CHADEMA mikutano ya hadhara kila siku inakera

CHADEMA mikutano ya hadhara kila siku inakera

Mikutano yenyewe haina jipya kila siku wanazungumza yaleyale ufisadi ufisadi ufisadi mpaka watu wamewachoka...hawana sera nyingine,hawasemi tukiwapa nchi watatusaidia vipi 2pate maendeleo...
Ndio maana mikutano yao inajaa Arusha na Moshi pekee,kwingine huwa wanakosa watu kabisa.
 
Hata Shetani anaposikia jina la MUNGU linahubiriwa kila siku anakereka sana. ni sawa endeleeni kukereka
 
Siku za hivi karibuni kumejitokeza wimbi la wabunge wa cdm kufanya mikutano ya hadhara sehemu nyingi za nchi, nakubaliana na ukweli ya kwamba cdm imepata umaarufa hasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.Ninachoaasi viongozi cdm na wafuasi wao ni kwamba binadamu yoyote ana hulka ya kukosa hamasa na kitu chochote hasa baada ya kuwa na mazoe na kitu husika, rai yangu ni kwamba hii mikutano ya hadhara mnayofanya imeanza kuwachosha wananchi na sitashangazwa na cdm kukosa kabisa wasikilizaji ama wahudhuriaji wa mikutano yao 2015.

Mtakoooma! Na bado. Kila idara tangu Bunge, Mhakama, Pesa(za kifisadi), na Utawala wameshika. Sie wetu ni WENYE NCHI. Magamba GOODBYE! 2015 utatujua. Unakumbuka Operesheni SANGARA ilifanyika lini?

Shutup!

M4C.

CHADEMA Nguvu ya Umma.

Viva Chadema.
 
Unataka wakae ofisini ili ikifika 2015 mseme CDM ni chama cha msimu?? IMEKULA KWENU
 
Wanachofanya ni kufikisha elimu ya uraia kule ilipokosekana pamoja na kutangaza sera zao ili itakapofika wakati wa wananchi kutoa ridhaa zao kwa kupiga kura waweze kuelewa haki zao na kulinganisha sera. Hata hivyo unaweza kupima matokeo ya mikutano yao kwa wanachama wengi kujiunga na chama chao, pia hata wanachama na viongozi wa vyama vingine vya siasa wanajiunga na chama hichi kwa wingi. Hii ni moja ya mafanikio yao machache katika hatua za kukamata dola na kuliongoza Taifa. Kama wanafanya hiyo mikutano yao pasipo kuvunja sheria, hiyo ndiyo demokrasia huru.
 
Halafu mods kwanini msiweke charges ktk kuanzisha uzi?? Yaani mtu akitaka kuweka uzi wake lazima alipie kidogo pesa ya uchakavu! Nadhani hii itapunguza nyuzi za kijinga jamvini..(mtazamo wangu mimi binafsi)
 
Kama wewe ni msafi na unamvuto kamwe huwezi kujificha ndani, ni haki CHADEMA kufanya mikutano kila siku kwani kwa kufanya hivyo wanaua ndege wawili kwa jiwe moja!, wanatoa elimu ya uraia, na utambuzi wa haki za raia, pili wana imarisha chama kwa kupata wanachama wapya. Kama unasema mikuta inachosha, Mbona CCM ambao hawafanyi mikutano kila siku wakifanya mikutano hawapati wasikilizaji? Mwendo mdundo CHADEMA mpaka 2015 asiyetaka shauri yake!
 
Hoja yako ni dhaifu. Siasa mtaji wake ni watu. Usipowafikia unatarajia nani afanye kazi hiyo kwa niaba yako? 2015 muda wa kampeni hautoshi kufika kila mahali na kuongea kila jmabo, ukumbuke licha ya kufanya mikutano pia bado inadhibitiwa. Jipange upya!!!
 
word..kila siku mnakalia politics tu kuwalemaza watu badala ya kuwahamasisha kufanya kazi..nchi haijengwi kwa satilili hii ya mikutano kila siku...hili swala lilikuwa linaniumiza kichwa sana..nashagazwa na utaratibu wa msajili wa vyama pamoja na sheria inayosimamia mambo ya vyama vya siasa kuwa weak kiasi kwamba inaipa vyama loop hole ya matumizi mabaya ya uhuru wa vyama kufanya kazi za kisiasa..mbona uchaguzi ulishakwisha kitambo ndugu zanguni?? let us be realistic..lini tutafocus kujenga taifa letu..ghafla tu..zimeashaanza vugu vugu za uchaguzi wa 2015 wakati bado miaka mitatu kufikia huko.. kwahiyo mnataka kuniambia tutaendelea na porojo hizi kwa miaka mingine mitatu mfululizo?? tuache ujinga na tufanye kazi period!!! anaenuna na anune..na ataenuna ni mmoja wapo wa wavivu wanaotuletea umaskini..
 
