CHADEMA 'Lowassa siyo fisadi', CCM 'Lowassa ni fisadi'

Waziri Mkuu wa Uingereza aitwaye Harold Wilson aliwahi kusema, A week is a long time in politics.

Watanzania tumejaliwa kila kitu cha kidunia mpaka unafiki na usahaulifu!

Septemba 15, mwaka 2007, Dk. Slaa alisimama jukwaani na kutangaza orodha ya mafisadi 11 katika mkutano ulioitishwa na vyama vya upinzani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. Mojawapo katika majina hayo lilikuwepo jina la Edward Lowassa.

Baada ya kutangaza, WanaCCM wengi walipinga kwa nguvu zote wakidai huo ulikuwa ni udaku huku wakitaka vielelezo vya ufisadi kuonyesha ukweli wa kile CHADEMA walikuwa wanakisema.

Miaka minane baadaye, wale wale waliosimama kwenye majukwaa na kudai Lowassa ni fisadi, kwa sasa wameanza tena kupiga kelele kuaminisha Watanzania wakidai Lowassa siyo fisadi, wakati huo huo, CCM nao wamebadilika na kuanza kupiga kelele wakidai Lowassa ni fisadi. CHADEMA nao kwa sasa wanaomba vielelezo vya ufisadi wa Lowassa.

Watanzania wengine wanajiuliza, what's going on?

Wanaopiganiwa kwa sasa wako kimya huku nyasi zikiumia!

This is more than political flip-flop!

Waingereza wanasema, money talks and money alone sets the entire world in motion!

Ama kweli, a flag follows the direction of the wind!

Siasa za aina hii zitaendelea kulitafuna taifa wakati wachache wakifaidika kwa unafiki na ufisadi.

Nijuavyo mimi, sisa ni mchezo kama michezo mingine tunayoifahamu, na ina mbinu za kupata ushindi!. Kisiasa kutuhumu, ndo siasa! Kuthibitisha mara nyingi ni kazi ya mtuhumiwa! Ukikaaa kimya sina haja ya kueleza nani anapata hasara! Kwa kete kama ya EL, ambaye kisiasa anamvuto mkubwa, sishangai kutumiwa kuthibitisha tuhuma zilezile kivingine! Safari hii zamu iwe ya CCM kuthibitisha kuwa EL, ni fisadi ndo maana alikatwa Dodoma! Wakifanya hivyo, watathibitisha kuwa hata tuhuma za awali zilikuwa na mashiko ila kiburi tu cha Wanasiasa kulindana na hawakutaka kuumbuana! Kwa sababu hio, sioni vibaya!
 
Tanzania hakuna mpinzani wa kweli, mijitu imekuja na hoja dhaifu sana, kwa hakili zile tutaweza kubadilisha serikali kweli
 
Unaweza ukaona uzi wako uliobandikwa jana saa 2 usiku uko na michango mitatu tu!! Ni kielelezo kuwa watu wamekupotezea!!!

Si lazima awe amesafishwa, Lowass anaweza kuwa bado na ubaya wake ila ni chuki yake dhidi ya CCM ndio inatumiwa kama silaha. Ni kama vile uo vitani na unakamata silaha ya adui au unachukua mateka na kumhoji maswali ili akupe taarifa zitakazo saidia kushinda vita. Hili bado aliondoi uhalisia kwamba bado unapigana vita na adui yako ikiwa ni pamoja na mateka uliyenae!!!
 
Huajaelewa nini? Kosa kubwa zaidi kwa sasa ni kuwa ndani ya mfumo uliooza na wa kifisadi wa CCM. Lowasa kujitoa ndani ya mfumo huo wa aibu ni hatua muhimu kuelekea katika usafi; anastahili pongezi sana.

Maandiko yanasema Mbingu hulipuka kwa shangwe mwenye dhambi mmoja anapotubu. Kama Mbingu hufurahi kwa kondoo mmoja tu kuhama kutoka mfumo wa dhambi, je, sisi (binadamu) ni nani hadi tusifurahi pale mmoja wetu anapoondoka kwenye mfumo mchafu tena kwa faida ya taifa letu? Tafakari!
 
‬Niliwahi kusema Mwakyembe ni mnafiki sana na wala hana ushujaa wala uzalendo...


Alitumiwa kumchinja Mamvi...


Mamvi naye alidanganywa na bosi wake ajiuzulu na atapewa kijiti sijui baadae na kutetewa, aaah wapi...


Mwisho wa siku wa kina Nape na Makonda wakatumiwa kumchamba.


Hahahahahah
I love and hate politics at the same time...
 
