CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi


umeona mbali saana, wakiwa haweajui nini wanataka bado
 
 
Ni suala la uwezo wa ufikiri na kuamua...ndugu yangu unaonekana uko vizuri na uko sahihi kabisa kutokuhitaji USHAURI ili uendelee kubaki kama ulivyo.
Ulishaondoka Chadema siku nyingi, sijui huko uliko hivi sasa wamekupa cheo gani. Lakini kuna msemo wa Wasukuma, ya Ngoshwe mwachie Ngoshwe. Mambo ya kuangalia angalia nyuma utageuka kuwa jiwe. Ni ushauri tu.
 

Sawa, nimekuelewa, ni nani kama SI Magufuli, atakayeweza kupambana na UFISADI, RUSHWA na UBADHILLIFU.
 

Hayo ni maoni yako, na hao wanaosema mkichagua CCM au UKAWA, ni maoni yao, kila mtu ana imani na sababu au hoja zinazomfanya aendelee lkuwa muumini au mshabiki wa chama fulani, hivyo basi, na mimi sitaweza kuruhusu chama cha watu wanafiki ambao walituaminisha ufisadi wa baadhi ya viongozi, halafu leo waniambie eti wale watu wamekuwa ni wasafi na wana maendeleo (mabadiliko), ni heri nibaki na maendeleo yangu ya mwendo wa kinyonga, nimeridhika na maendeleo yaliyopo ndani ya serikali kupitia chama cha mapinduzi, japo changamoto ni nyingi kama hizo za ufisadi, LAKINI SIWEZI KUMPA FISI MFUPA, NYAMA KAILA NA MFUPA NIMPE? bora nilambe hata mfupa
 
Hakuna shida.Sababu I value my vote.Pole.Ndiyo maana situmii matusi kukujibu.

If you value your vote, then i will be supprised if you vote for someone who has bad scandals
 
Basi CCM kuna sijui shimo au tuite pango la uongozi kabisaaaaa. Heri wenye ombwe. Majirani wameshatumbukia kwenye hilo pango la uongozi
 

Watanzania sasa hawataki blah blah wanataka mabadiliko na ninashikuru sana hata mgombea wenu amelitambua hilo kuwa hakuna mtu anataka kusikia kitu inaitwa CCM ila wanataka mabadiliko!!!
 

magufuliforpresident,what ever the case,issue hapo hakuna chama kilichomleta RAIS msafi wote ni wachafu.Mbaya zaidi kwa sasa tutatafuta sana kupata MSAFI.

Tunapoletewa wezi wawili kwenye uchaguzi mkuu ni lazima mmoja apite,tupende tusipende.Basi nilichokiangalia ni mbali zaidi ya kuwaangalia watu hawa wawili.Nimeangalia haya:

1.Nikimchagua Magufuli,jopo lake la Mawaziri ni wale waliotoa RUSHWA kwenye kura za maoni,sasa hivi pia wako busy wanamwaga pesa na kunua shahada za mpiga kura,ninajiuliza ni kweli atafanikiwa kupiga VITA RUSHWA na UFISADI?Nikaliona changa la macho nikipigwa nalo usoni.

2.Nikakaa nisikilize ule wimbo wa CCM Mbele kwa mbele unanieleza kinagaubaga kwamba CCM ni ile ile,na hapa wameniambia kwa uhakika CCM haiwezi kubadilika hata Nyerere arudi,hivyo nikapata mshtuka yale maovu yataendelea.

3.Nimeangalia nguvu kubwa inayotumiwa na waliopembeni akina JK mpaka kutumia matusi,kutudhalilisha watanzania bila kujua kwamba ili kupata URAIS lazima KURA zote zichanyike wasio na vyama,toka vyama vya upinzani na kutoka CCM sasa kama sisi wanachama wa vyama vya upinzani tunaitwa MALOFA,MBUMBU,WAPUMBAVU,NYUMBU,WAKASKAZINI nknk ,nikajiona kwamba hapa issue ya UBAGUZI haitakwisha kamwe,kama tunabaguliwa leo wakati wa UCHAGUZI kesho itakuwaje???

4.Kwa sasa ninaona bora niende vyama vyetu vya MALOFA maana atleast kuna mmoja ameona umuhimu wa kufikia makubaliano na maelewano ili kuondoa chuki zilizojengwa kati yetu kwa miaka mingi.Asante Juma Duni Haji aliyeona umuhimu wa kuwa na MARIDHIANO katika TAIFA.

Kwa unisamehe bure tu,nipo pamoja na MALOFA wenzangu kwenye TEAM ya MALOFA.
 
If you value your vote, then i will be supprised if you vote for someone who has bad scandals

Hata Magufuli anazo,tena mbaya zaidi,unapomtamkia mtu wa kawaida ambaye hata kula yake ya kesho haijui,unamwambia eti APIGE MBIZI kuvuka kwenda kigamboni ni dhihaka ya hali ya juu.

Pili wizi wa mabilioni ya pesa yaliyolipwa kwa WAKANDARASI hewa sijui inahesabiwa kama kitu gani.

Hebu tuone na huu uuzaji wa nyumba za serikali ambapo leo watu wanakaa kwenye mahoteli wengine wakilipiwa $300 kwa siku kwa miaka mitano sijui serikali imelipa kiasi gani na hasara kiasi gani imepata.

Wizara ya Magufuli imenunua kivuko cha mwaka 1970 kwa bilioni 8, na mpaka hii leo hakitembei je na hii nayo tunaiitaje???