Siku za hivi karibuni kumejitokeza wimbi la wabunge wa cdm kufanya mikutano ya hadhara sehemu nyingi za nchi, nakubaliana na ukweli ya kwamba cdm imepata umaarufa hasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.Ninachoaasi viongozi cdm na wafuasi wao ni kwamba binadamu yoyote ana hulka ya kukosa hamasa na kitu chochote hasa baada ya kuwa na mazoe na kitu husika, rai yangu ni kwamba hii mikutano ya hadhara mnayofanya imeanza kuwachosha wananchi na sitashangazwa na cdm kukosa kabisa wasikilizaji ama wahudhuriaji wa mikutano yao 2015.

Kwa hiyo unamaanisha mtoto huwa anamkibai baba kwa sababu huwa anaishi nae kila siku?Fikra zako mgando peleka kwa magamba wenzio sababu kwa mitizamo na akili zenu huwa mnafanana sana kama mazambarau.
 
CDM wanafanya kazi yao ya kisiasa(wanatimiza wajibu wao wa kisheria na kiuongozi), lazima waingie kwenye field na hii wanatimiza yafuatayo:
1. kutoa somo la uraia (very important), ccm haitaki hilo kwani wanajua fika waTz wakierefuka wataondolewa madarakani kwani wamekuwa manyang'anyi kwa miaka mingi
2. kuwaeleza wananchi kinachoendelea kwenye nchi yao
3. kuhamasisha kujiletea maendeleo wao wenyewe make ccm wanajiletea utajiri wenyewe, na hawana lengo na maisha bora kwa kila mTz.
4. kuwaelimisha juu ya haki/wajibu wao na haki/wajibu wa serikali
5. Kujiimarisha kisiasa kama chama cha SIASA ambacho kiko tayari kuchukua dola.
6. kufahamu matatizo ya wananchi na kuwasaidia pale panapowezekana na yale wasioweza kwa sasa wafanye baada ya 2015
7. kuwahamasisha wajitokeze kutoa maoni juu ya uundwaji wa katiba mpya.
8. na maswala mengine lukuki

ccm wanatawala CDM wanaongoza, ccm hawawezi kufika kwa wanachi kuwaambia chochote(mwezi akishafahamika atadhubutu kusimama mbele ya watu?). CDM wasipofanya haya waTz watawahukumu make ahkuna mwingine wa kufanya.

Kwa hiyo ndugu yangu Makupa na wengine mlioko nyuma yake, mkubali ukweli. ukitaka kupona sharti "unywe dawa japo ni chungu"
 
Siku za hivi karibuni kumejitokeza wimbi la wabunge wa cdm kufanya mikutano ya hadhara sehemu nyingi za nchi, nakubaliana na ukweli ya kwamba cdm imepata umaarufa hasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.Ninachoaasi viongozi cdm na wafuasi wao ni kwamba binadamu yoyote ana hulka ya kukosa hamasa na kitu chochote hasa baada ya kuwa na mazoe na kitu husika, rai yangu ni kwamba hii mikutano ya hadhara mnayofanya imeanza kuwachosha wananchi na sitashangazwa na cdm kukosa kabisa wasikilizaji ama wahudhuriaji wa mikutano yao 2015.

Makupa wa Old Moshi bana! Vipi umeshawasiliana na mama Recho hajambo?
 
Mikutano yenyewe haina jipya kila siku wanazungumza yaleyale ufisadi ufisadi ufisadi mpaka watu wamewachoka...hawana sera nyingine,hawasemi tukiwapa nchi watatusaidia vipi 2pate maendeleo... Ndio maana mikutano yao inajaa Arusha na Moshi pekee,kwingine huwa wanakosa watu kabisa.
chanzo cha umasikini ni ufisadi wa ccm na ni lazima kila Mtanzania aelezwe ili aikatae ccm
 
Siku za hivi karibuni kumejitokeza wimbi la wabunge wa cdm kufanya mikutano ya hadhara sehemu nyingi za nchi, nakubaliana na ukweli ya kwamba cdm imepata umaarufa hasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.Ninachoaasi viongozi cdm na wafuasi wao ni kwamba binadamu yoyote ana hulka ya kukosa hamasa na kitu chochote hasa baada ya kuwa na mazoe na kitu husika, rai yangu ni kwamba hii mikutano ya hadhara mnayofanya imeanza kuwachosha wananchi na sitashangazwa na cdm kukosa kabisa wasikilizaji ama wahudhuriaji wa mikutano yao 2015.

Magamba naweweseka sana veve!!tuna mpango kufanya kila baada ya masaa sio kila baada ya siku,kama mnajisikia kupoteza na nyie mwaweza kufanya japo kila mwezi ila angalieni meno yenu ya sebuleni,maana hata wananchi wachache wataokuja,watakuja kuwachapa mawe tu!
 
kama cameron vile! sasa nyie si mnasema wapinzani ni vyama vya msimu? wanawanakuja full tuone kanma ni chama cha msimu
 
Back
Top Bottom