Viongozi wa Chadema wilayani Morogoro Mjini, wamelazimika kukimbia ofisi zao baada ya kuvamiwa na kundi la Wanachadema kuwashinikiza kuondoka madarakani kwa madai ya kutumiwa na CCM kukihujumu chama.
Katika sakata hilo lililotokea juzi saa 9.00 alasiri viongozi kutoka kata 19 wakiwa na msafara wa pikipiki walifika ofisini hapo na kutaka kufanyike mabadiliko ya uongozi wakidai walioko madarakani wameshindwa.
Tukio hilo lilisababisha viongozi kadhaa wakiwamo Mwenyekiti wa Wilaya na Katibu Mwenezi wa Wilaya kufunga ofisi hizo na kutimka kitendo kilichosababisha kuzomewa.
Mwenyekiti wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Charles Mbasa, akizungumza kwa niaba ya wenzake alisema hawana imani na viongozi hao na kuwatuhumu kuwa wanatumiwa na CCM kuidhoofisha Chadema .
Alidai walimuandikia waraka Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willbroad Slaa, kumueleza kuwa viongozi hao wa wilaya wamekuwa wakiomba pesa mara kadhaa kutoka kwa kigogo mmoja wa CCM (jina tunalo) kwa ajili ya matumizi na maslahi binafsi. Madai mengine ni pamoja na kukwamisha mikutano ya hadhara inayoandaliwa na viongozi wa kata, kuwazuia wanachama na wanaharakati kujenga chama ndani ya jimbo la uchaguzi la Morogoro Mjini.
Mengine ni kutowasilisha ripoti ya mapato na matumizi ya wilaya , kutoandaa ripoti za matumizi ya michango ya harambee pia kuwatisha viongozi na wanaharakati wanapofanya kazi za kujenga chama.
Mjumbe wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) Wilaya ya Morogoro, Monica Mushi, akiongea kwa niaba ya baraza alisema wanaunga mkono viongozi hao kuondolewa madarakani kwa kuwa ni wasaliti.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema kata ya Mazimbu, Maximilium Livingstone , alimtaka Dk. Slaa, kufanya mabadiliko ya haraka ili kuondoa uongozi huo pamoja na mabaraza ya ndani ya chama hicho.
SOURCE: NIPASHE