CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi

CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi

Kwa jinsi ninavyoona hata Kampeni zenyewe,ninaona hali ni ile ile,Magufuli kama ameshindwa kukemea MATUSI na KUDHALILISHA watu wengine sidhani kama anuweza wa kumkamata mtu yeyote na kumfungulia kesi.

Huyu ameenda Bariadi amempigia promo Chenge,amempigia promo Tiba kwa ufupi maana hawa ni wasafi sana kuliko yule anayedhalilishwa kwenye majukwaa yake.

Angeweza hata kwa kidogo kukemea ujinga labda ningemfikiria.Amechaguliwa na wenye pesa zao sababu wanajua weakness zake.

Kwangu bado sijapata RAIS wa kumpa kura mpaka sasa.Ila Mbunge wangu ninaye siku nyingi hana haja ya kuifuata kura yangu nitampelekea tu.

Ila mwisho MABADILIKO ndani ya CCM ni ndoto mpaka watambue maovu na makosa yao ya msingi kabisa.Kwa sasa bado sana,ila kuna siku inakuja watajua.
Kamanda naona kama haujui chochote kinachoendelea katika ulimwengu wa siasa za nchi hii....WENYE pesa zao wako na Mzee wa Nywele nyeupe, wanasema ULIPO TUPO....Magufuli kapigiwa kura na wanyonge wa CCM na atapigiwa kura na wanyonge wa nchi hii ambao ndio wenye nchi...
 
unadhani watuakua na kauli ya kusema ikiwa wamemkaribisha adui yao mkuu? hawana jipya tena ndo maana wamekaa kimya
 
Hakuna mahali ambapo nimeainisha kama Dr.Slaa ni adui wa CDM,pili tulikaririshwa kwamba viongozi wazuri ni lazima watoke CCM.Lakini hii ilikuwa ile CCM yenye UZALENDO wa hali ya juu.

Magufuli alimpigia Promo Chenge na Tibaijuka.Na wale wabunge ambao leo wanatoa pesa ili kupata ubunge kesho watatoa pesa ili kupata uwaziri,unarudi na kusema RUSHWA na UFISADI utaisha ndani ya CCM ni ndoto mtu aotayo MCHANA.

Kwa trend iliyopo hakuna Kiongozi atakayetoka CCM akaweza kuipiga vita RUSHWA,ingewezekana hilo kufanyika kama CCM kwenye mchujo wangewatoa wote waliotoa RUSHWA ili kupata kugombea UBUNGE.

Ingewezekana tu kama ingewatoa wote wabadhirifu wa mali za umma,wala rushwa,mafisadi ambao hadi leo wako ndani ya CCM.

Kama nasema kama CCM ingewaondoa wote kabisa wote walioingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kwa rushwa ndogo au kubwa hii ni pamoja na Mtoto wa Mkulu,Nape Nauye kwenye ubunge hakika Mwanz ungenishawishi kuipigia kura CCM

Hii ni pamoja na Magufuli mwenyewe asingekuwepo kwenye kinyang'anyiro maana ameshindwa kuongoza wizara iliyokithiri kwa rushwa,ubadhirfu,wizi ,ufisadi nk nk leo atawezeje kutuaminisha kwamba ataweza kuondo RUSHWA kwenye TAIFA lenye wizara zaidi ya 30,hakika naweza kuwa sina PHD lakini hii haihitaji PHD kuona kwamba hata huyu hawezi..

Tuliaminishwa Mkapa ni Mr Clean alipokuwa akipigiwa debe na JKN mwisho wa siku ametoka akiwa MCHAFU kuliko choo cha wanafunzi kilichojaa.

Tukaaminishwa tena kwamba huyu anayetoka madarakani ni muadilifu,Mzalendo nk nk lakini leo UCHAFU wote unamuelea,wizi wa mali za umma ESCROW,Uuzaji na umikaji wa UDA kwa familia ya Mkullu,hii yote inaletea ukakasi.

Ni bora safari hii tuwape wapinzani,tena kwa kura za kishindo kabisa,hatuhitaji vita ya walionacho na wasio nacho,nawassa watanzania wenzangu,wakati ndiyo sasa TUBADILIKE,CCM imetosha,kama kula wacha na UPINZANI ule.

