CHADEMA, mchungeni Mwenyekiti Mbowe

CHADEMA, mchungeni Mwenyekiti Mbowe

Mwanachadema mfu hongera kwa kuwa mfu wa chama kinachojitahidi kutoa elimu ya uraia hapa nchi kwani mwanachadema yeyote ni vigumu kubishana naye kwa hoja.

Sasa njoo huku tukukate mkia na kukutoa akili ili tukushikie kwani huku kwetu ukiwa na akili sana hatakiwi kwani mwenye akili natakiwa mmoja tuu sisi wengine ni nduyooo sasa hili utaliweza ndugu.

Kwa hiyo Mbowe elimu ya uraia na ujasiri aliyoitoa kwa nchi nzima ilikuwa danganya toto na kwani chadema ina wajumbe wa mashina, madiwani na wabunge wangapi mpaka huyu kijana anazunguka nchi nzima kwa ajili ya kusimika ushawishi ambao tayari majibu yake yanaonekana kututisha sisi ccm kwa hii elimu ya uraia tuliyonayo ambao hatukubali kushikiwa akili.

Hivi hujiulizi kama vyama vingekuwa vimerusiwa kufanya mikutano kama kawaida huyu mwenyekiti wangu ungemsikia wapi tuache unafiki sio mzuri kabisa kwani unamwondolea mtu kujiamini na kuaminiwa na mtu yeyote asiyekubali kushikiwa akili
 
Subira yavuta heri, kuwa na subra nafasi za uteuzi bado zipo
 
1. Hebu tuletee taarifa za fedha za kampuni za Mbowe za miaka kumi iliyopita ili tulinganishe na ulichoandika kuhusiana na ustawi wa kampuni zake wakati wa Magufuli na huko nyuma.

2. Hivi kati ya Dk. Slaa na Mbowe nani alihusika kumleta Lowasa Chadema?
Mkuu aliyemleta el alitamka kwa mdomo wake kwamba amebadilisha gia angani, mara hii umeshalisahau hilo?
 
Benson Mramba nilipoanza kumjua kwa Mara ya kwanza nilimwona ni moja ya vijana wachache wenye ujasiri na moja ya Nuru ya chama pale Temeke na Taifa kwa ujumla.

La hasha, sijui alikuja kuwaje muda mfupi baadae kaja kawa kinyume na matarajio yangu.

Kama ulikuwepo ndani ya chama uliogopa nini kuyasema hayo utuaminisho Leo hii mpaka ujue useme ukiwa mwanachama mfu?

Unasema na kudiriki kutuaminisha kuwa Tuwe na taadhari na Mwenyekiti, sawa hata mke wangu ninaishi nae kwa tahadhari.

Je, Nasi (Wacha nizungumzie nafsi yangu, {Nami}) Niamini mpka Wewe ulipoamua kuwa mwanachama mfu nawe umepokea fedheha (Fedha) ama umeongwa mpaka ukaamua kuwa mfu kwa kushindwa kuwa baridi au moto na kuanza kuwa vuguvugu?

Kwa hakika vijana tunadhihirisha ni jinsi gani asilimia kubwa yetu tunashindwa kuwa viongozi.
 
Kama aliweza kuwasaliti wanachama wote akampokea lowassa ikabidi wanachama wajifanye wanampenda anaweza kufanya lolote
 
CHADEMA inakuuma mazee. Unapata wapi muda wa kuandika wakati umekuwa mwanachama mfu.
 
Mbowe ni mmiliki wa CHADEMA akiondoka na chama kimekufa hana tofauti na Zitto na ACT yake
Chagua Magufuli sio Chagua mgombea wa chama changu ccm. Hapa ndo tulimwoteshea mapembe nani wakumuuliza chochote kwa sasa ndani ya chama chetu. Kwanza tunatakiwa tusimlinganishe Mbowe na Magufuli ndugu .

Mbowe ni mtu aliyeanza siasa akiwa na umri mdogo ambaye anaweza kushabihiana na watu wa umri tofauti na anakubalika na kila rika ktk mijadala yoyote ambayo chama chao kimpa ridhaa ya kuwasilisha kwa sisi wapokeaji mpaka hapa alipo ni Mwanasiasa wa kuigwa. Hebu niambie ktk vyama vyote hapa nchi ni mwenyekiti yupi unaweza kumfananisha na huyu Bwiji wa Siasa za hapa Tz lile la ukweli nitalisimamia kwa ukweli na kuweka ukada pembeni kwani huyu ni mmoja wa Kiongozi mwenye nia ya kuona Tanzania inakuwa nchi yenye neema kwa kila raia.