Nimemsoma sana Robert Greene. Ameandika kitabu kinaitwa 33 STRATEGIES OF WAR. Law #2 inasema: LEARN HOW TO USE YOUR ENEMIES. Aya moja ya sura hiyo inasomeka hivi: "...Hire a former enemy and he will be more loyal than a friend, because he has more to prove..." Kwanini mwandishi huyo anasema hayo? Kwa sababu, anaeleza, "...you have more to fear from friends than from enemies. If you have no enemies, find a way to make them." Namwamwini sana mwandishi huyo kutokana na utafiti wa MASHIKO aalioufanya. Kwa hiyo naona, kwa kutambua au bila kutambua, CHADEMA wametumia RULES #2
 
‬...

I love and hate politics at the same time...

So you're neutral! This will enlighten you;

If you are neutral in situations of injustice, you have chosen the side of the oppressor. If an elephant has its foot on the tail of a mouse and you say that you are neutral, the mouse will not appreciate your neutrality.
by Desmon Tutu.
 
Nimemsoma sana Robert Greene. Ameandika kitabu kinaitwa 33 STRATEGIES OF WAR. Law #2 inasema: LEARN HOW TO USE YOUR ENEMIES. Aya moja ya sura hiyo inasomeka hivi: "...Hire a former enemy and he will be more loyal than a friend, because he has more to prove..." Kwanini mwandishi huyo anasema hayo? Kwa sababu, anaeleza, "...you have more to fear from friends than from enemies. If you have no enemies, find a way to make them." Namwamwini sana mwandishi huyo kutokana na utafiti wa MASHIKO aalioufanya. Kwa hiyo naona, kwa kutambua au bila kutambua, CHADEMA wametumia RULES #2

Dah! Chadema kweli wana vichwa! Hawa maadui waliwatengeneza wenyewe leo wanakuja wapole kama hua tayari kumkabili adui halisi. Mkuu hiyo post yako ilitakiwa uifungulie uzi unaojitegemea; darsa tosha wengine hatukuwahi kukutana na dhahabu kama hizi.

Hiki hapa, shule safi sana: https://omungameshack.files.wordpress.com/2013/06/the-33-strategies-of-war.pdf
 
Mtanzania msema kweli na makini ni yule aliye kufa.....sie tulio hai ni wanafiki, wajinga, miaka nane unaimba ufisadi leo unakuja na maneno njoo na ushaidi, jamaa sio fisadi mara hv mara vile ni ujinga tu kwa mtindo huu ccm wataendelea kutuongoza sababu ya ujinga kutoka vyama vya upinzani
 
Waacheni wapokee bomu jingne kw vl uwzo wao wakufkr ni duni kuanzia viongozi hadi wafuasi wao wa viroba vya zed na empire,wamesahau mamluki shibuda na zitto? Ccm ni tishio na mawazo yao ya max-weber.
 
Sina haja ya kueleza mabaya na uchafu wa Lowassa kwakuwa wakubwa wetu tayari wameisha "msafisha" kuwa tatizo sio Lowassa bali tatizo ni mfumo wa CCM
Kuazia sasa Lowassa ni jemedari shujaa na mzalendo wa kweli kwa taifa hili anayestahili kuwa rais wetu wa awamu ijayo

Kwa jicho la tatu ujio wa Lowassa unatupa picha gani kwenye vyama vyetu vya upinzani?

Ni dhahiri sasa kuwa wapinzani hawana watu makini wa kushawishi watanzania wawaamini kuwapa kura hadi wategemee mgombea mwenye nguvu na anayekubalika kutoka CCM ndio aje kuwakomboa
Kwa hilo wapinzani lazima wakiri kwamba wameshindwa kuwashawishi watanzania kuwaamini kwa kuwaimbia wimbo wa CCM mafisadi kisha wanarudi tena kawachukua hao mafisadi kuja upinzani ili kuwashawishi watz kuwapa kura kutokana na ushawishi wao hao mafisadi

Tunaaminishwa eti kama Lowassa atabadilika na atakubaliana na matakwa ya cdm na ukawa kwa ujumla basi wao hawana kinyongo wata mkaribisha
Lakini je hadi hivi sasa ni nani kati ya ukawa na Lowassa ameisha mbadilisha mwenzake?