Kama tulikuwa tunaishi msalani hivi sasa tumepata option nyingine ya kwenda kuishi kwenye jalala, ambalo lenyewe limepokea baadhi ya vitu kutoka huko chooni, kwa hiyo jalala limekuwa zaidi ya choo. Huko upinzani siajona wa kumchagua mimi.
 
Ndugu yangu hakuna mahali nimekwambia huna elimu.Nimesema kutokana na sentensi yako watanzania tunauhitaji wa kupewa elimu ya uraia.

Pili hapo ndipo ile idea yangu inapopata mashiko baada ya kuisoma na kuitafakari hoja yako hii.Tunahitaji kujua kazi za WABUNGE ni zipi na kazi na wajibu wao na zipi ni kazi za SERIKALI na wajibu wake.

Kwenda shule kwa mtu siyo kigezo cha kujua kila kitu.Ukiwa unamjibu mtu hoja yake itafakari kwanini amesema aliyoyasema

Kukariri ni kubaya sana, hivyo ilivyo sivyo ilivyo. Kwa bunge tulilokuwa nalo awamu ya nne, kama ingekuwa ni hivyo unavyozungumzia wewe basi mafisadi wangeisha, lakini hao wabunge ndio wanaoshiriki kutuumiza, wakiwa bungeni wanatuitetea lakini wakitoka basi hawana la kutufanyia zaidi ya kutuumiza. Wabunge wa upinzani walifanya kazi kubwa ya kufichua mafisadi lakini leo hii wanawaficha hao mafisadi, hiki ni nini sasa. Ndio majukumu ya mbunge, ndiyo elimu ya uraia tunayopaswa tujifunze?
 
Kamanda naona kama haujui chochote kinachoendelea katika ulimwengu wa siasa za nchi hii....WENYE pesa zao wako na Mzee wa Nywele nyeupe, wanasema ULIPO TUPO....Magufuli kapigiwa kura na wanyonge wa CCM na atapigiwa kura na wanyonge wa nchi hii ambao ndio wenye nchi...

Magufuli siyo kiongozi bora sababu ya kutoa maneno ya karaha pale anapokuwa Challenged.Pili wala si kiongozi wa wanyonge bali wa wenye pesa zao akina JK & Coy.

Na mwisho kama aliuza Nyumba za serikali kwa bei poa,akanunua meli ya mwaka 1970 kwa bei kubwa zaidi hata ya Meli mpya.Kama ameshindwa kuzuia RUSHWA kwenye wizara yake atawezeje kuzuia RUSHWA kwa WIZARA 30.

Mwisho kama wabung wa CCM kwa asilimi 99 wamehonga kupita kwenye kura ya maoni na kwa sasa wako busy kutafuta kura kwa kumwaga pesa kama vichaa,tunategemea kati yao wabunge 66 atawateua kuwa mawaziri/naibu mawaziri hivi ataweza kuwaambia wasichukue RUSHWA kubwa,kuendeleza ufisadi???

Naweza nikawa shule yangu ndogo lakini ninauelewa mpana zaidi.Hakika Magufuli hatufai hata kwa pesa.
 
Kama tulikuwa tunaishi msalani hivi sasa tumepata option nyingine ya kwenda kuishi kwenye jalala, ambalo lenyewe limepokea baadhi ya vitu kutoka huko chooni, kwa hiyo jalala limekuwa zaidi ya choo. Huko upinzani siajona wa kumchagua mimi.

Siwezi kukukatalia,ila huko Msalani uliko yuko unayeweza kumchagua.Maana kama Mchafu mmoja katoka kaacha wachafu 100 huko msalani basi,ninategemea huko msalani unauwezo wa kuchagua,kuna akina Chenge,Tibaijuka,Nyalandu,Wauza Unga nk nk.Hope huko wako wa kuwachagua.
 
