CHADEMA kumjadili Kikwete

CHADEMA kumjadili rais Kikwete na si serikali,CCM wala sera zake katika vikao vyake ni dhahiri bila kutafuna maneno kuwa usumbufu wote wanaowasababishia watanzania ni mtazamo na chuki binafsi waliyonayo baadhi ya viongozi wakiongozwa na Dr Slaa.
 
Vikao vingine ni vya kula posho Raisi anatekeleza majukumu yake kikatiba; hao Chadema watathmini M4C zao; ni upuuzi mtupu Raisi wa jamhuri ya Muungano ashurutishwe kutekeleza majukumu yake na kikundi cha wahuni wachache hivi wanajua nini maana ya Raisi JMT? Raisi Kikwete hakujiweka madarakani tulimchagua kwa kishindo na anatufanyia kazi kwa uwezo wake wote bila kutubagua.
Chama
Mongavyeru

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hawawezi kujadili udaku na upuuzi kama huu! Jadili wewe na Nape na yule mwizi wa pembe za ndovu(jangili)........

Rottashololwa kama hii issue ya kadi inanyamaziwa katika vikao vyenu basi CHADEMA hakuna wanachama hai kuna wafu.
 
- Bado wanakwepa kujadili kadi ya Slaa? Kweli Slaa ni kiboko huko Chadema!!Es!

..........

Mi mbona ninazo za Chama pamoja na umoja wa vijana niliizipata wakati ule tukilazimishwa mashuleni na vyuoni, unatakiwa ujue hilo suala ni la kipuuzi na limeanzishwa na mpuuzi na ndo maana linaishia kupuuzwa tu.
 
Rottashololwa kama hii issue ya kadi inanyamaziwa katika vikao vyenu basi CHADEMA hakuna wanachama hai kuna wafu.
Hizo zilizotajwa ni Agenda muhimu hilo linaweza kujadiliwa kwenye MENGINEYO kwa sababu si muhimu sana.
 
CDM walisema hawakubaliani na utaratibu uliotumika kumweka rais madarakani. Na ndio maana leo hii unauona mchakato wa katiba mpya kitu ambacho hakikuwa kwenye ilani ya mafisadi (ccm).........

kama ishu ni utaratibu mbona huo utaratibu ulikuwepo kabla ya uchaguzi ilikuaje waingie kwenye uchaguzi wasiokubali taratibu zake!. Wataenda watarudi hawana wa kumlilia shida zao zaidi yangu-Ndugu Kikwete!
 
CHADEMA kumjadili rais Kikwete na si serikali,CCM wala sera zake katika vikao vyake ni dhahiri bila kutafuna maneno kuwa usumbufu wote wanaowasababishia watanzania ni mtazamo na chuki binafsi waliyonayo baadhi ya viongozi wakiongozwa na Dr Slaa.
Ni usumbufu upi wanaopata Wanzania kutokana na CDM?1. CDM ndo imefanya bei ya Sukari kuwa juu?2. CDM ndo waliofanya Huduma za Afya kuwa duni?3. CDM ndo waliofanya kiwango cha Elimu kushuka hapa nchini?
 
Ni usumbufu upi wanaopata Wanzania kutokana na CDM?1. CDM ndo imefanya bei ya Sukari kuwa juu?2. CDM ndo waliofanya Huduma za Afya kuwa duni?3. CDM ndo waliofanya kiwango cha Elimu kushuka hapa nchini?
Unapozungumzia mfuko wa bei unajua chanz chake au unaropoka tu? shule haina mwisho achana elimu za wanasiasa wanazokupa kwenye mikutano ya hadhara.We mwenyewe ushangai leo wanahubiri amani kesho wanakuambia twende msituni..
 
Nafikiri CHADEMA wangetumia muda huo kujadili matatizo ta watanzania ya namna ya kutatua kero mbalimbali na kumpelekea mapendekezo yao Rais. Otherwise, nitashawishika kuamini kuwa CDM hairidhiki kuona nchi imetulia kama ajenda mojawapo ya DR Slaa aliposema nchi isitawalike.
 
Nafikiri CHADEMA wangetumia muda huo kujadili matatizo ta watanzania ya namna ya kutatua kero mbalimbali na kumpelekea mapendekezo yao Rais. Otherwise, nitashawishika kuamini kuwa CDM hairidhiki kuona nchi imetulia kama ajenda mojawapo ya DR Slaa aliposema nchi isitawalike.
Upeo wako bado ni mdogo sana.

Hivi wewe uoni maauaji ya raia yanayofanywa kila siku na vyombo vya dola halafu wanasingiziwa chadema?

Hujui kama msingi wa maendeleo popote duniani ni Haki, Amani na Uhuru?

CHADEMA ni chama makini sana wanajidili issues tu.
 

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), inakutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam, leo na kesho, katika kikao chake cha kawaida, ambapo mbali na mambo mengine itamjadili Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, ilisema kuwa Kamati Kuu itapokea taarifa ya utekelezaji kutokana na maazimio ya kikao cha dharura kilichokutana Septemba 9, mwaka huu.

Kikao hicho mbali ya kuagiza chama kimwandikie barua rasmi Rais Kikwete ili asimamie utekelezaji wa baadhi ya masuala yaliyoko kwenye mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Nchi, Kamati Kuu pia iliazimia masuala kadhaa.

Miongoni mwa masuala hayo ambayo yaliazimiwa ni kuwataka Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema, na Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, wawajibike kwa kujiuzulu nafasi zao au wafukuzwe kazi.

