PreGE2025 CHADEMA kuomba mapitio ya uamuzi wa Jaji Mwanga

PreGE2025 CHADEMA kuomba mapitio ya uamuzi wa Jaji Mwanga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
248
Reaction score
969

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakijaridhishwa na uamuzi uliotolewa na Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu wa kusitisha shughuli za chama hicho, kikisema kitaomba mapitio ya shauri hilo, huku pia kikiomba jaji huyo ajitoe kwani hawana imani naye.

Katika uamuzi huo uliotolewa Juni 10, 2025, Jaji Mwanga amewazuia Katibu Mkuu wa chama na Bodi ya wadhamini kutofanya shughuli za kisiasa hadi uamuzi wa mahakama utakapotolewa kwenye shauri hili.

Pia watumishi wa chama na wote waliotajwa kwenye amri ya pili ya kesi hiyo wamezuiwa kutumia rasilimali za chama hadi uamuzi wa mahakama utakapotolewa kwenye shauri hili.

Kesi hiyo imefunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Zanzibar), Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili, wakilalamika kutokuwepo kwa mgawanyo sahihi wa rasilimali za chama hicho, huku wakiomba chama hicho kisitishwe kufanya kazi hadi kesi hiyo itakapoamuliwa.

Akizungumza leo Juni 17, 2025 Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche amesema kesi hiyo ina msukumo nyuma yake wa watu wenye nia ovu.

Soma taarifa nzima: CHADEMA kuomba mapitio uamuzi wa Jaji Mwanga
 
Bahati mbaya sana mahakama zetu zimejaa machawa ya bibi titi
 
Back
Top Bottom