Zaidi kwa nje, kuliko waliomo ndani ya chama, lakini pia kuna walioko ndani, wanayaona madhaifu na mapungufu ya Chadema from within, lakini kwa vile wamo, wanakosa objectivity ya kujiambia, kujitathinini na kujikosoa, hata hivyo tathmini ya kweli, inapaswa ifanywe na watu wa nje na sio kujitathmini yenyewe.

Chadema Isiwabeze Wanaohama, Ni Haki Yao, Ila Pia Izingatie Hoja Zao, Wana Hoja za Msingi
Kati ya wanachama na viongozi wa Chadema wanaohamia CCM, kuna wengine wanahama kimya kimya bila kusema sababu, kuna wengine wananunuliwa, na kuna wengine na haswa baadhi ya viongozi, wanapohama, wanaandika barua Chadema na kuaga kwa kutoa sababu, ziwe ni sababu za kweli au ni visingizio tuu, lakini kuna kitu wanasema, na wengine hawasemi chochote kuhusu Chadema lakini siku wanapokelewa CCM, Chadema, japo ni kweli wengi kinachowahamisha Chadema ni njaa zao tuu, na wanakwenda CCM kufukuzia fursa, lakini kuna baadhi, wana hoja za msingi sana, hivyo Chadema inatakiwa kutozipuuza hoja zao, isisikilize na kujitathmini kuhusu ukweli wa hoja hizo.

A Way Forward, Chadema Ifanye Nini.
  1. Kwanza Chadema ijitathmini, is it on the right track?, itambue makosa yake, ikubali makosa, ijirekebishe, isonge mbele. CHADEMA ni sikio la kufa? Iambiwe vipi ili isikie? Masha ana hoja za msingi, zisikilizwe, zizingatiwe, zisipuuzwe!
  2. Ianzishe grassroots recruitment ya wanachama wake waaminifu, isije kujikuta imewakumbatia CCM ndani, Chadema nje hadi ndani ya CC yake, kama ilivyotokea kwa Mwenyekiti wa Bavicha.
  3. Ianzishe headhunting na spotting leadership talents na able people toka kwenye jamii kujiunga Chadema na kujenga kada ya viongozi wake wa kesho, born and breed in Chadema, kwa kuwafanyia grooming, ili kupata wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi.
  4. Ipunguze kushobokea makapi kutoka CCM, wana CCM wanaojitoa CCM na kujinga Chadema, wawe wanachama wa kawaida tuu kama wanachadema wengine na sio kupapatikiwa na kupewa uongozi moja kwa moja.
  5. Chadema I invest on people na mass mobilization, na sio ku invest on vitu na mikutano tuu ya hadhara, kupitia social media na kumiliki media yake yenyewe, kutawafikia watu wengi Zaidi kuliko kutegemea mikutano na maandamano pekee.
  6. Chadema irudishe ukomo wa uongozi, hata kiongozi awe mzuri vipi, anafikia kiwango cha ukomo wake na kuwa kama saturated solution, he can do no more than what he can!, anakuwa hana jipya!, pia Chadema waandae succession plan, by now, wawe na a pool of able people from within kushika nafasi zote za uongozi, na kuendesha serikali, kungekuwa na ukomo, by now watu wangejua Mbowe amefikia ukomo wa uwezo wake, hivyo nani watampokea.
  7. CCM ni chama dola, hivyo Chadema isitumie model ya CCM kuitafuta ikulu, iandae model yake yenyewe ya kupata viongozi wake na wagombea wake, mtindo wa the democrats ya US ni mzuri kuanzia kwenye primaries.
  8. Kuondokana na viongozi ving'ang'anizi na miungu watu, maadamtarget ni kuingia ikulu, umeshindwa kuuingiza Chadema ikulu, unapisha wengine wanaendeleza, sio umeshindwa hala unang'ang'ania!.
  9. Kuwafanyia tathmini wabunge wake na kukubalika kwao, na kuwe hakuna haki miliki ya majimbo, mfano 2020, Mdee anatathminiwa amefanya nini Kawe for 10 years, na jee bado anakubalika?, Wanachadema wote wenye uwezo, wawe huru kumchallenge Mdee, akitokea mwanachama mwingine mwenye sifa Zaidi, uwezo Zaidi na kukubalika Zaidi, Mdee anawekwa pembeni, vinginevyo 2020, kuna majimbo kibao Chadema mtayarudisha CCM!.
  10. Chadema kionyeshe ukomavu na kuwa ni chama mbadala kwa kuachana na cheap politics ya siasa za matukio, na kujikita kwenye real politics ya kushindanisha sera, sio kwa kupinga kila kitu, CCM ikifanya mazuri, mfano elimu bure, Chadema ikubali hili ni zuri, lakini ionyeshe ingekuwa Chadema ingefanya bora zaidi kwa elimu bure hadi chuo kikuu, kwa kuonyesha how CCM inatapanya fedha kwa mambo yasiyo na maana, halafu inanyanyasa Watanzania masikini kwa kuwanyima mikopo. Chadema wajifunze kuibomoa CCM kwa hoja na sio siasa za matukio, mfano mwaka 2020, Magufuli anaingia ulingoni akiwa na elimu bure, ndege za ATCL zinapaa dunia nzima, flyovers, reli ya SGR, na Tanzania ya viwanda. Chadema lazima waje na sera mbadala kuonyesha jinsi ATCL, flyovers na SGR zilivyowatia umasikini Tanzania, kama fedha hizo zingewekezwa kwenye sekta ya kilimo nini kingepatikana, bila kuinua sekta ya kilimo, hiyo Tanzania ni Tanzania ya viwanda gani vinavyotumia malighafi gani?. Ijikite kwenye hoja kama hizi Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...
  11. Chadema ipiganie a level playing field kwenye the political ground, kupitia tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, haiwezekani watu wawili wanagombea urais, mgombea mmoja anakuja na vingora, na full government media team, paid by public money for the advantage ya CCM, halafu, mwingine with nothing, halafu utegemee kushinda!.
  12. Chadema ipiganie true free and fair elections with maximum transparency, kama hakuna manouvers zozote zinazofanywa na Tume ya Uchaguzi, kwa nini wazueie party tallying?, wanaogopa nini, kama matokeo yote hadi ya urais yanabandikwa vituoni mbele ya mawakala wa vyama, kuna kosa gabi kama mawakala wote watakuwa na smart phones, ku scan matokeo na kutuma makao makuu kwenye tallycenters za vyama, kama haki itatendeka, then tallying za vyama zitafana na tallying ya NEC, what is it there to hide kuzuia tallying?.
  13. Chadema kutimiza majukumu yake kikamilifu kama Chama cha upinzani kazi yake sio tuu kuikosoa serikali, bali ku I check serikali kuhakikisha inafuata katiba na kutekeleza sharia, taratibu na kanuni, mfano, katika kuzuia mikutano ya kisiasa, rais Magufuli amevunja katiba wazi wazi kabisa mchana kweupe!, chama chochote makini, by now, kingeifungua shauri mahakamani, ili mahakama itoe tafsiri rasmi, kama itathibitisha rais amevunja katiba, anashitakiwa na bunge, na kuondolewa madarakani!. Mfano hata suala dogo tuu kama Daudi Bashite, nilishauri Je, wajua suala vyeti vya Bashite, linaweza kabisa kumng'oa Rais ...
  14. Chadema waipinge CCM kwa kujikita kwenye hoja zenye maslahi kwa taifa, ujinga, umasikini, maradhi, rushwa na ufisadi, kwa kuonyeshea CCM katika kipindi chote cha miaka 50, CCM imeshindwa, na katika rushwa na ufisadi, Chadema iwaeleze wananchi, CCM ndio shina na mlezi wa rushwa zote na mafisadi karibu wote ni CCM!, ili wananchi waelewe kuwa CCM inapigana vita ilivyovilea na kuvijenga.
Ni hayo kwa uchache, nikikumbuka mengine nitayaongeza.