CHADEMA iliazimia hivyo kwa kuzingatia kwamba mauaji kadhaa yametokea mikononi mwa Jeshi la Polisi ambalo liko chini ya usimamizi wao; na vilevile waliazimia kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Morogoro na askari waliosababisha mauaji ya raia wasio na hatia Morogoro na Iringa wafikishwe mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

Licha ya Rais Jakaya Kikwete kukionya chama chake kuacha kutegemea nguvu ya jeshi la polisi katika kukabiliana na wapinzani, mpaka sasa bado hajajibu barua aliyoandikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kuhusu mauaji yanayofanywa na jeshi hilo kwenye shughuli za chama hicho.

Hata hivyo, watuhumiwa wanaolalamikiwa na CHADEMA wakitakiwa kujiuzulu, kufukuzwa au kuchukuliwa hatua za kisheria, bado Rais Kikwete ameshindwa kuwachukulia hatua yoyote mpaka sasa. Kwa mujibu wa Makeni, kikao hicho cha siku mbili, mbali na kupokea taarifa hiyo kuhusu Rais Kikwete, pia kitakuwa na ajenda tatu ambazo ni taarifa ya hali ya siasa nchini; mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya nchi; na Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).

Mara kadhaa viongozi wakuu wa chama hicho, wamekuwa wakimkumbusha Rais Kikwete kujibu barua yao na kuwachukulia hatua wahusika ili kuondoa hofu ambayo imetawala kwa umma kuhusu mauaji ya raia yanayozidi kujitokeza.

CHADEMA katika barua hiyo kwa Rais Kikwete walitoa wito wakimtaka aunde tume ya huru ya kiuchunguzi ya kimahakama (Judiciary Commission of Inquiry) kuchunguza vifo vilivyotokea katika mazingira tata katika mikoa ya Arusha, Tabora, Singida, Morogoro na Iringa.

Pia kutokana na utendaji wasiokuwa na imani nao wa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, Kamati Kuu ilimtangaza kuwa ni adui wa demokrasia asiyefaa kuwa katika nafasi aliyo nayo.
Kamati Kuu iliazimia kuwa pamoja na kuendelea kuheshimu sheria ya vyama vya siasa, CHADEMA haitashiriki shughuli zozote zitakazosimamiwa na Tendwa hadi hapo atakapoondolewa katika nafasi yake na kuteuliwa msajili mwingine.

Likini pia azimio hili hadi leo halijatekelezwa pamoja na lile la kutaka vyombo vya habari vya umma kuripoti taarifa zao bila upendeleo wowote kwa weledi, maadili na utaalamu wa hali ya juu kutokana na kuendeshwa kwa kodi za wananchi.

eti wamjadili kikwete! kama nani? kwani wao si wanae rais wao slaa? kichekesho.
 
Chadema hawana muda wa kujadili mambo ya kipuuzipuuzi wanajadili issues tu.
Kujadili mambo ambayo huwezi kuyatolea maamuzi ni kupoteza muda; serikali ipo chini ya chama makini CCM; chama tawala ndicho chenye uwezo wa kuijadili serikali kuona inatekeleza vipi sera zake; wengine ni kumpigia mbuzi gitaa.

Chama
Mongavyeru


Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Upeo wako bado ni mdogo sana.

Hivi wewe uoni maauaji ya raia yanayofanywa kila siku na vyombo vya dola halafu wanasingiziwa chadema?

Hujui kama msingi wa maendeleo popote duniani ni Haki, Amani na Uhuru?CHADEMA ni chama makini sana wanajidili issues tu.

CHADEMA inayumba kwa sasa. There are more serious issues za kujadili zaidi ya kumjadili Kikwete. Kaa na mapenzi yako and you will realize when it is too late. Sikulazimishi kuamini ninachokiamini.
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kutetea yanayofanywa na serikali chini ya uongozi wa CCM kupitia JK. Mafisadi na watoto wao kama kina Mingoi na Ritz ndio wanaoweza kufanya hivyo.

Kujadiliwa kwa JK ndani ya Chadema hakumaanishi kwamba wanamkubali. Kwanza mleta mada hajasema kwamba wanamjadili RAISI, bali JK.... Na kutokutumika kwa neno RAISI kunamaanisha kwamba CDM hawamtambui ndio maana wanamuita kwa jina lake .....hawatangulizi hata Mhe ....Hahahahahaha ...akili ndogo kweli hasara!!! Halafu mbaya zaidi ukishazaliwa nazo huwezikuongezewa hata kama utakesha kanisani ama msikitini!!!!!!!
 
Nafikiri CHADEMA wangetumia muda huo kujadili matatizo ta watanzania ya namna ya kutatua kero mbalimbali na kumpelekea mapendekezo yao Rais. Otherwise, nitashawishika kuamini kuwa CDM hairidhiki kuona nchi imetulia kama ajenda mojawapo ya DR Slaa aliposema nchi isitawalike.

istawalike ana ubavu wa kufanya nchi isitawalike?.
Hana..wanamuangalia tu na akicross line anapambana na vitu vizito vinavyoruka.na hapo ndo inakua final.
 
- Bado wanakwepa kujadili kadi ya Slaa? Kweli Slaa ni kiboko huko Chadema!!

Es!

dr.slaa na cdm walisema wana ushahidi kuwa malecela ni fisadi,alipewa hela na patel milioni 200,sofia simba naye aliyasema haya..if i were you i would hate him too
 
CHADEMA wana masuala ya msingi sana ambayo rais alipaswa ayachukulie uzito,lakini hakufanya ivyo. Acheni kugeuza kila kitu kuwa ni siasa. Mi siamini yule kamanda wa polisi wa iringa yuko kazini hadi leo?

I smell something fishy comming in the future...Magamba wanaweza rukana kimanga muda si mrefu.....Just thinking loudly!
 
Back
Top Bottom