Kukariri ni kubaya sana, hivyo ilivyo sivyo ilivyo. Kwa bunge tulilokuwa nalo awamu ya nne, kama ingekuwa ni hivyo unavyozungumzia wewe basi mafisadi wangeisha, lakini hao wabunge ndio wanaoshiriki kutuumiza, wakiwa bungeni wanatuitetea lakini wakitoka basi hawana la kutufanyia zaidi ya kutuumiza. Wabunge wa upinzani walifanya kazi kubwa ya kufichua mafisadi lakini leo hii wanawaficha hao mafisadi, hiki ni nini sasa. Ndio majukumu ya mbunge, ndiyo elimu ya uraia tunayopaswa tujifunze?

Wamewaficha wapi???Sijaona mahali ambapo umeongea point ikaeleweka.Hakuna mahali ambapo Mbunge wa CCM amekemea ujinga wa ndiyoooo kwenye masuala ya KITAIFA.

Kwa sisi wa kristu bado tunaamini hata mdhambi anaweza kufika mbinguni kama akitubu.Hata huyo mnayedhani ni msafi hana usafi hata chembe.
 
Siwezi kukukatalia,ila huko Msalani uliko yuko unayeweza kumchagua.Maana kama Mchafu mmoja katoka kaacha wachafu 100 huko msalani basi,ninategemea huko msalani unauwezo wa kuchagua,kuna akina Chenge,Tibaijuka,Nyalandu,Wauza Unga nk nk.Hope huko wako wa kuwachagua.

Mimi sijui, ila unapoenda machinjioni ukakuta wengine wanachinja na wengine wapo tu pembeni wanawatizama wenzao, si kwamba waliokaa wakiwatizama wenzao hawajui kuchinja, ni kwamba wamekosa visu na wa kuwachinja, sasa ukitaka kuwajua wanachinjaje, wape kisu.
 
Magufuli siyo kiongozi bora sababu ya kutoa maneno ya karaha pale anapokuwa Challenged.Pili wala si kiongozi wa wanyonge bali wa wenye pesa zao akina JK & Coy.

Na mwisho kama aliuza Nyumba za serikali kwa bei poa,akanunua meli ya mwaka 1970 kwa bei kubwa zaidi hata ya Meli mpya.Kama ameshindwa kuzuia RUSHWA kwenye wizara yake atawezeje kuzuia RUSHWA kwa WIZARA 30.

Mwisho kama wabung wa CCM kwa asilimi 99 wamehonga kupita kwenye kura ya maoni na kwa sasa wako busy kutafuta kura kwa kumwaga pesa kama vichaa,tunategemea kati yao wabunge 66 atawateua kuwa mawaziri/naibu mawaziri hivi ataweza kuwaambia wasichukue RUSHWA kubwa,kuendeleza ufisadi???

Naweza nikawa shule yangu ndogo lakini ninauelewa mpana zaidi.Hakika Magufuli hatufai hata kwa pesa.

Chagua magufuli mwadilifu,,mchapakaz,,mzalendo,,mfwatiliaji
 
Wamewaficha wapi???Sijaona mahali ambapo umeongea point ikaeleweka.Hakuna mahali ambapo Mbunge wa CCM amekemea ujinga wa ndiyoooo kwenye masuala ya KITAIFA.

Kwa sisi wa kristu bado tunaamini hata mdhambi anaweza kufika mbinguni kama akitubu.Hata huyo mnayedhani ni msafi hana usafi hata chembe.

Naona unaichukia sana CCM, kama hujaona point, ni hivi, mimi kinachoniuma, wale wabunge na viongozi wa upinzani tuliowategemea kuwa ndio watakaotuokoa na mafisadi na rushwa leo hii wanawakumbatia mafisadi, nashindwa kuelewa.

Unafikiri wataanzanje kukemea mafisadi tena, bunge lijalo ilhal wameukumbatia ----- waliosema unawasha. Tena muda huo wameshashindwa uchaguzi mkuu, itakuwa ni aibu na anguko kubwa kwetu na kwao
 
Mimi sijui, ila unapoenda machinjioni ukakuta wengine wanachinja na wengine wapo tu pembeni wanawatizama wenzao, si kwamba waliokaa wakiwatizama wenzao hawajui kuchinja, ni kwamba wamekosa visu na wa kuwachinja, sasa ukitaka kuwajua wanachinjaje, wape kisu.