Paskali
mkuu nyuzi zako ni tamu kuzisoma na ni vikirishi saana hata kama ni ndefu kiasi gani huchoki kusoma.

i declare wewe ni mtu nnayekutamani saana kwanna unavyofanya uandishi wako na maudhui yake.

kwa jinsi nnavyokuona ni kama chadema ingekutumia kama mshauri wao tuu wakakuelewa basi wangefanikiwa saana na iwapo hata Serikali wangekuweka katika kundi la washauri wake nadhani tanzania tungefika mbali.

nnaimani hutokufa moyo kuwashauri viongozi wetu wa vyama na serikali ipo siku haya unayoyashauri wasipo yakubali wao basi kizazi kijacho kitaona dhamani yake yatawasaidia
 
Kaka Pascal Mayalla, nakubaliana na hoja yako. Lakini, ugonjwa mkubwa uliobaki na kuwasumbua CHADEMA ni kuwepo kwa Lowassa na kundi lake. Kundi la Lowassa likiondoka kwa kuhamia chama kingine au kuanzisha chama chao, CHADEMA itarejea kwenye njia yake. Hakika, uwepo wa Lowassa na kundi lake ni jambo gumu sana kwa CHADEMA kwakuwa inakuwa na muda mwingi wa kujibu tuhuma kuliko kujijenga.
Kwa hili tupo pamoja!
Chadema inakosa kujua tatizo liko wapi!
Wanaohamahama huku kule wapo kimaslahi zaidi.
Chadema wasiwababaikie saaaana na watu wanaohama toka ccm.
Hili zoezi la kuhama vyama naona lipo Tz tuu shida ni nini?
Chadema fanyeni mikutano ya kichama kuchanganua mambo sio kauliiiiii tuuuu kila siku!
 
