CHADEMA, Ludovick Rwezahula anaangamia mahabusu, utu uko wapi?

CHADEMA, Ludovick Rwezahula anaangamia mahabusu, utu uko wapi?

Status
Not open for further replies.

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,829
WanaJF!

Leo ni siku ya kesi ya bwana Lwakatare kusikilizwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini kesi imehairishwa mpaka July 22, 2013.

Pamoja na hayo, mshitakiwa na.2 bwana Ludovick Rwezahula ameshindwa kupata dhamana kwa sababu ya kutokamilika kwa nyaraka za dhamana, ingawa dhamana yake iko wazi kabisa.

Bwana Ludovick akiwa nje ya mahakama, ameonekana akiwa mnyonge na alikuwa akilia sana kwa uchungu huku akilalamika ndugu zake (ambao hawakufika mahakamani) hawafatilii dhamana yake.

Kwa hali kama hiyo, kijana Ludovick anaendelea kusota gerezani na kuzidi kuangamia, kwani wote sisi ni wanaadamu na tunajua makali ya maisha ya gerezani.

Rai yangu kwa CHADEMA; haijarishi kijana Ludovick kama alikuwa mwajiriwa wa CHADEMA kimkataba ama alikuwa volunteer, jambo la msingi ni kwamba alikuwa ana kitumikia CHADEMA kwa moyo wake wote na nguvu zake zote. Ludovick alijitoa kwa CHADEMA kwa namna ya pekee, ni kijana ambae alikuwa bega kwa bega na Dr Slaa kiutendaji na vile vile alikuwa kama mtoto kwa Dr Slaa.

Katika hali kama hiyo sikutarajia kama CHADEMA kinaweza kumtema na kumkataa kabisa bwana Ludovick Rwezaura. Kwani wote tunafahamu kuwa, kosa aliadhibiwi kwa ubaya, bali kosa dawa yake kukosolewa. Sasa kwanini CHADEMA wana muadhibu kijana Ludovick kwa ubaya? kwanini wasimsaidie hata kwa dhamana ili aweze kutoka kwenye 'jehanamu' ya duniani?

Maamuzi haya ya kumtupa mkono kijana Ludovick katika hali hii mbaya inayo mkabili, inajenga wasiwasi mkubwa kwa vijana wengi walio CHADEMA juu ya hatma yao endapo wakikosea jambo. Je, chama kitawasaidia kwa lolote? Ni wakati vijana wakawa makini sana na namna ambavyo CHADEMA na viongozi wake wana shughulikia nidhamu na makosa ya wanachama wao, hiki anacho fanyiwa Ludovick, hakina tofauti sana na walicho fanyiwa Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.

IMG-20130708-WA0000.jpg Kijana Ludovick akionekana amenyong'onyea leo mahakamani, pembeni yake ni bwana Lwakatare wakiwa na askari magereza.
 
kama kweli unauchungu kwanini usiende kumtolea dhamana? kinacho mtafuna ni usaliti wake. na kitu nilichokuwa nadhani na kinanipa yawezekana kuwa ni kweli. huyu jamaa inaonesha alishiriki moja kwa moja kumpiga kibanda, na hivyo kuepuka damu zilizo kuwa zimemrukia, akavua nguo kisha akadai amnyang'anywa mpaka nguo. wakumuomba kumtolea dhamana ni mwigulu.
CCM wamemgeuza jamaa kama toilet paper, na walichokuwa wakikikuthudia kuhusu ugaidi hawajafanikiwa. Usimuhusishe Dr. slaa na usaliti!
 
Kama Mwigulu alikuwa anamtumia pesa kipindi kile anashindwa nini leo kumwekea dhamana mshirika wake huyo? Hapo asiye na huruma na utu ni nani? Ni hao unaowalaumu au huyo aliyemtelekeza baada ya kumtumia kama mpira wa akina baba?
 
