CHADEMA-Maendeleo, CCM-Amani

Wakati CCM wanajaribu kudumisha amani, Chadema wana mtazamo tofauto kwamba amani bila maendeleo ni bure. Je, maendeleo bila amani itakuwa vipi? Basi nashauri vyama hivi na wadau wao, wajaribu ku-synchronize the two, yaani hivi vitu viwili, amani na maendeleo, vinategemeana.

Haya Magamba ya Nape, tuyaondoe humu JF. Kwa kutochangia post zao au kwa kuyapinga.
 
Haya Magamba ya Nape, tuyaondoe humu JF. Kwa kutochangia post zao au kwa kuyapinga.
Mbona mtoa mada hajaonesha kuwa upande woote? wewe umejuaje au kigezo gani umetumia kum categorize kwamba ni wa Nape?
 
Wakati CCM wanajaribu kudumisha amani, Chadema wana mtazamo tofauto kwamba amani bila maendeleo ni bure. Je, maendeleo bila amani itakuwa vipi? Basi nashauri vyama hivi na wadau wao, wajaribu ku-synchronize the two, yaani hivi vitu viwili, amani na maendeleo, vinategemeana.

"Penye njaa siku zote Amani hutoweka kupitia dirishani"Hivi je unayajua mawazo ya mtu masikini juu ya mstakabali wa maisha yake?.Fikiri kabla ya kuandika
 
Haya Magamba ya Nape, tuyaondoe humu JF. Kwa kutochangia post zao au kwa kuyapinga.

Stein, sifa zao ni zipi ilinisije nikajikuta na pambana nao, maana mimi nawachukia wote wenye kutetea mageuzi ya kuvua Gamba.
 
Wakati CCM wanajaribu kudumisha amani, Chadema wana mtazamo tofauto kwamba amani bila maendeleo ni bure. Je, maendeleo bila amani itakuwa vipi? Basi nashauri vyama hivi na wadau wao, wajaribu ku-synchronize the two, yaani hivi vitu viwili, amani na maendeleo, vinategemeana.

Sio kweli. hiyo notion yako ni kama inasema kwa CHADEMA kitu muhimu ni maendeleo na si amani... SIO KWELI. CDM inathamini Amani lakini pia inatambua umuhimu na ulazima wa kupigania maendeleo ya wananchi wake. Ingekuwa ni kama unavyolazomisha wewe iwe basi CDM ingeletaje maendeleo kwenye machafuko?

Kwa upande wa CCM ulichosema ni kweli, wao msingi mkubwa ni 'amani' tena ukiwaambia waitafasili amani watakwambia ni absence of war... Kwa maana nyingine hata hicho wanachoking'ang'ania kama msingi hawakijui!
 
Chimbuko la CCM ni "Mapinduzi", na hata kwa jina inajieleza kabisa kuwa mantiki na falsafa yake ni "Mapinduzi"..... wakati kwa CHADEMA ni "Demokrasia na Maendeleo"....! Nayo kwa jina hujieleza.....! Zaidi ni kwamba, mapinduzi wanayoita CCM hayajawahi kufafanuliwa kama ni mapinduzi ya namna gani hmaanishwa na CCM.... matokeo yake nchi ikapinduliwa miguu juu, kichwa chini...! Kwa hiyo kama CCM wanavyosema "Amani" ni kiini macho tu....! Hebu fikiria; Ukiwa baba, kila siku ukifika nyumbani, watoto na mama yao pamoja na wafanyakazi wako, huku wakiwa wameshinda njaa kutwa nzima, wanapata makwenzi walau mojamoja..... lakini kwa kuwa hakuna mwenye ubabe wa kukurudishia, wala kukuchukia hatua, wanabaki kuumia bila jinsi....! Sasa nikuulize, katika ile nyumba yako kutakuwa na amani? Au ni utulivu tu umetawala....? Hiyo ni picha halisi ya CCM kwa sababu wakiwa watawala wa nchi, lakini wananchi wakiteseka bila huduma yoyote, njaa, nk.... hutumia ubabe kuwazuia wananchi hao kufikisha hisia zao panapohusika.....! Sasa amani iko wapi? Lakini vilevile, kwa maneno mengine, "Demokrasia" huleta amani hasa pale "Maendeleo" yanapowezekana kwa kila mmoja....!
mapinduzi ya kijani.
 
Wanadanganywa wabongo kuwa amani itapotea ili waendelee kudhoofisha uchumi.
 