Chadema ni tishio kwa siasa za hapa kwani ni chama kinachokubalika na kila rika na mtu yeyote ambaye sio mwanachama wa hiki chama lakini anakikubali huwa sehemu yeyote unapoibuka mjadala wa elimu ya uraia huwa hushiriki kutoa elimu kama ambavyo walivyowanachama wa hiki chama yaani wanaodhubutu wa kutosha kama mtu mwenye semina ya jambo flani. Hili nichunguze utaliamini lakini nahisi utakuwa unalijua hili ndo maana sisi ccm kila atakaye kuwa tofauti kimawazo huwa tunamchulia kama mwana chadema kwanini hatuvitaji hivi vyama vingine hapa kuna jambo.

Magufuli sio Mwanasiasa huyu ni Mtendaji kwa hiyo hapa kuna watu wawili tofauti Mwanasiasa na Mtendaji .Na kumbuka mwanasiasa ndo anamchagua Mtendaji ili aweze kufanya utekelezaji ndo maana nasema Magufuli uwezi kumfananisha na Mbowe huyu ni hawa ni watu wawili tofauti kiuwedi

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Inastaajabisha, pale simba anapowaambia swala wamlinde kiongozi wao!

LoRd JeSuS ChRiSt - The Creator Of All.
 
Chagua Magufuli sio Chagua mgombea wa chama changu ccm. Hapa ndo tulimwoteshea mapembe nani wakumuuliza chochote kwa sasa ndani ya chama chetu. Kwanza tunatakiwa tusimlinganishe Mbowe na Magufuli ndugu .

Mbowe ni mtu aliyeanza siasa akiwa na umri mdogo ambaye anaweza kushabihiana na watu wa umri tofauti na anakubalika na kila rika ktk mijadala yoyote ambayo chama chao kimpa ridhaa ya kuwasilisha kwa sisi wapokeaji mpaka hapa alipo ni Mwanasiasa wa kuigwa. Hebu niambie ktk vyama vyote hapa nchi ni mwenyekiti yupi unaweza kumfananisha na huyu Bwiji wa Siasa za hapa Tz lile la ukweli nitalisimamia kwa ukweli na kuweka ukada pembeni kwani huyu ni mmoja wa Kiongozi mwenye nia ya kuona Tanzania inakuwa nchi yenye neema kwa kila raia.

Chadema ni tishio kwa siasa za hapa kwani ni chama kinachokubalika na kila rika na mtu yeyote ambaye sio mwanachama wa hiki chama lakini anakikubali huwa sehemu yeyote unapoibuka mjadala wa elimu ya uraia huwa hushiriki kutoa elimu kama ambavyo walivyowanachama wa hiki chama yaani wanaodhubutu wa kutosha kama mtu mwenye semina ya jambo flani. Hili nichunguze utaliamini lakini nahisi utakuwa unalijua hili ndo maana sisi ccm kila atakaye kuwa tofauti kimawazo huwa tunamchulia kama mwana chadema kwanini hatuvitaji hivi vyama vingine hapa kuna jambo.

Magufuli sio Mwanasiasa huyu ni Mtendaji kwa hiyo hapa kuna watu wawili tofauti Mwanasiasa na Mtendaji .Na kumbuka mwanasiasa ndo anamchagua Mtendaji ili aweze kufanya utekelezaji ndo maana nasema Magufuli uwezi kumfananisha na Mbowe huyu ni hawa ni watu wawili tofauti kiuwedi

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app

mhenge vipi??

naona unaongelea zamani,

chadema ya dr. slaa ndio ina sifa hizo
 
mhenge vipi??

