zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 22,920
- 36,869
Benson benson brother nakuone huruma unavyopotosha na hapa ndipo napomuheshim dr slaa yaani pamoja na kwamba alionekana amekisaliti chama ila alipoondoka alikaa kimya mpaka leo ila wwe toka ujiuzulu kila cku mitandaoni kuishtaki chadema hivi kwani lazima uwe chadema?? si uhamie ccm au usubiri uchaguz wa ndani ugombee uenyekiti untoe mbowe kipi kigumu??? anyway hoja zako nyingi hapo ni hearsay huna ushahidi kabisaWahenga walisema “Mtu Mzima akilia ujue kuna Jambo”
Katika siku za hivi karibuni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA akiwa jimboni kwake Hai amesikika akilalama au kujinasibu kuwa asingekuwa na roho ngumu angekuwa ameshaachana na upinzani. Nukuu iliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii hususani kanda ya Kaskazini ilisomeka ifuatavyo “ Upinzani ni wito, wenye roho nyepesi hawawezi, kama ningekuwa napenda Fedha, nina roho nyepesi, ningeshachukua hizo pesa na ningeshakimbia kabisa upinzani” Habari hii pia iliandikwa kwenye gazeti la Mwananchi.
Habari hii haikuwa mpya kwangu kwani inaonekana Mh Mbowe amekuwa akiirudia sehemu mbalimbali anapokutana na viongozi wa Chama kwa malengo ya kuwajengea imani juu yake hususan kwenye swala zima la tamaa ya fedha. Maslani akiwa mkoani Tanga wakati wa Uchaguzi aliouvunja kwasababu zake binafsi wa Kanda ya Kaskazini Mh Mbowe inasemekana aliwaambia baadhi ya viongozi kuwa ameshawishiwa apewe Bilioni 70 ili aivuruge CHADEMA (Niliambiwa na kiongozi mmoja ambaye ni rafiki yangu mimi ninayemuamini) Baada ya kusikia habari hii ilinishtua sana na kuogopa kuwa huenda Fisi anajaribiwa kwa Mfupa.
Aidha Dr Mashinji Katibu Mkuu wa CHADEMA alitoa taarifa kwa Umma siku za karibuni pia kuwa kuna Wabunge wa CHADEMA wanataka kuhongwa ili wajiuzulu ubunge. Hakutuambia kama Mwenyekiti wake nae ni miongoni mwao au la.
Maoni yangu kwa mfululilizo huu ni kuwa Wanachama na viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuwa macho sana na Mwenyekiti wao katika wakati huu kuliko wakati mwingine wowote kwasababu zifuatazo:-
1. Mbowe ametikiswa au kutikisika kiuchumi katika awamu hii kuliko ambavyo imewahi kumtokea wakati mwingine wowote. Billcanas imefungwa, gazeti halifanyi vizuri sana, Madeni ya malimbikizo ya kodi na shamba la mboga nalo limeharibiwa.
2. Awamu ya nne siasa ilikuwa ni mradi na fursa kwa viongozi wengi na makada wa vyama hususan vya upinzani. Lipo andiko la Mh Zito liliwahi kuonekana mtandaoni kuonyesha kuwa kuna wana CCM wa wakati huo waliokuwa wakiwapa fedha viongozi wakuu wa upinzani kwa maslahi yao. Mbowe amekuwa Mbunge katika awamu yote ya nne na biashara zake zikiendelea vizuri pia taasis kama TAKUKURU na TRA hazikuwa moto kama wakati huu. Ukaguzi kwenye vyama nao ulikuwa mdogo tofauti na ninavyotarajia kwa wakati huu.
3. Mbowe hajawahi kupata shida akiwa yoyote ya kiuchumi au msukosuko wa jela au mahabusu akiwa CHADEMA. Kuna wahenga wa Chama waliniambia miaka ya 2004 Mbowe alipata mtikisiko wa ndani ya Chama wakati huo akiwa amepoteza Ubunge wake huko Hai kwa hasira akatishia kuhamia CCM miaka hiyo. (Maneno ya Wahenga hayo sio yangu) Hii inamaanisha kuwa maslahi yake ndani ya upinzani yakidhibitiwa basi anaweza kufanya lolote kuyanusuru.
