hapa naona udhaifu mkubwa sana kufanywa na kiongozi wa juu wa taasisi.Mwigulu sialimpa 50,000/- ili afanye hiyo kazi......?! Subiri Mwigulu atamtoa tu, sasa hivi anaona soo....!
Hiyo ndio ccm ya Mwigulu haina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.!!
Pole Mwigulu a.k.a Hammy-D, najua ndio mmemaliza kikao cha majukumu ya utoto wenu hapo lumumba na kila mtu kujaziwa bundle tayari kwa kueneza propaganda za kitoto mtandaoni eti mnasema mnapambana na Chadema mitandaoni. Kwanza nikuombe uwaambie viongozi wako wa CCM wasigeuze magereza zetu kama sehemu za kutesea watanzania wenzetu ambao ama wamekosa maadili huku uraiani ama wamesingiziwa. Ni jambo la aibu wewe kushabikia na kusema kwamba mahabusi/gerezani ni mahali pakutesea watu na sio mahali pakurekebishia maadili. Tunaomba haki za binaadamu walitolee jicho hili tatizo ambalo Hamy-D kwa kutojua anadhani ni sifa kusema mahabusu ni sehemu ya kutesea. La Pili na la msingi ni kwamba wewe na CCM yako kama mna roho nzuri na mnawatumikia watanzania ni muda wenu kumtoa Ludovick huku kwenye mateso gerezani kwa kumuwekea dhamani maana wewe Mwigulu a.k.a Hammy-D ulikuwa ukimtumia hela kwa njia ya mpesa. Mbona hukuwa kuwashauri Chadema wamtumie hela kwa mpesa wewe ndio ulikuwa mwema kwake kwa kumtumia. Acheni utoto na siasa za kipumbavu kwa kutunga kesi ambazo hamtaki kwenda kutoa ushahidi mahamani.WanaJF!
Leo ni siku ya kesi ya bwana Lwakatare kusikilizwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini kesi imehairishwa mpaka July 22, 2013.
Pamoja na hayo, mshitakiwa na.2 bwana Ludovick Rwezaura ameshindwa kupata dhamana kwa sababu ya kutokamilika kwa nyaraka za dhamana, ingawa dhamana yake iko wazi kabisa.
Bwana Ludovick akiwa nje ya mahakama, ameonekana akiwa mnyonge na alikuwa akilia sana kwa uchungu huku akilalamika ndugu zake (ambao hawakufika mahakamani) hawafatilii dhamana yake.
Kwa hali kama hiyo, kijana Ludovick anaendelea kusota gerezani na kuzidi kuangamia, kwani wote sisi ni wanaadamu na tunajua makali ya maisha ya gerezani.
Rai yangu kwa CHADEMA; haijarishi kijana Ludovick kama alikuwa mwajiriwa kwa CHADEMA kimkataba ama alikuwa volunteer, jambo la msingi ni kwamba alikuwa nakitumikia CHADEMA kwa moyo wake wote na nguvu zake zote. Ludovick alijitoa kwa CHADEMA kwa namna yake, ni kijana ambae alikuwa bega kwa bega na Dr Slaa kiutendaji na vile vile alikuwa kama mtoto kwa Dr Slaa.
Katika hali kama hiyo sikutarajia kamaCHADEMA kinaweza kumtema na kumkataa kabisa bwana Ludovick Rwezaura. Kwani wote tunafahamu kuwa, kosa aliadhibiwi kwa ubaya, bali kosa dawa yake kukosolewa. Sasa kwanini CHADEMA wana muadhibu kijana Ludovick kwa ubaya? kwanini wasimsaidie hata kwa dhamana ili aweze kutoka kwenye 'jehanamu' ya duniani?
View attachment 101283Kijana Ludovick akionekana amenyong'onyea leo mahakani, pembeni yake ni bwana Lwakatare wakiwa na askari magereza.
Bwashee kumbe una huruma!?
Simply wasiliana na Mwigulu Nchemba ataachiwa bila makaratasi yoyote yale ya dhamana. malipo ni hapahapa Duniani hizi ni sheria za karma.