CHADEMA kuwasha moto nchi nzima

CHADEMA kuwasha moto nchi nzima

Uchaguzi unaotambulika duniani ni ule wa octoba 25 , ule mwingine uliohusisha AK - 47 na Manowari za kivita hautambuliki .
Uchaguzi ushapita kama mmesusa sawa, hakuna liloharibika ni mpaka 2020!!!!!! nchi lazima ikabidhiwe kwa the right political party. Serikali ya SUK haikujali minority yaani haikuwa ya haki sawa kwa wote kama mnavyoimba, lakini ya sasa imefanya mazuri,
 
Unaogopa nini wakati miezi 6 imeisha kukiwa hakuna lolote ?
Miezi 6 ni muda mfupi sana. Mpk sasa JPM anajenga nidhamu serikalini. Bajeti yake ya kwanza ikishapitishwa. Ndipo tuanze kuangalia wapi wanakosea.
Pili, ndani ya chadema kuna nyufa nyingi sana zilizosababishwa na mgawanyo wa majimbo kwa vyama vya ukawa. Ikumbukwe kuwa mgawanyo huu umekuja baada ya wanachadema kumaliza mchakato wa kura za maoni. Mgawanyo ulipata upinzani sana sehemu nyingi sana.
Lakini pia kuondoka kwa dokta Slaa ni chanzo kingine cha nyufa ndani ya chadema. Kuondoka tu siyo tatizo. Tatizo ni NAMNA alivyoondoka. Wengi wa wanachadema wana fikra tofauti juu ya hili.
Ningependa kuona chadema inapanga kujenga mshikamano na umoja ndani ya chama kwa sasa kabla ya kwenda kwa wananchi.
 
Subiri moto uwashwe kudadeki ! Hapo ndio utaitambua chadema ni nini ?
Mioto mingapi imewashwa na hakuna lolote,ndio kwanza mnachukua mafisadi
Tumechoka na siasa za matukio,pangeni jambo lingine ili mtoke
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) , Kinatarajia kuanza mikutano ya hadhara na ya ndani nchi nzima ili kujenga na kuinua uhai wake kuanzia juni mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Mh Daktari Vicent Mashinji alipoongea na waandishi wa habari jiji Dar es salaam.

Chanzo - Mwananchi .

WITO - ni vema CHADEMA ikatumia mikutano hiyo Kuanika ukweli wote kuhusiana na sakata la sukari , Ajenda ya KATIBA YA WARIOBA na TUME HURU YA UCHAGUZI vishikiwe bango .

Mungu ibariki CHADEMA , Mungu ibariki UKAWA .
Hivi Lowassa anahudhuria vikao vya kamati kuu au halmashauri kuu ya Chadema kama nani? Au ni mmiliki wa chama?
 
mimi bado na shida na siasa ya vyama vyetu bila kujali ni chama gani ni kama chadema kupeleka mamia ya mamilion kwenye uchaguzi wa marudio wa CHALINZE ccm kupeleka mamilioni kwenye uchaguzi wa marudio wa ARUMERU way back .kuna vyama hawana hata makao makuu ya office wamepanga unaenda kutumia milion mia kadhaa sehemu ambayo unajua haushindi ?

Ni jambo nalifuatilia sana sipati sioni mantiki ya wanasiasa kusema wanajali raia
 
Wafanye tu ili tujue uwezo wa Mashinji kuunganisha chama.
Hivi Salim Mwalimu na Mnyika wapo? Au wamemsusia Mashinji
 
mimi bado na shida na siasa ya vyama vyetu bila kujali ni chama gani ni kama chadema kupeleka mamia ya mamilion kwenye uchaguzi wa marudio wa CHALINZE ccm kupeleka mamilioni kwenye uchaguzi wa marudio wa ARUMERU way back .kuna vyama hawana hata makao makuu ya office wamepanga unaenda kutumia milion mia kadhaa sehemu ambayo unajua haushindi ?

Ni jambo nalifuatilia sana sipati sioni mantiki ya wanasiasa kusema wanajali raia
Chama cha siasa ni mabarabarani na majukwaani - Jk Nyerere .
 
To be Honest...CHADEMA ishatuchosha

To be honest, ingekuwa vyema sana ungeeleza ni kwa namna gani "CHADEMA inawachosha!"...

Sasa wewe unasema inawachosha tu bila kueleza kwa namna gani, hueleweki mkubwa!!

Sema inawachosha kwa kuleta uhaba wa sukari au inawachosha kwa kuhangaika ku - dizaini propaganda tofauti tofauti kila uchao dhidi yao bila mafanikio.... au nini hasa......sasa mmechoka?

Please, funguka mkubwa.... acha kubania bania bhana.....!!
 
Ikumbukwe kwamba chai ndio kinywaji namba 2 ambacho masikini anaweza kukimudu , kupiga marufuku sukari kutoka nje wakati hatuna sukari ya kutosha ni kulazimisha umaarufu wa bure .
Ndio agenda yenu hiyo? Pole sana. Hivi unajua mtu anapopendwa?! Unajua wananchi wanajua kabisa wanajua nia nzuri ya Rais na nia chafu ya wafanya biashara. Sasa badala ya kuwalaumu wafanyabiashara mnataka eti kusambaza sumu kuwa serekali ndio imesababisha. Watanzania wa leo sio wa jana ndio manana wabunge wanawake huko wanahangaikai suala la baby!!!! Can you imagine. What type of wabunge we have jamani .Siku nzima wanapoteza muda na kodi zetu kwa suala la kitotoeti la baby. My Goid they are not serious! Kuna issue kubwa sana za kina mama. wanawake wangapi wanafariki kwa uzazi eti wanawake wanatoka bungeni kisa baby. Hopeless kabisa. na katiba ijayao tunataka ipige marufuku Wabunge wa kuteuliwa wanawake! Or else kuwe na interview watu waende kwa vigezo na sio ki-baby.Kodi zetu zinapotea tu bure!Enough is enough!
 
mwana msipoteze umma mi nachukia sana mtu anapoongea jambo halijui kwa comfidence alisema mh rais vibali atakua anatoa yeye tafuta hotuba ya upinzani last yr ya viwanda na biashara mlilalamika sukari vibali vinatolewa hovyo mpaka sukari ya viwandani inauzwa masupermarkets tatizo la kufuata matukio unashindwa kujua base ya jambo linapozuka unazuka nalo
 
Chadema, Chadema, Chadema. What a mess! Watanzania tunataka kufanya kazi na si kuwasikiliza nyie. Kumbukeni mliyoyasema Nzega wakati wa kampeni kuhusiana na MCC na nini mliasema hivi majuzi MCC walivyoondoa kimsaada chao! Wasio na uwezo wa kufikiria ndiyo wanaowakubali ila mimi NO.
 
Back
Top Bottom