naona unaongelea zamani,

chadema ya dr. slaa ndio ina sifa hizo
Ya zamaipi kwani aliyemleta Slaa chadema ni nani zaidi ya Mbowe tuache upitoshaji mwenyeuwezo wa kusajili tumkubali kwa uwezo wake tuwe wakweli kwa jambo husika. Sasa labda ni kusaidie kimawazo au wewe unisaidie hivi tunapoamua kuzuia upinzani kufanya siasa ktk nchi yao Je ww uoni ya kuwa tunaligawa taifa hili lenye umoja na ni kwa nini tuwazuie wasifanye shughuli za kisiasa wakati ndiyo kazi yao alafu tunajisifia kwa mambo yasiokuwa na competition. Ni kwani tunamwogopa mshindani wetu hapa huoni ya kwamba hatuwezi kiutendaji. Pia tukumbuke wapinzani wetu wametufundisha namna ya kuongoza sasa anayekufundisha kuongoza tumweshimu kwani tukumbuke Mzee Kinana na Mku Nape walienda kwa wananchi tunawaona wanalima, wanapiga Tofali yaani wakishiriki kufanya shughuli za kijamii Je pasipo chadema wangelikwenda kufanya hizo kazi wakati sisi tumeandaliwa kutawala kwa mikwara tuu. Nikuambie tuu ndugu yakuwa Itikadi inaishi rohoni kama zilivyo imani zingine kwa hiyo tunawaogopa wamekaa na itikadi zao na wanazidi kutoa elimu ya uraia pale inapopatikana nafasi mfano si tunaona huko vyuoni anachokifanya mpaka tunawaona wivu ktk harakati zao

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
mhenge vipi??

naona unaongelea zamani,

chadema ya dr. slaa ndio ina sifa hizo
Mbowe kàbadiri katiba ili aongezee miaka yote kila anayetaka kugombea uenyekiti ana undiwa zengwe Mbowe chadema kaifanya kuwa mradi wake binafsi na amekuwa na project za kula ruzuku project za viti maalum ambazo kageuza kuwa vitu.maalum atawezaje kuicha chadema ? Mbowe huyo alipewa magari mia moja na wadau waliopo Japan yaweze kusaidia chama wakati wa uchaguzi 2015 Mpaka leo haijulikani kupeleka wapi kama kuna mtu fisadi umjuae Tanzania Mbowe ni number moja nashangaa hata huyu anjiita chadema mfu bdo anatoa maonyo ondoka huko haraka hicho sio chama. Wanachama wanajiita kamanda mtu hajawahi kuwa kuruta au hata kupitia mgambo huo kama sio utapeli yaani unajiita kamanda kamanda wa nini hawajui maana ya kamanda nini una blackmail wanachama wajifanye makamanda iliiwe nini? Cheo cha kijeshi anajipachika anatofauti gani na wanao gushi vyeti? Nani atabisha mtu akisema chadema ni Sacoss ya Mbowe kwa swala la wabunge wa East Africa? Waziwazi bila aibu anapendelea rafiki zake bdae analeta wanawake wote kutoka kasikazini huyu mtu ni wa kumwogopa Mungu amepishilia mbali nchi hii kuchukuliwa na watu wa aina hii leo tungeshuhudia mabaya mengi

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kamanda mbowe nafanya mengi mazuri lkn nadhan Ni wakati wake akapumzika kwa sasa akawaachia kijiti na wengine.
 
Hata mtoto wa shule ya msingi anajuwa Lowassa alilipa hela ajiunge na CHADEMA agombee urais, sio siri wala kificho, swala hizo hela zilienda wapi?! Au ndizo zile za nje?!
 
Wahenga walisema “Mtu Mzima akilia ujue kuna Jambo”

Katika siku za hivi karibuni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA akiwa jimboni kwake Hai amesikika akilalama au kujinasibu kuwa asingekuwa na roho ngumu angekuwa ameshaachana na upinzani. Nukuu iliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii hususani kanda ya Kaskazini ilisomeka ifuatavyo “ Upinzani ni wito, wenye roho nyepesi hawawezi, kama ningekuwa napenda Fedha, nina roho nyepesi, ningeshachukua hizo pesa na ningeshakimbia kabisa upinzani” Habari hii pia iliandikwa kwenye gazeti la Mwananchi.

