CHADEMA: Kuna wengine watamfuata Dkt. Mashinji

Mashinji mgombea wake sumaye na mbowe mgombea wake lowasa akafanya abadili via angani

My take
Mgombea wa mashinji Mzee sumaye karudi ccm na mashinji nae karudi ccm
Mgombea wa Mbowe Mzee lowasa karudi ccm tutegemee mbowe nae kurudi ccm ? Muda utaamua.
 
Sawa Sawa Acha Tuone.
Kauli Za Waoondoka Baadhi Yao Hawajielewi
Unasema Siasa Sasa Basi, Mara Sitaki Kuwa Na Chama Mara Oops
Nilikaa Bila Chama Siwatendei Haki Watanzania
Nashangaaa sana kuona eti watu kama aina ya Mbowe anadai Demokrasia wakati kwake atakayempinga anapewa sifa ya kuitwa Msaliti, Masalia n.k.
Na Wabishi tumeshuhudia yaliyowakuta akina Chacha,
Zitto Kabwe amedai Democracy wakati Madiwani wa Act Wazalendo kigoma walijaribu Democracy ya kutokuwa na imani na Meya, what was happen aliwapiga biti na aliwaeleza watakao kisaliti chama Waganga wake watawashughulikia. Na aliwaamuru waandike barua kwenda kwa Mkurugenzi ili wazikatae saini zao, kwa hofu ya kulogwa walifanya hivyo. Sasa hizo Democracy za ramli zitatuvusha. So Democracy ninayoiona ni ile ya kutukanana na kuharibiana heshima.
Tujitafakali kwanza kabla kukubali kugeuzwa zuzu.
 
Kwahiyo mlimunyima ukatibu mkuu kisa alitikisa kiti cha mbowe?

Maana kwa maelezo ya makene ni kwamba mashinji alitaman mwambe ndo awe mwenyekiti hivyo ndo maana wakamnyima ukatibu mkuu

Ni kweli ukigusa uenyekiti taifa chadema umekwisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHADEMA asilia watabaki lakini mamluki kama akina mashinji lazima watawafuata. CCM inapanda mbegu mbaya sana shimo hili wanalochimba watatumbukia wenyewe mark my word

Yaani chadema hawajiekewi, yaani mtu anateuliwa kuwa katibu mkuu wa chama kumbe mamluki.

Shame upon this chama.

Wajipange sana.

How comes kila anayeondoka ni mamluki
 
Mashinji Na Mwambe Wanakesi Mahakama Ya Songea,hakimu Alisisitiza Ikiwa Hawataonekana Atatoa Hukumu Wasidharau Mahakama,sa Sijuwi Hapo Baada Ya Kuunga Mkono Juhudi
 
Kombo Chini -TAPA, Team gani anayotengeneza mbowe? Kuna mtu alitengeneza timu isiyo na mashaka chadema kama dr silaa. ? Aliwatengenezea imani katika chama na sio mtu ndio maana alipoondoka pamoja na kukubalika na kuamini walichoamini wote kwa miaka kumi bado watu walibaki CHADEMA.

Leo mbowe anatengeneza timu inayomsujudia yeye. Jiulize leo ester bulaya anakuwaje chief whip wakati kuna yule mama mbunge wa mlinga bi suzan kiwanga ambaye amewekwa ndani kila mara?

Ndani ya chadema mbowe amejitengenezea base kiasi ambacho ukiwa tofauti haudumu. Angalia hata Mrema anasema Mashinji alikuwa na timu yake ya mwenyekiti ambaye ni cecil mwambe, sasa kwani lazima wote wamuunge mkono mbowe? Yaani ameshaathirika na siasa za mbowenism.Halafu wakitoka nje wanalilia demokrasia.

Anaenda mbali zaidi anasema ataondoka na watu, kwa hiyo chadema ya sasa sio ile ya chama aliyoacha dr silaa. Hii ni ya mtu. Akitoka anaondoka na watu wake.

Kazi ipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa wote ni washirika wa karibu sana wa Sumaye, Mwambe na Mashinji isipo Selasini, Mbunge wa Rombo, kila mmoja anafahamu lengo la hii team na mikakati yao ya kushika nyadhifa za juu CHADEMA. Hata sauti zao zilivuja lakini harakati zao hizo ziligonga mwamba na hatimayee wameanza kujitoa chamani, alianza Sumaye, akaja Mwambe na sasa Mashinji. Je, Kubenea na Komu nao tutarajie siku chache zijao kuondoka Chadema na kwenda CCM? Just a matter of time!

Mbunge Selasini naye baada ya kushindwa uchaguzi kanda ya kaskazini alianza kulalamika kuchezewa rafu kwenye uchaguzi kama haitoshi akaanza kumtusi Mbowe na kujivua nafasi yake ya Mnadhimu bungeni, ni wazi mzee huyu kwa sasa hayuko na furaha ndani ya CHADEMA na hawaivi na bwana Mwenyekiti. Je, tutarajie na yeye kuondoka chamani?

Ni swala la muda tu kila kitu kitu kitakua wazi.
 
Siku kadhaa zimepita tangu nilipokutana na Prof. Abdallah Safari maeneo ya Posta Dar es salaam ambaye pamoja na kusema anahama Chadema wakati wowote alimtupia lawama Mhe. Mbowe na kikundi chake cha kina Sugu, Msigwa, Mdee, Lema na wengineo kuwa wanakiharibu chama. (Nisiingie kwa undani kuhusu hilo maana sio lengo la thread hii) lakini Prof akatoa 'compliment' kwa ndugu Kigaila kwa kusema kwa kimombo...'he is excellent'!

Wakati mwingine nilikuwa Dodoma kikazi ikawa kama coincidence nilikutana na Cecil Mwambe ambaye na yeye pamoja na mameno yake kufanana na ya Prof lakini alisema Kigaila ndio mtu pekee ambaye angeweza kukiunganisha Chama na kwamba ni mtu asiyefisadika!

Baadhi ya wajumbe wa Kamati kuu kwa nyakati tofauti walionekana 'kumpenda' Kigaila.

Kigaila ana nini? Kwa nini wote wanaoondoka Chadema na wenye mpango wa kuondoka Chadema wanasema wasingeondoka kama Kigaila angekuwa Mwwnyekiti Chadema?

Huyu Kigaila hapendagi ujinga ujinga sijui ni mchaga wa wapi huyu au ni mgogo?!
 
Kwa katibu mkuu yeyote wa chama chchte akiondoka athari haikoseni, kukubali ukweli si udhaifu
 
Back
Top Bottom