CHADEMA-Maendeleo, CCM-Amani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA-Maendeleo, CCM-Amani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dume la Mende, Jun 9, 2011.

 1. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wakati CCM wanajaribu kudumisha amani, Chadema wana mtazamo tofauto kwamba amani bila maendeleo ni bure. Je, maendeleo bila amani itakuwa vipi? Basi nashauri vyama hivi na wadau wao, wajaribu ku-synchronize the two, yaani hivi vitu viwili, amani na maendeleo, vinategemeana.
   
 2. g

  gambatoto Senior Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maendeleo kwanza, amani baadaye.
   
 3. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa Tanzania, Amani = Upumbavu/Ujuha/Ujinga/Umasikini/Ufisadi/Mtaji wa CCM/
   
 4. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa mkuu, maendeleo huku tunatimuana kwa mapanga raha iko wapi?
   
 5. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kukosa amani si lazima kumaanisha watu wanakurupushana kwa mapanga mkuu. kukosekana kwa amani ni dhana pana sana ambayo watu wanaitizama kwa wepesi.
   
 6. S

  Salimia JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hata maandiko matakatifu yanasema wazi kwamba, ni heri kulala juu ya paa na amani, kuliko ndani ya nyumba na ugomvi au vita.
   
 7. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  be specific. maandishi gani?
   
 8. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye ekundu: chadema hawasemi amani bila maendeleo ni bure bali wanasema "amani bila haki ni bure". Na kutoka hapo tunaweza kumalizia kwamba "amani bila haki hakuwezi kuwa na maendeleo". Haki ni msingi wa maendeleo na amani ya kweli. Kukikosekana haki hakuwezi kuwa na maendeleo wala amani ya kweli.
   
 9. S

  Salimia JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yes,, please elucidate so we know dhana hiyo.
   
 10. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Chimbuko la CCM ni "Mapinduzi", na hata kwa jina inajieleza kabisa kuwa mantiki na falsafa yake ni "Mapinduzi"..... wakati kwa CHADEMA ni "Demokrasia na Maendeleo"....! Nayo kwa jina hujieleza.....! Zaidi ni kwamba, mapinduzi wanayoita CCM hayajawahi kufafanuliwa kama ni mapinduzi ya namna gani hmaanishwa na CCM.... matokeo yake nchi ikapinduliwa miguu juu, kichwa chini...! Kwa hiyo kama CCM wanavyosema "Amani" ni kiini macho tu....! Hebu fikiria; Ukiwa baba, kila siku ukifika nyumbani, watoto na mama yao pamoja na wafanyakazi wako, huku wakiwa wameshinda njaa kutwa nzima, wanapata makwenzi walau mojamoja..... lakini kwa kuwa hakuna mwenye ubabe wa kukurudishia, wala kukuchukia hatua, wanabaki kuumia bila jinsi....! Sasa nikuulize, katika ile nyumba yako kutakuwa na amani? Au ni utulivu tu umetawala....? Hiyo ni picha halisi ya CCM kwa sababu wakiwa watawala wa nchi, lakini wananchi wakiteseka bila huduma yoyote, njaa, nk.... hutumia ubabe kuwazuia wananchi hao kufikisha hisia zao panapohusika.....! Sasa amani iko wapi? Lakini vilevile, kwa maneno mengine, "Demokrasia" huleta amani hasa pale "Maendeleo" yanapowezekana kwa kila mmoja....!
   
 11. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Amani unayoizungumzia ni ipi?
  Madini asilimia 3%
  Foleni massa matatu kwenda kazini
  Mlo mmoja kwa siku
  Amani ya kikaburu
  Amani ya mabomu ya mbagala na Gongs
  Amani ya wengine kulipwa millioni 12 na wewe elfu 20
  Amani gani?:glasses-nerdy:
   
 12. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  CCM hawahubiri amani ila wanavuruga amani kwa matendo yao..
   
 13. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mithali 25:24
  Pia Mithali 17:1 Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Acha kupotosha watu...
   
 15. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  hivi maana halisi ya amani unaifahamu!?, Hapa Tanzania amani hakuna bali kuna utulivu amani haiwezi kuwepo sehemu ambapo hakuna haki, kunaubabe, kuna dhuluma, kuna watu wanaofikiria kwamba bila wao hakuna mtawala mwingine, watu wengine wapo kwenye Neema wakati wengine wamechoka kwa ugumu wa maisha huwezi kunishawishi nikakubali kwamba hapa kuna amani.

  Amani wanayohubiri ccm ni kwamba wao waendelee kutawala, kuiba fedha za umma, kugawana madini yetu, kurithishana utawala vizazi na vizazi, waendelee kuwaona watanzania mabwege, wazidi kuwanyima watanzania elimu ya kujitambua. na pia watanzania wazidi kukosa huduma bora za kijamii, hii ndiyo amani wanayotaka tudumu nayo hawa ccm.

  Chadema kinaamini kwamba Haki ni msingi wa maendeleo na maendeleo ndiyo yanaleta amani, bila haki hakuna amani, na ndicho kilichopo hata huko kwa waarabu hakuna haki na ndio maana hawana amani.

  Hakuna Chama kilianzishwa ili kitawale daima so Haki, maendeleo na amani bila ccm vinawezekana watanzania tuchukue hatua.
   
 16. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Vipi mbona unakurupuka ghafla tena? kipi unachojua wewe? Kupinga maoni ya wenzio bila kuweka ya kwako ni sawa na kumkonyeza mtu gizani
   
 17. M

  MPG JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa serikali ya CCM upumbavu mbele,amani ya fikra finyu,kubadilisha uongo kuwa ukweli,ulimbukeni mwingi wa viongozi wa CCM,kuwadanganya watanzania na kuwadhurumu mali zao na kuwafanya kuwa maskin,Chadema fikra mbele na kuwaletea maendeleo watanzania.
   
 18. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  CHADEMA - Mwananchi amka usingizini, CCM-Tulia uliwe.
   
 19. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Lahaula lakwata. Kama ni hivyo basi, una maana CCM ni matajiri sana? Mbona wengine twawaona choka mbaya tu?
   
 20. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,665
  Trophy Points: 280
  Amani huku tunalala njaa,raha iko wap?
   
Loading...