Habari hii haikuwa mpya kwangu kwani inaonekana Mh Mbowe amekuwa akiirudia sehemu mbalimbali anapokutana na viongozi wa Chama kwa malengo ya kuwajengea imani juu yake hususan kwenye swala zima la tamaa ya fedha. Maslani akiwa mkoani Tanga wakati wa Uchaguzi aliouvunja kwasababu zake binafsi wa Kanda ya Kaskazini Mh Mbowe inasemekana aliwaambia baadhi ya viongozi kuwa ameshawishiwa apewe Bilioni 70 ili aivuruge CHADEMA (Niliambiwa na kiongozi mmoja ambaye ni rafiki yangu mimi ninayemuamini) Baada ya kusikia habari hii ilinishtua sana na kuogopa kuwa huenda Fisi anajaribiwa kwa Mfupa.

Aidha Dr Mashinji Katibu Mkuu wa CHADEMA alitoa taarifa kwa Umma siku za karibuni pia kuwa kuna Wabunge wa CHADEMA wanataka kuhongwa ili wajiuzulu ubunge. Hakutuambia kama Mwenyekiti wake nae ni miongoni mwao au la.

Maoni yangu kwa mfululilizo huu ni kuwa Wanachama na viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuwa macho sana na Mwenyekiti wao katika wakati huu kuliko wakati mwingine wowote kwasababu zifuatazo:-

1. Mbowe ametikiswa au kutikisika kiuchumi katika awamu hii kuliko ambavyo imewahi kumtokea wakati mwingine wowote. Billcanas imefungwa, gazeti halifanyi vizuri sana, Madeni ya malimbikizo ya kodi na shamba la mboga nalo limeharibiwa.

2. Awamu ya nne siasa ilikuwa ni mradi na fursa kwa viongozi wengi na makada wa vyama hususan vya upinzani. Lipo andiko la Mh Zito liliwahi kuonekana mtandaoni kuonyesha kuwa kuna wana CCM wa wakati huo waliokuwa wakiwapa fedha viongozi wakuu wa upinzani kwa maslahi yao. Mbowe amekuwa Mbunge katika awamu yote ya nne na biashara zake zikiendelea vizuri pia taasis kama TAKUKURU na TRA hazikuwa moto kama wakati huu. Ukaguzi kwenye vyama nao ulikuwa mdogo tofauti na ninavyotarajia kwa wakati huu.

3. Mbowe hajawahi kupata shida akiwa yoyote ya kiuchumi au msukosuko wa jela au mahabusu akiwa CHADEMA. Kuna wahenga wa Chama waliniambia miaka ya 2004 Mbowe alipata mtikisiko wa ndani ya Chama wakati huo akiwa amepoteza Ubunge wake huko Hai kwa hasira akatishia kuhamia CCM miaka hiyo. (Maneno ya Wahenga hayo sio yangu) Hii inamaanisha kuwa maslahi yake ndani ya upinzani yakidhibitiwa basi anaweza kufanya lolote kuyanusuru.

4. Ujio wa Mawaziri Wakuu wawili wastaafu nao ni Changamoto kwa Chama. Mawaziri hawa wanahesabika kama wasaliti ndani ya CCM na dola pia. Nakumbuka nguvu kubwa iliyotumiwa na CHADEMA kupambana na Zitto Kabwe kwa hoja au dhana kuwa Zitto ni Msaliti. Naamini kanuni ni hiyo hiyo hata CCM pia. So by Compromising or by Force Mbowe lazima atikiswe.

5. Dr Slaa wakati akijitoa kwenye Ukatibu Mkuu alidai kuwa alitaka kuhongwa Bilioni 5 ili ampokee Lowassa akakataa. Dr Slaa akadai anashangaa Mwenyekiti wake alivyokubali kumpokea Lowassa wakati alimjulisha juu ya swala la yeye kutaka kupewa fedha.

6. Dili ya Bilioni saba (7) ndani ya Chama nayo nimeitia mchanga naamini TAKUKURU watakuwa wanaifuatilia kwa karibu.

Kwa hoja hizo mimi binafsi simuamini Mbowe kabisa linapokuja swala la fedha. Na kwa yowe hili analolipiga sasa inaonyesha kabanwa mahali. Wito wangu wanachama na viongozi mchungeni Mwenyekiti wenu asije kutusaliti tena watanzania. Ukiona mtu mzima Analia ujue kuna jambo

.
Mbowe anazimudu sana siasa za upinzani kusini mwa jangwa la Sahara.Kama ungejua ni namna gani chama dola kinavyotumia mapandikizi katika vyama vya upinzani...ungekaa kimya tu.

Post sent using JamiiForums mobile app

 
Back
Top Bottom