Elections 2010 CHADEMA kuzindua kampeni “Tanzania ya wananchi”

SHILLINGS

Senior Member
Oct 24, 2013
160
648
Kampeni hii itakayojulikana kwa jina la “TANZANIA YA WANANCHI” inalenga kuelimisha, kuhamasisha wananchi katika kutambua haki zao za msingi kwa kuzingatia misingi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambayo pamoja na mambo mengine inatambua: Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa na wananchi ndio msingi wa mamlaka yote.

Pamoja na mambo mengine kampeni hii inalenga vilevile kuvunja kile kinachoelezwa kwamba ni dhana potofu ya “Tanzania ya Magufuli” ambayo inalenga kupoka mamlaka ya umma wa Watanzania ambayo yapo kikatiba.

Mtonyaji anabainisha kwamba maandalizi yameanza na itagegemewa kuzinduliwa rasmi hizi karibuni.
 
Kweli hawa jamaa wameishiwa, yani wanaanzisha program ya kutuambia kuwa Tanzania yetu wananchi? Nani asiyejijua kama Tanzania ni yetu watanzania...
Tunajua nchi ni yetu sote ila kuna kundi la wapuuzi fulani wanataka kujimilikisha na kutuaminisha nchi ni yao

Usipokuwa upande wao, hupati ajira
Usipokuwa upande wao, huna haki ya kusikilizwa
Usipokuwa upande wao, huna thamani
Usipokuwa upande wao, ukitoa maoni unaitwa msaliti

Watu hao inabidi wakumbushwe kwamba Tanzania ni yetu sote wala si ya mtu wala si ya kikundi cha hao wahuni
 
Kwani kuna nchi isiyokuwa ya Wananchi?

Hizi ni dalili za kuishiwa sasa!
Pole pole mkuu ruzuku italiwaje na viongozi wa makao makuu.Lazima wabuni vitu Kama hivyo wapate sababu ya kula ruzuku.Hiyo ni project ya chadema makao makuu kunywa Panadol ya pesa za ruzuku kumeza kavukavu bila hata tone la Maji la kuisindikizia tumboni
 
Safi sana.. tupo tayari kueneza habari hii hata wakizuia mikutano
Kampeni hii itakayojulikana kwa jina la “TANZANIA YA WANANCHI” inalenga kuelimisha, kuhamasisha wananchi katika kutambua haki zao za msingi kwa kuzingatia misingi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambayo pamoja na mambo mengine inatambua: Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa na wananchi ndio msingi wa mamlaka yote.

Pamoja na mambo mengine kampeni hii inalenga vilevile kuvunja kile kinachoelezwa kwamba ni dhana potofu ya “Tanzania ya Magufuli” ambayo inalenga kupoka mamlaka ya umma wa Watanzania ambayo yapo kikatiba.

Mtonyaji anabainisha kwamba maandalizi yameanza na itagegemewa kuzinduliwa rasmi hizi karibuni.
 
huwa sina lugha za kuudhi iia sasa unaonyeza upuuzi wako. Unajisikiaje kuandika utoto muda wote? Kuna wakati mambo yanayojadiliwa ni muhimu sana alafu unaingiza utoto.
 
Back
Top Bottom