Chimbuko la CCM ni "Mapinduzi", na hata kwa jina inajieleza kabisa kuwa mantiki na falsafa yake ni "Mapinduzi"..... wakati kwa CHADEMA ni "Demokrasia na Maendeleo"....! Nayo kwa jina hujieleza.....! Zaidi ni kwamba, mapinduzi wanayoita CCM hayajawahi kufafanuliwa kama ni mapinduzi ya namna gani hmaanishwa na CCM.... matokeo yake nchi ikapinduliwa miguu juu, kichwa chini...! Kwa hiyo kama CCM wanavyosema "Amani" ni kiini macho tu....! Hebu fikiria; Ukiwa baba, kila siku ukifika nyumbani, watoto na mama yao pamoja na wafanyakazi wako, huku wakiwa wameshinda njaa kutwa nzima, wanapata makwenzi walau mojamoja..... lakini kwa kuwa hakuna mwenye ubabe wa kukurudishia, wala kukuchukia hatua, wanabaki kuumia bila jinsi....! Sasa nikuulize, katika ile nyumba yako kutakuwa na amani? Au ni utulivu tu umetawala....? Hiyo ni picha halisi ya CCM kwa sababu wakiwa watawala wa nchi, lakini wananchi wakiteseka bila huduma yoyote, njaa, nk.... hutumia ubabe kuwazuia wananchi hao kufikisha hisia zao panapohusika.....! Sasa amani iko wapi? Lakini vilevile, kwa maneno mengine, "Demokrasia" huleta amani hasa pale "Maendeleo" yanapowezekana kwa kila mmoja....!