Mkuu pasco.
Kama ni kushindana kwa hoja, hii unaweza kushindana na atakayekua radhi ushindane naye.

Hatahivyo Mpaka sasa naona CCM haiko tayari kushindana kwa hoja na xhama chochote ikiwemo CDM.

Mfano. Tundu lisu alishindana kwa kujenga hoja makini za kusaidia jamii, matokeo yake sisi tu mashahidi kwa jinsi alivyo nusurika Umauti. Tukashindwa hata kumfanyia maombi ya kitaifa.
Huku wapo wanao hoji uzalendo wa Tundu Lisu kwa Taifa.

So mi nachoona ukiongozwa na dikteta. Kuna kua hakuna the way foward.

Wako wasanii kama akina Roma Mkatoliki.

Mwisho nakubaliana na wewe kua adui wa CDM sio CCM. Kwasababu moja kubwa. Naiona CCM yenyewe ikiwa imeshikwa. CCM imefungiwa minyororo haiwezi kufurukuta. This is one man show.Not a party show.

Sote tulishuhudia swala la kuvamiwa kituo cha Clouds FM lilivyotumika kumng'oa uwaziri Nape.


Mwisho napenda ufahamu kua:-
ushauri wako unaweza kua sehemu ya trial amd era kwa manufaa mapana ya CDM lakini sio suluhisho per Se.
Its a one man Army fight and he won't prosper. Ukitizama kwa umakini mkubwa pia utagundua kuwa wale wapiganaji ni kama wamesusia na kukaa kando.

Ccm ya sasa hawawezi kushindana kwa hoja. Na hao waliowapokea juzi hawana uwezo tena kuwashawishi wananchi ni bora cdM nyarandu anaeleweka kwa wananchi
 
Mkuu Paschal,

Aliekuwa ameiimarisha Chadema na kuipa nguvu kubwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 alikuwa ni Dr Slaa.

Tunafahamu ni kwanini Dr Slaa aliondoka Chadema na sasa anapumzika kabla ya kurejea CCM (tetesi).

Chadema haina nguvu sana na inachofanya chama hicho kisimame vizuri bungeni ni kujitutumua kwa mwenyekiti wake Freeman Mbowe kwa hoja za matukio badala ya sera.

Kama wote humu tumewasikiliza kwa makini Profesa Kitila Mkumbo na Patrobas Katambi ambao kwa hakika wametoa mwelekeo wa uwezo wa kufikiri wa wapinzani wa Tanzania ambao bado ni mdogo sana.

Simaanishi hawa wawili na wengine wanaohamia CCM kutoka Chadema, au ACT au CUF kwamba wao wana akili sana, la hasha bali wana wezo wa kutathmini yale walokuwa wanayaamini kama kweli ni sera za vyama vyao.

Kama una mwenyekiti wa baraza la vijana katika chama chako na mwenyekiti huyo anaondoka, hilo ni pigo kwa chama kwasababu baraza la vijana ndilo msingi wa ukuaji wa chama chochote kile.

Kama tunakumbuka mwaka 2014 BAVICHA walifanya uchaguzi ambapo Katambi alipambana na vijana wenzie Daniel Naftari na Upendo Peneza ambao wapo Chadema Bavivha kabla ya Katambi.

Sababu za Katambi kushinda uchaguzi ule ilhali alikuwa ni mtu wa nje yaani outsider, kilionyesha uwezo wake wa kujenga hoja na kuzungumza kwa ufasaha anapokuwa jukwaani.

Hivyo ni kweli Chadema inahitaji kujitafakari sana katika uwezo wake wa kupata wanachama wapya na hasa vijana ambao ndiyo msingi wa chama.
Katambi huyo tangu ashinde BAVICHA umemsikia kafanya lolote? Sisi vijana hatujamuona hata katika ziara akipitia mikoa yote wenzake kina Heche walipita. Kama unamuona Katambi ameua chama lets wait and see mwisho wake. Wengi walihama CHADEMA awaone walivyoshuka kisiasa. Base on facts not non-sense
 
Kaka Pascal Mayalla, nakubaliana na hoja yako. Lakini, ugonjwa mkubwa uliobaki na kuwasumbua CHADEMA ni kuwepo kwa Lowassa na kundi lake. Kundi la Lowassa likiondoka kwa kuhamia chama kingine au kuanzisha chama chao, CHADEMA itarejea kwenye njia yake. Hakika, uwepo wa Lowassa na kundi lake ni jambo gumu sana kwa CHADEMA kwakuwa inakuwa na muda mwingi wa kujibu tuhuma kuliko kujijenga.


Mkuu ungekuwa karibu amini nakuambia ningekuagizia kinywaji chochote upendacho.


Asante kwa kunisemea pia.


Nimemkumbuka mh.Mnyika daaaaah.
 
Back
Top Bottom