Why CHADEMA na sio Mwigula Nchemba mfuga mbwa? acha unafiki mto hoja nakubaliana na aliyekushauri ukamlipie wewe.
 
Mdhamana ni jukumu la mwigulu et al, ile elfu 50 aliyo ituma kupitia m-pesa ilikuwa ya kushika kamera na kurekodi tu kazi ambayo aliitimiza!.
 
HAMMY-D, CCM ndio walivyo, ukishawafanyia kazi yao wanakutosa, subiri zamu yako wewe na wenzako hasa yule jamaa anayeongozana na Mwigulu kuonesha majeraha ya tindikali!
 
Hakuna ye yote mwenye akili timamu ambaye atakubaliana na rafiki yako au mwezi aliyegeuka adui mwangamizi. Kama ni shauri ya kushabikia kiitikadi okay lakini hali halisi Ludovick anaanza kutumikia adhabu yaka hapa hapa duniani.

Kuna majeshi matatu serikalini ambayo ni
  • Jeshi la wananchi kulinda taifa na mipaka ya nchi
  • Jeshi la Polisi kulinda amani na usalama wa raia
  • Usalama wa taifa majasusi wa serikali
  • Kila serikali duniani inayo majeshi yote matatu,
    • Serikali nyingine zimeongeza jeshi jingine la uchunguzi kama Marekani FBI, Tanzania TAKUKURU kutokana na jeshi la kijasusi kutofanya mambo yake kwa uwazi na hivyo pengine kusababisha mambo muhimu kutofanya kazi vizuri inavyotakiwa.

Usalama wa Taifa ni jeshi ambalo si mali ya serikali kama wengi tunavyofikiria, ni jopo la dunia ndio wana mtandao po pote. Tatizo kwa vile ni jeshi la siri hapo hakuna mambo ya uwazi, na pale mwanajeshi yanapomsibu ajua kupigana peke yake ama kushinda au kushindwa tofauti na majeshi mengine ambayo yako kwa uwazi na itokeapo haki za askari kulindwa abasi atalindwa kwa uwazi. Jeshi la siri haliwezi kusimama mahakamani na ikibidi inatakiwa watumie njia ya kudai haki kama raia mwengine hilo hufanyika kwa mtu binafsi si jambo lenyewe kama ilivyo kwa majeshi mengine kwa uwazi kuvunjiwa haki zake.

Ludovic katumiwa na hao na leo waliomtumia hawana haja naye, walimhitaji walipotaka huduma yake. Akishatumika basi kila mtu kivyake na sasa abaki kusota huko maana aliyataka mwenyewe, alikuwa na uhuru wa kuchagua kwa vile ni mtu mzima mwenye akili timamu. Upande aliochagua ndio huo na yanayomkuta ni kutokana na utashi wake mwenyewe.

Wazoefu hufanya kazi hiyo kwa dau kubwa, yeye alikubali kupimiwa vipande vya fedha 50,000 na leo kwa matatizo yaliyompata pesa hiyo aliyopewa na mwigulu haipo kwani hata ingekuwepo haitoshi kumwekea dhamana mahakamani.

Wapo wapi akini Mwigulu Mchemba waliompa vitendea kazi? Wapo wapi akina Michuzi waliojigamba kufanikisha mpango huo?
 
Hiyo ndio ccm ya Mwigulu haina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.!!
 
Mwigulu sialimpa 50,000/- ili afanye hiyo kazi......?! Subiri Mwigulu atamtoa tu, sasa hivi anaona soo....!
hapa naona udhaifu mkubwa sana kufanywa na kiongozi wa juu wa taasisi.
hivi katika 'mpango nyeti' kama huu aliwezaje kumtumia mtekelezaji pesa kwa simu yake bila kushtuka kuwa itajulikana kirahisi na kurahisisha ushahidi!?

 
Badilisha title yako, pale ulipoandika CHADEMA andika Mwigulu nadhani hapo ndipo utaonekana walau umemuenea huruma Ludovick.
 
WanaJF!