Kwa wenye akili timamu watabaini Lowassa hivi sasa ni opportunist na mwanasiasa mkongwe na as for now yeye ndio anaendesha mchakato mzima kwa namna anavyotaka yeye kwa kuwabadilisha kabisa ukawa kwa ujumla wao waendane na maslahi yake zidi kisiasa

Inanipa sana ukakasi Lowassa kugeuka shujaa na mkombozi wa wapinzani lakini kinachoendelea hapa ni mchezo wa pata potea
Lowassa anauhitaji urais Ukawa wanahitaji kura na majimbo zaidi
Mwisho wa siku mnufaikaji mkubwa atakuwa CDM na Lowassa atabaki kama a biggest
loser


".....CCM kuongelea ubaya wa Lowassa kwa sasa ni sawa na mtu
kujichungulia nyeti zake...Chadema kuongelea uzuri wa Lowassa
kwa sasa ni sawa na mtu kujitekenya na kucheka mwenyewe....Vyo
te vinahitaji uso usio na soni"-Edo kumwembe.

Mzee siku hizi ni pesa tu
 
Moja ya sifa kubwa ya nchi za Scandinavia ni jinsi ambavyo wameweza kupambana na rushwa kupitia ngazi zote za maisha yao. Katika nchi hizi, rushwa inapambanwa katika ngazi ya jamii zaidi ya taasisi kama mahakama. Sote tunafahamu ni kwa kiasi gani mahakama ya jamii ilivyo na nguvu kuu kuliko taasisi za kimahakama zenyewe. Wala rushwa na watoa rushwa hawana ujiko wala nafasi ya kukwezwa mbele ya jamii. Kitendo hiki ndio njia pekee yenye ufanisi mkubwa kuweza kukabiliana na rushwa kwenye jamii changa kama Tanzania inayopitia ushamba wa materialism. Material life inapata heshima tu pale mhusika anapokua kajipatia hayo kwa njia ambayo zinakubalika na jamii husika.

Chadema na sasa UKAWA, walituonyesha njia hii ya kupambana na ufisadi kama walivyo wa Scandinavia. Mnano mwaka 2007, Dr. W. SLAA alianzisha mahakama hii ya kijamii pale Mwembeyanga. Huu ndio ulikua mwelekeo sahihi wa kupambana na ufisadi hapa nchini. Hakuna njia nyingine yoyote iliyofanisi ya kung'oa mizizi ya ufisadi isipokua mahakama za jamii. Inapofika hatua watu wanahoji gari umenunua kwa hela zipi? Na ndugu zako wa karibu wanagoma kupanda gari uliyonunua kwa njia za kutatanisha, ndipo wezi na mafisadi wanang'amua kukataliwa. Kukataliwa na watu unaowapenda ni hukumu kuu kuliko kufungwa miaka kadhaa Segerea.

Katika, "orodha ya fedheha," jina la ndugu Edward Lowassa lilitajwa kama fisadi mmojawapo. Kulingana na mazingira ya kimaisha nchini na changamoto zake, ndugu Edward Lowassa alizidi kupaa kwa umaarufu. Katika hatua za awali za vita hii, naweza kusema ilitegemewa kwa sababu jambo lolote zuri na la kudumu haliji kwa mbinu za zima moto. Chadema kama waanzilishi wa mahakama ya jamii, walipaswa kulitambua hili. Na kwa ujumla wake sikutegemea wafikiri kazi hii ilikua ya muda mfupi. Isitoshe, umaarufu wa Chadema ya leo unabebwa sana na dhana hii ya kupambana na ufisadi bila woga wala haya.

Kilichotokea juzi kwa Lowassa kujiunga na Chadema na kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho kinasikitisha na kuzorotesha mapambano dhidi ya ufisadi. Badala ya kuendeleza adhabu za kijamii, "kuwakataa mafisadi," leo Chadema imeibuka kidedea kuwasifu na kuhalalisha ufisadi. Hii ni kali kuliko.
 
Habari za asubuhi wanajf
Nina swali moja tu naomba mnisaidie,kwamba kwa muda mrefu sana chadema wamemchafua sana lowasa tena kwa kutumia gharama kubwa sana, leo wamempokea fisadi mkuu huyu na kumpa nafasi kubwa kabisa ktk chama chao.je sasa mnadhani itawagharimu tena kuzunguka nchi nzima na kumsafisha?
 

Attachments

  • 1438226307598.jpg
    1438226307598.jpg
    27.3 KB · Views: 216
Habari za asubuhi wanajf
Nina swali moja tu naomba mnisaidie,kwamba kwa muda mrefu sana chadema wamemchafua sana lowasa tena kwa kutumia gharama kubwa sana, leo wamempokea fisadi mkuu huyu na kumpa nafasi kubwa kabisa ktk chama chao.je sasa mnadhani itawagharimu tena kuzunguka nchi nzima na kumsafisha?
Itawagharimu kujisambaratisha baada ya kuonyesha kuwa hawana msimamo bali ni wachumiamatumbo. Hakuna hata mtu mmoja mwenye akili timamu atawakubali wajasariamali hawa wakiongozwa na FM
 
Back
Top Bottom