4. Ujio wa Mawaziri Wakuu wawili wastaafu nao ni Changamoto kwa Chama. Mawaziri hawa wanahesabika kama wasaliti ndani ya CCM na dola pia. Nakumbuka nguvu kubwa iliyotumiwa na CHADEMA kupambana na Zitto Kabwe kwa hoja au dhana kuwa Zitto ni Msaliti. Naamini kanuni ni hiyo hiyo hata CCM pia. So by Compromising or by Force Mbowe lazima atikiswe.
5. Dr Slaa wakati akijitoa kwenye Ukatibu Mkuu alidai kuwa alitaka kuhongwa Bilioni 5 ili ampokee Lowassa akakataa. Dr Slaa akadai anashangaa Mwenyekiti wake alivyokubali kumpokea Lowassa wakati alimjulisha juu ya swala la yeye kutaka kupewa fedha.
6. Dili ya Bilioni saba (7) ndani ya Chama nayo nimeitia mchanga naamini TAKUKURU watakuwa wanaifuatilia kwa karibu.
Kwa hoja hizo mimi binafsi simuamini Mbowe kabisa linapokuja swala la fedha. Na kwa yowe hili analolipiga sasa inaonyesha kabanwa mahali. Wito wangu wanachama na viongozi mchungeni Mwenyekiti wenu asije kutusaliti tena watanzania. Ukiona mtu mzima Analia ujue kuna jambo
.
1 Ndio katikiswa kiuchumi sababu ni mpinzani wa serikali na ili kuona anaonewa mbona shauri lake la kuhusu kuvamiwa shamba ameshinda?? kma ni haki si angeangushwa !!! je kwakuwa katikiswa kiuchumi wwe unaamini hafai kuwa mwenyekiti tena ama? kwani uongozi ni pesa ama utendaji???
2. HEARSAY eti lipo andiko?? andiko la zitto likwapi?? unasema alidai viongozi wa upinzani je huyo kiongozi upinzani alimaansha nu mbowe??? hivi unapotosha ili iweje???
3.HEARSAY tena eti kuna wahenga waliniambia??? hivi hearsay inaweza tumika kujengea hoja? unaweza kuwataja hao wahenga?? na ulitihibitisha au maneno yao ulichukua kma yalivyo???
4. changamoto gani?? itaje??? na maamuzi ya kumleta lowasa wapi yalikuwa personal ya mbowe mbona mshenga slaa alikiri iliwahusisha gwajima mbowe lisu na slaa??? unapotosha kwa faida ya nani???
5. HEARSAY tena eti Dr slaa alidai?? dr slaa alithibitisha?? alienda TAKUKURU??? alichosema dr slaa ni kwamba wakati wa sakata la richmond alifuatwa kuhongwa milion 500 ili ajenge hoja na ushawishi ripoti isisomwe bungeni hayo madai ya bilion 5 aliyatoa wapi na lini??? we kila kitu ni cha kuambiwa hata utafiti hufanyi no wonder mkoa zima hatuna mbunge wa chadema kumbe all ths tym tumeweka vilaza kma wwe
6 Dili gani ya bilion 7??? HEARSAY tena huku ushahidi hamuweki kipi kigumu kuwka hapa credible source ya taarifa zako hta za kiutafiti kuliko maneno tu cjui nliambiwa sijui kuna taarifa n.k
kwa ufupi huna hoja kabisa na nashangaa ilikuwaje ukawa kiongozi mkubwa hivo wa chama wakati upstairs mweupe sana na kma hawa ndio aina ya viongozi wa chadema tulionao mikoani basi naona dalili za ccm kutawala milele maana sio kwa ujengaji hoja huu hta polepole hashawishiki kukupa ukuu wa wilaya
SHAME SHAME SHAME