Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimetangaza dhamira yake ya kujenga chuo cha kumbukumbu kwa ajili ya kumuenzi muasisi wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei.
Kwa mujibu wa chama hicho, chuo hicho kitajengwa katika moja ya maeneo yanayomilikiwa na Chadema na kitalenga kuwajengea vijana maadili ya uadilifu, uongozi, uchumi pamoja na mbinu za kupinga rushwa, masuala ambayo yalikuwa ni sehemu ya maono ya marehemu Mzee Mtei alipokuwa hai.