Wanasema Mjinga akierevuka mwerevu yu Mashakani.Pole.
 
Chagua magufuli mwadilifu,,mchapakaz,,mzalendo,,mfwatiliaji

Kama UADILIFU unaenda na hii sawa basi mimi nitaitwa MTAKATIFU:

1.UUzaji wa nyumba za serikali kwa bei poa.

2.Kuhakikisha nduguze na vidosho vyake vinapewa/kumilikishwa nyumba za serikali

3.Upotevu wa Bilioni 262 kwa kulipa wakandarasi hewa.

4.Ununuzi wa meli ya mwaka 1970 kwa bei ya kununulia kivuko kipya.(bilioni 8 wakati Azam kanunua brand new kwa bilioni 6)

5.Kutukana watu mfano mzuri kuwaambia watu wakigamboni wapige mbizi wakikosa sh.200 na kuwaambia watu wa Biharamulo waliolalamikia barabara kukwepesha kupelekwa Chato badala ya Wilaya,na kuwaambia wakapakaze vinyesi vya o ili viwe lami.

Huyu ndiyo kiongozi tunayeambiwa ni BORA....
 
Naona unaichukia sana CCM, kama hujaona point, ni hivi, mimi kinachoniuma, wale wabunge na viongozi wa upinzani tuliowategemea kuwa ndio watakaotuokoa na mafisadi na rushwa leo hii wanawakumbatia mafisadi, nashindwa kuelewa.

Unafikiri wataanzanje kukemea mafisadi tena, bunge lijalo ilhal wameukumbatia ----- waliosema unawasha. Tena muda huo wameshashindwa uchaguzi mkuu, itakuwa ni aibu na anguko kubwa kwetu na kwao

Siichukii CCM hata kidogo ninawachukia viongozi wanafiki ,wezi wanaotumia ujinga wa watanzania kuiba na kutulazimisha tuendelee kuiamini.

Ninawachukia viongozi wanaojidai wanapiga vita rushwa wakati wao ndiyo vinara wa rushwa,madawa ya kulevya,ufisadi nk nk.

Ninachukia viongozi ambao wanajidai wanapiga vita rushwa wakati ndiyo watoaji wakubwa wa rushwa wakati wa kutafuta uongozi.

Kamwe siichukii CCM,ila ile CCM iliyokuwa na wazalendo ilishaondoka na mwenye kuiasisi.Waliobaki ni wapigaji tu,ndiyo maana hata kwenye uteuzi wa nafasi za viti maalumu waliopita ni watoto wa viongozi waandamizi walio ndani ya CCM.

Ninawachukia viongozi wa CCM amabao wanajifanya kupiga vita UKANDA na UKABILA wakati wakipanda majukwaani kila siku ni kuwabagua watu wa ukanda wa kaskazini.Haifurahishi wala haipendezi.

Hivyo ndugu siichukii CCM nawachukia waliotuweka tulipo.Wameuza viwanda vyote,wakitegemea wachina na wazungu watuletee maendeleo,wanuza madini na maliasili zetu kwa kupewa vyandarua na pesa kidogo toka mataifa mbali mbali.

Sijawahi kusema Lowassa Msafi,lakini ndani ya CCM leo wasafi ni wangapi???Kama ni wapo ni wale wa enzi ya Mwalimu wengine wote ni wezi,mafisadi na wala rushwa,hawa ni pamoja na mgombea urais wa CCM.
 
Kwa maana hiyo kiongozi unayemtaka wewe hayupo, sahau.
 
Wamewaficha wapi???Sijaona mahali ambapo umeongea point ikaeleweka.Hakuna mahali ambapo Mbunge wa CCM amekemea ujinga wa ndiyoooo kwenye masuala ya KITAIFA.

Kwa sisi wa kristu bado tunaamini hata mdhambi anaweza kufika mbinguni kama akitubu.Hata huyo mnayedhani ni msafi hana usafi hata chembe.

Tutachagua ccm kwakuwa ubora wao bado unazidi udhihirika kadri siku zinavy
osonga daima 2015 ni mwaka wa kwenda na Magufuli tuu.... #HapaKaziTu
 
Back
Top Bottom