Nasema hivi Mwanz tumepewa wezi wawili tuwapigie kura na mmoja ni ndiyo atakayepita,hivyo usidhani sisi watanzania tunavyoitwa MALOFA ,WAPUMBAVU na MAMBUMBU ni kweli tuko hivyo,bali ni baada ya hawa tuliodhani wako kwa ajili ya TAIFA kumbe wako kwa ajili ya matumbi yao na leo wakitutukana sioni ajabu.Waliingia wakiwa wasafi wametoka wachafu,wanaonuka UFISADI,WIZI, na RUSHWA,leo bora tumuingize MCHAFU anaweza akabadilika maana kwa Mungu kila kitu chawezekana maana hata SAULI leo wakristu tunamuita MTAKATIFU PAULI.....
 

Kuna mawili unarithika na maendeleo unayodhani yapo lakini ni mfaidika mkubwa wa system mbovu iliyopo.Miaka 54 watu wanalala chini hospitali.Miaka 54 watanzania hawana maji safi na salama ya kunywa.Nimekaa Mbeya mjini kwa siku tatu mfufulilizo hakuna maji hata tone na wanalalamika wanamwaka maji hawapati,sasa najiuliza kama mijini hakuna maji vijijini kukoje???

Sijaona cha maana kilichopo ambacho naweza kuisifia CCM.Tulichangishwa kwa lazima CCM ikafungua Supermarket (SUKITA) ilikufa kifo cha mende,Mabasi ya wanafunzi ya kafa kifo cha mende,RTC zikafa kifo cha mende,shule za wazazi sidhani hata kama zinathamani ya kuitwa shule leo,viwanda hakuna vyote vimeuzwa na kila kiongozi kajipatia fungu lake.

Hakika napata hasira zaidi na zaidi,ni bora hawa unaowaita wanafiki na wao waingie tuone watatuvusha mpaka wapi.Na CCM wakae chini wajitafiti kuona ni wapi wanaweza kujirekebisha,ili kisife kabisa kibaki kama kumbukumbu ya Nyerere.
 
Sawa, nimekuelewa, ni nani kama SI Magufuli, atakayeweza kupambana na UFISADI, RUSHWA na UBADHILLIFU.

Hawezi sababu yeye mwenyewe ni FISADI kwenye ngozi ya KONDOO,na kati ya hao atakao wateua kuwa mawaziri pamoja na waziri wake mkuu wamepata UBUNGE kwa RUSHWA.Hebu ona wale ambao hawakutumia RUSHWA kwenye kura za maoni ndiyo wengi wametemwa,99% ya wanaogombea ubunge leo kwa CCM wametoa RUSHWA kwenye kura za maoni na sasa wako busy kununua wapiga kura maana wanajua hali za watanzania hivyo wanatumia pesa walizoiba kuendelea kukaa madarakani.

Hivyo in short MAGUFULI hawezi na hataweza kamwe,labda hiyo MAHAKAMA ya mafisadi na wala rushwa na muundia LOWASSA tu.

Juzi tu ameenda kumpigia debe CHENGE na kumsifia sana wakati ana skendo nyingi sana,leo utaniambia eti MAGUFULI ataweza labda wabunge wote waliotoa rushwa wafe kabla ya kuapishwa na wengine waje.
 

Fisi apewe mfupa, siyo, hayo unayoyanena, ningepende uje na ushahidi kwamba baadhi walipata uwaziri kwa rushwa na bla blaa nyingine, wewe ni shabiki wa LOWASSA bila shaka, umeshikwa masikio
 
Fisi apewe mfupa, siyo, hayo unayoyanena, ningepende uje na ushahidi kwamba baadhi walipata uwaziri kwa rushwa na bla blaa nyingine, wewe ni shabiki wa LOWASSA bila shaka, umeshikwa masikio

Hivi Mbunge anapoingia BUNGENI akiwa na asilimi 100 ya kuingia huko kwa kutumia RUSHWA tumuitaje?Tumuite SHUJAA au???

Ni vyema mtu akanishika MASIKIO kuliko wewe uliyeshikwa UBONGO maana hata kufikiri ni sifuri.Pole.

For your information mimi siyo Pro-Lowassa wala Pro-Magufuli kwangu mimi wote hawa wawili ni wezi,huyu mmoja anajulikana na huyu mwingine amejivika NGOZI ya kondoo.Usilolijua ni kama usiku wa kiza.

Bora huyu anayejulikana ni rahisi kumcontroll kuliko huyu aliyevaa ngozi ya kondoo.

Pole sana.
 

Sasa wewe inaonesha ni sawa na mtu aliyekuwa njia panda haelewi afanye nini, maana kwa hali ilivyo tunahitaji kufanya uamuzi wa nani anakuwa rais, kwa kuwa hujaniambia hasa unachokilalamikia ni nini, bila ya kujua njia ya kutatua. Mf ukisema huna pesa, inajulikana watu watakutafutia kazi, sasa unalalamika halafu kichwani kwako hujui hata cha kufanya. Umesema wewe siyo PRO wa Lowassa wala Magufuli, sasa hizo taarifa ulizozitoa ya kwamba wao ni wezi umezitoa wewe kama nani, hakimu au polisi?
 
kama wakiwa wakiendelea tu kwenda kwenda tu bila muelekeo na kufanya mambo bora liende, wataishia pabaya saana, na kama hawatajipanga vizuri, nakuishia kutetereka kwa migogoro yao, tutawazika oktoba, hii .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…