Leo ni siku ya kesi ya bwana Lwakatare kusikilizwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini kesi imehairishwa mpaka July 22, 2013.

Pamoja na hayo, mshitakiwa na.2 bwana Ludovick Rwezaura ameshindwa kupata dhamana kwa sababu ya kutokamilika kwa nyaraka za dhamana, ingawa dhamana yake iko wazi kabisa.

Bwana Ludovick akiwa nje ya mahakama, ameonekana akiwa mnyonge na alikuwa akilia sana kwa uchungu huku akilalamika ndugu zake (ambao hawakufika mahakamani) hawafatilii dhamana yake.

Kwa hali kama hiyo, kijana Ludovick anaendelea kusota gerezani na kuzidi kuangamia, kwani wote sisi ni wanaadamu na tunajua makali ya maisha ya gerezani.

Rai yangu kwa CHADEMA; haijarishi kijana Ludovick kama alikuwa mwajiriwa kwa CHADEMA kimkataba ama alikuwa volunteer, jambo la msingi ni kwamba alikuwa nakitumikia CHADEMA kwa moyo wake wote na nguvu zake zote. Ludovick alijitoa kwa CHADEMA kwa namna yake, ni kijana ambae alikuwa bega kwa bega na Dr Slaa kiutendaji na vile vile alikuwa kama mtoto kwa Dr Slaa.

Katika hali kama hiyo sikutarajia kamaCHADEMA kinaweza kumtema na kumkataa kabisa bwana Ludovick Rwezaura. Kwani wote tunafahamu kuwa, kosa aliadhibiwi kwa ubaya, bali kosa dawa yake kukosolewa. Sasa kwanini CHADEMA wana muadhibu kijana Ludovick kwa ubaya? kwanini wasimsaidie hata kwa dhamana ili aweze kutoka kwenye 'jehanamu' ya duniani?

View attachment 101283Kijana Ludovick akionekana amenyong'onyea leo mahakani, pembeni yake ni bwana Lwakatare wakiwa na askari magereza.
Pole Mwigulu a.k.a Hammy-D, najua ndio mmemaliza kikao cha majukumu ya utoto wenu hapo lumumba na kila mtu kujaziwa bundle tayari kwa kueneza propaganda za kitoto mtandaoni eti mnasema mnapambana na Chadema mitandaoni. Kwanza nikuombe uwaambie viongozi wako wa CCM wasigeuze magereza zetu kama sehemu za kutesea watanzania wenzetu ambao ama wamekosa maadili huku uraiani ama wamesingiziwa. Ni jambo la aibu wewe kushabikia na kusema kwamba mahabusi/gerezani ni mahali pakutesea watu na sio mahali pakurekebishia maadili. Tunaomba haki za binaadamu walitolee jicho hili tatizo ambalo Hamy-D kwa kutojua anadhani ni sifa kusema mahabusu ni sehemu ya kutesea. La Pili na la msingi ni kwamba wewe na CCM yako kama mna roho nzuri na mnawatumikia watanzania ni muda wenu kumtoa Ludovick huku kwenye mateso gerezani kwa kumuwekea dhamani maana wewe Mwigulu a.k.a Hammy-D ulikuwa ukimtumia hela kwa njia ya mpesa. Mbona hukuwa kuwashauri Chadema wamtumie hela kwa mpesa wewe ndio ulikuwa mwema kwake kwa kumtumia. Acheni utoto na siasa za kipumbavu kwa kutunga kesi ambazo hamtaki kwenda kutoa ushahidi mahamani.
 
Bwashee kumbe una huruma!?

Simply wasiliana na Mwigulu Nchemba ataachiwa bila makaratasi yoyote yale ya dhamana. malipo ni hapahapa Duniani hizi ni sheria za karma.

Mkuu, unataka kusema muda wote huo bado tu hajajua kuwa kijana yuko mahabusu, tena amekongoroka vibaya! CHADEMA imuangalie jamani, kiubinadamu tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom