CHADEMA kumtema mbunge wa NCCR (Mkosamali) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kumtema mbunge wa NCCR (Mkosamali)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by 2015, Oct 12, 2011.

 1. 2

  2015 Senior Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Itakuwa busara cdm wakikataa kumpokea huyu kijana kwa lengo la kumsimamisha kuwa kugombea ubunge labda awe mwanachama wa kawaidi kwa sababu zifuatazo:

  1. Mkosamali ana uwezo wa kawaida sana kiasi kwamba atawasumbua wakati wa kumnadi labda angekuwa na uwezo km wa kafulila angefikiriwa.

  2. Alishinda kwa kubebwa sana na baadhi ya viongozi wa dini ambao walikuwa na ugomvi na mgombea wa ccm kwa kuwa aliwahi kuwashtaki mahakamani na kutakiwa na mahakama kumlipa mamilioni ya fedha na pia mgombea huyo wa ccm anasemekana kuwa ni jambazi, endapo ccm watambadilisha itakuwa hatari sana kwa chadema.

  3. Hadi leo hana hata chembe alichokifanya ktk jimbo ile hali wakati wa kampeni alitoa ahadi nyingi sana kwa kusema atazikamilisha ndani ya muda mufupi hivyo ccm watapata mahala pa kushikia kwa kusema wapinzania hawawezi kuwaona mawaziri ndo maana hata huyu hadi leo hana alichoweza

  4. Kesi yake ni kubwa sana na ana asilimia nyingi sana za kushindwa na ndo maana anahangaika mapema hivi, kwa mtaji huu chadema wampokee au wasimpokee uchaguzi mdogo itakuwa ni lazima.

  5. Huyu mkosamali ni miezi 3 kabla ya uchaguzi wa mwaka jana alikuwa ni kiongozi wa vijana wa chadema wilaya na alihamia nccr yeye na Moses machali wa kasulu mjini kwa taarifa zisizo rasmi kuwa mbatia atawapa pesa za uchaguzi ambazo chadema walisema hawataweza kuwapa kwa uchaguzi ule. Km aliweza kuhama kwa sababi mbovu km hii kuna haja gani ya kumpokea? Akipewa pesa na ccm si atatuuzia jimbo?
  6. Chadema kwa sasa ina vijana wengi waadilifu na wenye mapenzi ya kweli km vile kashindye wa igunga watakaoweza kupeperusha bendera ktk uchaguzi mdogo na sio tuokoteze hawa wasioeleweka misimamo yao na kuwakabidhi majimbo.

  Chadema imara itajengwa na wanachama imara,
  Viva chadema viva Tanzania

  Naomba kuwasilisha
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu unataka kunyemelea jimbo au?
   
 3. 2

  2015 Senior Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi jimbo langu ni kasulu mjini na sio muhambwe la kibondo ila ni mwanachama muadilifu wa chadema ninaeamini chadema ni yetu na tutaijenga sisi wenyewe na sio hawa maweru weru
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kumbe mnajuana!! Huenda una mtu wako huko Muhambwe!! Hivi mzee Ntagazwa aligombea jimbo gani na kwa ticket ya chama gani?
   
 5. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kichwa cha habari 'kina-mis lead',

  Naona unatafuta ''attention''
   
 6. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,177
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Mbona mtoa mada kama anaonekana kuwa asiyeamin ktk alichokiandika!??
   
 7. 2

  2015 Senior Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kivip kaka elezea
   
 8. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuuu ujui historia ya mbunge umesemaye,
  Tatizo ni wivu.?
  Mbona alikuja shibuda na akashinda kwa tiketi ya CDM
   
 9. 2

  2015 Senior Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Muhambwe ndo jimbo la huyu huyu mkosamali, pale kwa yule mzee chadema walikosea ila ikikosea. Mambo ya kuwa na mtu uyapeleke ccm chadema wote mnachukua form km ilivyofanyika igunga then mwenye kura nyingu anateuliwa, pia mtu ukiwa na unatoka karibu na mtu fulani hautakiwi kutoa mtizamo wako? unatakiwa uangalie kilichoandikwa na sio aliyeandika anatoka wapi
   
 10. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hoja zaifu sana juu ya mbunge yule.
  Amesahau kuwa kijana yule alijifanyia kampeni na kuwabwaga CCM NA CDM
  Je wataka akafanye nini zaidi ya kushirikiana na wananchi waliomchagua yeye hapate wapi pesa ya kutatua mataizo ya watu wake.
   
 11. 2

  2015 Senior Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haya bana yangu tayari nimeyasema, sidhani km kutoa mtizamo kwa jambo fulani ni wivu.
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  kijana anajitahidi ila CDM wasimpe dhamana hiyo otherwise aende CCM wampige benchi ka Tambwe Hizza
   
 13. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,129
  Likes Received: 2,188
  Trophy Points: 280
  acha utoto mkuu fikiria kabla ya kurusha rusha vdole vyko hvo!
   
 14. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kichwa cha habari 'kina-mis lead',

  Naona unatafuta ''attention''
   
 15. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2011
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Well, alibebwa na viongozi wa dini? Huwezi kuthibitisha hili. Ninachojua ni kuwa viongozi wa dini walikemea rushwa sana, na mtaji wa CCM Muhambwe ulikuwa ni Rushwa.

  Huyo mgombea wa CCM Jamal Tamim hakuwa safi (Kura za maoni za Wahusika wa Biashara za Maalbino alikuwa No. 1 wilaya ya Kibondo), hata Kamati ya Maadili ya CCM Mkoa haikuwa na imani naye.

  By the way, kwa nini Castico alihamishwa kutoka Kigoma wakati wa kampeni? Ni kwa kuwa naye hakuwa anakubaliana na kupitishwa kwa Jamal.

  CCM walijiangusha wenyewe Muhambwe kwa chaguo baya la mgombea na CHADEMA walifanya kosa kumweka Mzee Ntagazwa ambaye alishaboa sana. Hapo hata bila ya viongozi wa dini njia ilikuwa nyeupe kwa Mkosamali lakini alijipigania kiasi cha kutosha.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hakuna sababu ya kuongeza zaidi gharama za uchaguzi. Bora aendelee kuwa mbunge kama alivyo, na litakapovunjwa bunge ndipo ajiunge na Chadema akipenda.
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  aisee....... kwahiyo chadema ni yenu??mbona hapo umeongea kama Nape aliyesema tanzania ina wenyewe??
   
 18. n

  nndondo JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  He mbona huyu jamaa anaongea vapour? inamaana haoni tofauti ya kauli ya nape ya kwamba Tanzania ni ya CCM na ya huyu mr 2015 kwamba chadema ni yetu? shit! watu wengine bwana ni stereo type kwa kwenda mbele ni lazima wapinge hoja za wenzao and in so doing wanazidi kuwa mambumbumbu, niko very dissapointed ni kiwango cha michango ya watu wengine, yaani ili mradi tu apinge na aonyeshe kwamba hakuna tofauti lakini maisha bora ya kija ndio hao watakaokua wakwanza kufaidika na hatauliza kuna tofauti gani kati ya utawala wa CCM na chadema maana atakua ameshiba amevimbiwa, shame kabisa!
   
 19. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mbona mbowe anauwezo wa kawaida sana kataka kufikiri kuliko mkosamali na mmempa uenyekiti wa chama au bso chama ni cha mkwe wake(mtei),kama ni kuhama chama mbona Dr slaa alikua mwanachama mwaminifu wa ccm au hilo hamlijui na leo ni katibu mkuu kwa nini asinge pewa prof.baregu ambae katika maisha yake hajawai kua ccm,kama hakuna alicho kifanya jimboni kwake mbona hata lema wa arusha hakuna alichokifanya zaidi ya kuwa na malumbano na viongozi wake wa chama jimboni.kama tatizo ni kesi inamwendea vibaya mbona hata lema wa arusha kesi yake lazima ashindwe.kamanda kama unanyemelea ubunge kwa chadema kaa vizuri ya mbowe kwani CDM sio chama bali ni kampuni
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkosamali kimsingi ni kijana wetu ambaye alijichagulia kujifunza siasa hata akiwa mazingira nje ya CHADEMA lakini sasa AMEJIFUNZA kwamba nyumbani kwake sahihi ni CDM.

  Sasa kijana akisharudi nyumbani na zile juhudi zake binafsi tunazozifahamu kwa rekodi ya hapo nyuma kidogo, ni vema tukampitisha kwenye tanuri lile lile la kuzingatia utaratibu wetu wa demokrasia ya ndani ya chama chetu ambapo binafsi nampa nafasi kubwa kuibuka mshini, CHADEMA tumpe huyu kijana sapoti ya nguvu.

  Tunapojiuliza maswali ya msingi kama vile 'Mhe Mkosamali anatafuta nini tena CDM ambacho hakipati kule NCCR Mageuzi ambacho hashawishiki kwenda kukitafuta kupitia hata huko CCM au TLP wakati kama ni ubunge tayari yeye yuko mjengoni Dodoma???????' na jibu linaonekana wazi mno hapa chini.

  Hakuna ubishi kwamba Mhe Mkosamali (1) anatafuta CHOMBO SAHIHI kumwezesha kutumikia vema wapiga kura wake, (2) anatafuta demokrasia ya ndani ya chama na kupewa nafasi ya kutosha KUWA CHACHU WA MABADILIKO YA KWELI HUKU AKICHEZA KAMA MWANA-TIMU anayepewa ushirikiano wa kutosha.

  Ndio, nasema ya kwamba mbali na huyu ndugu yetu kuhitaji zaidi kutiwa moyo kama mfano bora VIJANA KUWA NI VIONGOZI WA LEO NA WA SI LAZIMA KUWA TU VIONGOZI WA KESHO; (3) Mhe Mkosamali kama mwanasiasa chipukizi kuliko wote katika Bunge letu hili kimsingi anatafuta MALEZI MEMA KISIASA ili baadaye naye aje awe kama Mwalimu Nyerere wa kizazi chetu hiki ambapo hakuna ubishi kwamba tunakabiliwa na changamoto za HITILAFU ZA MAADILI NA UONGOZI BORA.

  Hakuna anayeshindwa kukubali kwamba huyu ndugu tayari anayo mtandao wake wa kutegemewa jimboni, aliyenayo MKAKATI MAENDELEO YA JIMBO iliobora zaidi kwa sasa ni Mhe Mkosamali.

  Nawaamini sana viongozi wetu wa chama busara zao, umahiri katika maamuzi ya kidemokrasia hivyo kumsaidia zaidi kujenga jimbo lake na hivyo tutaweza kufanikiwa kupunguza idadi ya maadui wa kisiasa mkoani hapo, kutumia gharama ndogo kumpata mbunge kupitia kijana anayependwa sana mashinani, na kubwa zaidi kuweza kuteka majimbo mengine mengi maeneo ya hapo jirani.

  Vijana tutazame mbele zaidi kuona picha kubwa kuliko kuendelea kutukuza vitu vidogovidogo. Maslahi ya Tanzania mbeeeeeele kama tai, mambo mengi yote baadaye.


   
Loading...