CHADEMA kumburuza Dk. Magufuli kortini

CHADEMA kumburuza Dk. Magufuli kortini

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Ni baada ya Dk. Magufuli kutangaza kuwa nembo ya Movement for Change (M4C) ‘kuipora' wakati akifanya mkutano wake wa kampeni mkoani Kigoma kwenye Uwanja wa Kawawa uliopo Ujiji.

Katika mkutano huo Dk. Magufuli alisema "hawa jamaa zangu wa CHADEMA wananipenda, hata ile nembo yao ya M4C ni Magufuli for Change-maana yake Magufuli kwa Mabadiliko."

CHADEMA wanaratajia kufungua kesi hiyo Septemba 21 mwaka huu na kwamba, madai hayo yatakwenda sambamba na madai ya kutumia kauli mbiu ya ‘mabadiliko Lowassa' ambayo kaibadilisha na kuwa ‘mabadiliko Magufuli'.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Ngome Kawe, Mwanasheria wa CHADEMA, John Malya amesema "CCM imekuwa ikivunja sheria za uchaguzi kila siku bila kuchukuliwa hatua yoyote na mamlaka husika, wanatumia nembo za CHADEMA ambazo zimesajiliwa na kujulikana."

Hata hivyo imeelezwa, baada ya Dk. Magufuli ‘kuiba' alama hizo za CHADEMA; wafuasi wake, bodi ya wadhamini na watu wake wa kampeni walianza kusambaza mitandaoni nembo ya M4C huku wakidai ni nembo mpya ya CCM.

Malya amesema mbali na hilo la kuiba nembo ya chama, wamekuwa na tabia ya ‘kukopi' na ‘kupesti' kila hatua inayo pigwa na CHADEMA na kuzitumia katika kampeni zao.

Akivitaja baadhi ya vitu vinavyokopiwa na CCM amesema, Magufuli amesikika mara kadhaa akiwa anatumia sera na Ilani ya CHADEMA na UKAWA, pia amekuwa akiiba kauli mbiu za CHADEMA pindi anapokuwa katika kampeni zake.

"Hii ni dalili za kushindwa kwa CCM hana sera wameishiwa na ndio maana wanafuata nyayo zetu kila tunapoenda na kila tunalofanya wanalifuatilia na kuaza kutukopi. Kwa mfano sisi tunatumia Lowassa mabadiliko mabadiliko Lowassa na wao wameshaiga kwa kutumia jina la Magufuli".
Aidha, Malya amesema CHADEMA inasikitushwa sana na kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa kimya huku vitendo vya rushwa vinazidi kukithiri toka kwa CCM.

Malya ametaja baadhi ya matukio yenye viashiria vya rushwa kuwa, Magufuli alionenekana akimpatia mtoto pesa taslimu elfu 30000 katika moja ya kampeni zake, huku Mgombea mwenza wa CCM Samia Suluhu Hassani naye mara kadhaa ameonekana akigawa pesa kwa wananchi wanaohudhulia katika kampeni zake.

"Matukio yote hayo bado tume imekaa kimya japo kuwa tumeshapeleka barua za malalamiko na kutuahidi kulishughulikia kesho. Vivyo hivyo kwa Taasisi ya Kushuhulikia Rushwa Tanzania (TAKUKURU) ambayo tulitegemea itakuwa ya kwanza kukemea hilo lakini ipo kimya na tumeshaandika barua ya malalmiko".

Amedai, pia CCM wamezidi kukiuka sheria za uchaguzi kwa kuyachana mabango ya Mgombea Urais wa CHADEMA, Edward Lowassa hadharani na kwamba, wanakiuka sheria

Amesema, matendo hayo yote yanayofanywa na CCM na kuwa wanakuika sheria za umiliki wa nembo za biashara ya mwaka 1986 na kanuni ya umiliki huo ya 2000 pamoja na taratibu zingine za umiliki.
 
Mahakamani ni hatua nzuri ila nakuhakikishia hata huko mahakamani itakuwa ni blablaa tu. Katika nchi za kiafrika chama dola huweza kufanya chochote bila hatua za maana kuchukuliwa.
 
Safi sana....hii italeta contradictions.... ashtakiwe tu mana hamna namna. Haahhaahaa, maguful inaonesha alikuwaga anadesa darasani huko nyuma ndo mana anapiga madesa tu hapa. Nani alimuambia ajifanye kiherehere cha kugombea nafasi ambayo haiwezi?
 
Jamani hivi ilani (party manifesto) ya chadema ni ipi? Mie nimefuatilia kwenye mikutano sijamkia mgombea wao akiielzea ilani ya CHADEMA.
 
Haina haja ya kwenda mahakamani hawa watu inaatakiwa washitakiwe kwa wananchi ambao watatoa maamuzi yao october 25
 
jamani hivi ilani (party manifesto) ya chadema ni ipi? Mie nimefuatilia kwenye mikutano sijamkia mgombea wao akiielzea ilani ya chadema

Ilani waitoe wapi porojo tu vipaumbele walivyoviandika vingine anavyoongea mgombea vingine. Lowasa kaja na vipaumbele toka CCM ndo maana unaona wanagongana na Magufuli kuhusu ajenda ya mabadiliko.

UKAWA waliandaa ilani yao ila hakuna cha maana page nyingi ni picha tu za Lowasa akiwa kwenye mikutano hawana tofauti na wanafunzi wanaochora katuni kwenye mtihani wa taifa huku wakiwa na mategemeo ya kufaulu
 
Mmesajili lini Hilo neno lenye M ya Magufuli.?
 
Mahakama nzuri ya kufikisha kushindwa kwa ccm na Magufuli ni ile ya umma wa Watanzania...
Fanyeni siasa... tafuteni namna nzuri ya kuwasiliana mashtaka yenu haya kwa wananchi...
 
Unachelewa kwenda Mahakamani! Nenda tukutane huko...
 
Kwa mtazamo wangu neno ''M4C" naweza lichukulia maana zaidi ya Milioni ilimradi lilete maana ya maneno niliyokusudia....!
 
Kiukweli kimkakati ukawa wameizidi sana Ccm. Na hata kwenye majukwaa ya kampeni. Tatizo ninalo liona Mimi binafsi ni kwamba ccm timu yao ya kampeni siyo wabunifu kitu ambacho kinawafanya was copy baadhi ya mambo kutoka ukawa.
Nafikiri kuna kila sababu Ccm kuangalia upya safu yao ya kampeni haraka iwezekanavyo, tofauti na hivyo watakuwa kwenye wakati mgumu sana siku za mwisho za kampeni zao
 
Back
Top Bottom