Amani haiji kwa kutumia mitutu ya buduki, kwa kuua watu wasio na hatia (Tarime, Arusha, Pemba etc.) na kuwatisha wafanyakazi wanapodai haki zao (mbayuwayu). Amani haiji kwa kutumia tume ya uchaguzi ili kuchakachua matokeo! Amani ya kweli inatoka mioyoni mwa watu. Ccm wamekuwa wakijitapa kwamba wanadumisha amani lakini ukweli ni kwamba wamekuwa wakiivuluga kwa kuendeleza umasikini wa watanzania, kwa kukumbatia mafisadi, kwa kuongeza kwa kasi ya ajabu pengo lae aliye nacho na asiye nacho (kipato cha chini na cha juu)
 
kwaiyo bora amani kwanza.au mi naona vyote vinategemeana kama pete na kidore
 
'Piece does not mean absence of war alone, its more that' kwa hiyo usifikiri kwa sababu Tanzania hakuna vita basi ndo amani yenyewe, amani lazima iendane na maendeleo ya watu wote huku tofauti kati ya walichonacho na wasionacho ikiwa ndogo kadiri inavyowezekana,lakini kwa hali hii tuliyonayo ufisadi kila mahali,ugumu wa maisha ndo kwanza unaongezeka, tofauti ya walichonacho na wasichonacho inazidi kua kubwa nk huwezi kuiita amani ya kujivunia bali ni bomu linalosubiri kulipuka.
 
wakati ccm wanajaribu kudumisha amani, chadema wana mtazamo tofauto kwamba amani bila maendeleo ni bure. Je, maendeleo bila amani itakuwa vipi? Basi nashauri vyama hivi na wadau wao, wajaribu ku-synchronize the two, yaani hivi vitu viwili, amani na maendeleo, vinategemeana.

Tanzania haina amani ila ina utulivu... Tunahitaji maendeleo ili tuwe na amani ya kweli!?
 
Wakati CCM wanajaribu kudumisha amani, Chadema wana mtazamo tofauto kwamba amani bila maendeleo ni bure. Je, maendeleo bila amani itakuwa vipi? Basi nashauri vyama hivi na wadau wao, wajaribu ku-synchronize the two, yaani hivi vitu viwili, amani na maendeleo, vinategemeana.
Mkuu amani na maendeleo vinaenda pamoja.
Huwezi kudumisha amani wakati maendeleo hayapo, labda kama kuna maana nyingine ya maendeleo upande wako.
 
Matumizi ya Neno "AMANI" ndiyo silaha pekee waliyobaki nayo mafisadi ccm. Ni neno hilo ndilo hulitumia wapumbavu wa ccm kuwatishia wananchi wapenda haki na maendeleo. Wananchi wasio na elimu na wajinga ktk kufikri. Lakini ni lazima tujue, amani ni njia tosha ya kuyafikia maendeleo. Hatuna amani tz. Kama kungekuwa na amani basi tungekuwa tumeendelea. Lakini, mmmh kila kukicha ni bora ya jana. Amani ni tunda la haki. Haki haipo tz. Kama nchi ni lazima tuitafute haki, baada ya haki tutaipata amani ya kweli na maendeleo yatakuja automatically. Ccm wasitudanganyie amani, amani, haki na maendeleo vyote havipo tz.
 
Mkuu amani na maendeleo vinaenda pamoja.
Huwezi kudumisha amani wakati maendeleo hayapo, labda kama kuna maana nyingine ya maendeleo upande wako.
Mkuu mbona unapotoka? mimi sentensi yangu ya mwisho inasomeka hivi:
Basi nashauri vyama hivi na wadau wao, wajaribu ku-synchronize the two, yaani hivi vitu viwili, amani na maendeleo, vinategemeana.
Ambayo ni sawa kabisa na sentensi yako ya kwanza. Sasa sentensi yako kwenye green haina mashiko kabisa
 
'Piece does not mean absence of war alone, its more that' kwa hiyo usifikiri kwa sababu Tanzania hakuna vita basi ndo amani yenyewe, amani lazima iendane na maendeleo ya watu wote huku tofauti kati ya walichonacho na wasionacho ikiwa ndogo kadiri inavyowezekana,lakini kwa hali hii tuliyonayo ufisadi kila mahali,ugumu wa maisha ndo kwanza unaongezeka, tofauti ya walichonacho na wasichonacho inazidi kua kubwa nk huwezi kuiita amani ya kujivunia bali ni bomu linalosubiri kulipuka.
Mkuu nadhani hapo kwenye wekundu ulitaka kuandika "Peace"? na hapo penye kijani bila shaka ingependeza ingesomeka "it is more than that"? Wakati mwingine ni afadhali tuienzi lugha yetu ya kiswahili
 
soma thread ya ushauri wa Ulimwengu kwa Slaa
 
Mkuu nadhani hapo kwenye wekundu ulitaka kuandika "Peace"? na hapo penye kijani bila shaka ingependeza ingesomeka "it is more than that"? Wakati mwingine ni afadhali tuienzi lugha yetu ya kiswahili
Mkuu nashukuru mpaka umeona hizo corrections ujumbe utakua umefika,ulikua ni msisitizo tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom