CHADEMA kuitikisa Tanzania tarehe 16 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kuitikisa Tanzania tarehe 16

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by namboyo, Apr 13, 2011.

 1. n

  namboyo Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chama cha demokrasia na maendeleo siku ya jumamosi kitawasha moto maeneo mbalimbali kupinga mswada mbovu ulioletwa serekiali juu ya uundaji wa katiba nikwaa maeneo ya udom jana maeneo coed wanachuo wameanza kujipanga vilivyo huku tawi la udom likiwa lishaanza uhamasishaji wa maandamano kwa wanafunzi.habari zilizopo ni kwamba lema atakua dodoma dokta dar mbowe mbeya mswada mbovu hautapita
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni...

  dawa ya ccm ni kuwabana mpaka wajivue chipu!!
   
 3. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  People's power,vp dar yatakuwepo?
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nilivyo sikia Zitto atakuwa Arusha, Dr Slaa atakuwa Tabora.....
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Afu jana Jk tbc1, anasema CCM watapita nchi nzima kuwaambia wananchi upotoshwaji unaofanywa na Wapinzani, nilimshangaa! CDM TUKO PAMOJA.
   
 6. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Mswada umeshaondolewa nawashauri cdm tujipange upya.
  Yapop madudu mengi hata spika makinda tukitangaza maandamano atatoka kwenye kiti.
   
 7. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tutaandamana tunataka serikali ya JK ijui tupo makini na swala la katiba, katiba sio ya chama cha siasa ni ya wananchi. Katiba ndio moyo wa nchi hivyo JK kujifungia chumbani na akina makamba na kutuletea karatasia zilizojaa mzaha hatupo tayari. Wao wameuandika kwa lugha ya kigeni sisi tunakwenda kueleza wananchi kwa lugha ya kimatumbi ili kila raia ajue ni nini kimeandikwa na ni nini kinafanyika.

  1. tunapinga muswada

  2. tunataka uandikwe kiswahili

  3. hakuna dhararu kwenye kutengeneza, kutunga na kuchukua maoni ya katiba

  4. tunataka iundwe tume huru ya kusimamia muundo wa katiba hii

  5. tunataka pasiwe na sehemu yoyote amboyo inawekewa masharti eti isijadiliwe

  6. wadau lazima washirikishe makundi yote ya jamii ili kupata usawa haki na kujumuisha matakwa halisi ya jamii.

  7. hakuna sababu ya kuogopa wananchi ambao ndio waathirika wakubwa wa sheria za yao.

  8. katiba haiwezi kuasisiwa na ikulu kwani ni conflict of interest

  9. JK ni mwana siasa hivyo ushiriki wake utaletwa kutoka kwenye kikundi anachowakilishwa nacho kama vikundi vingine vyovyote.

  10. ni uhuni tume ya uchaguzi kushiriki kwa namna yeyote kwani hawa ndio wezi na walaghai wakubwa
  NK.......
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145




  Na Rehema Mohamed

  CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetaja mikoa 10 ambako yatafanyika maandamano ya Aprili 16 mwaka huu kushinikiza serikali
  kubadili muswada wa katiba na uzingatie maoni ya wadau na kushirikisha umma.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mkuu wa operesheni ya maandamano hayo Bw. Singo Benson ambaye pia alitaka viongozi wa chama hicho watakaoyaongoza, alisema lengo lingine ni kushinikiza mswada huo uandikwe kwa lugha ya Kiswahili badala ya Kiingeleza.

  Bw. Benson alisema suala lingine ni kutaka serikali kutoa muda kwa umma kabla ya muswada huo haujaenda bungeni kupitishwa.

  Aliitaja mikoa itakayofanyika maandamano hayo kuwa ni Morogoro ambapo kiongoozi wa maandamano atakuwa Mbunge wa Mpanda mjini Bw. Said Arfi, Arusha Bw. Zitto Kabwe, Kigoma Bw. Ezekiel Wenje na mkoa Ruvuma yataongozwa na Bw. John Mnyika.

  Mikoa mingine ni Dodoma yatakayoongozwa na Mbunge wa Arusha Bw. Godfrey Lema, Pwani Makamu mwenyekiti wa Chadema, Zanzaibar, Mtwara yatakayoongozwa na Bw. Mabere Marando, Tabora Bw. Willibod Slaa, Mbeya Bw. Freeman Mbowe pamoja na mkoa wa Kilimanjaro.
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,198
  Trophy Points: 280
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetaja viongozi wake wakuu watakaoongoza maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika katika mikoa 10 ya Tanzania Bara, Jumamosi wiki hii.

  Maandamano hayo yanalenga kuishinikiza serikali, pamoja na mambo mengine, kubadilisha Muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba wa Mwaka 2011.

  Pia, kuitaka serikali kutoa muda kwa wananchi kushauriana, kujadiliana na kutoa maoni kabla muswada haujafikishwa bungeni; na muswada kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

  Mkuu wa Operesheni hiyo, Singo Kigaila, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa maandamano hayo yataongozwa na timu 10 tofauti zitakazojumuisha viongozi wakuu wa kitaifa, wabunge, wajumbe wote wa Kamati Kuu (CC) na wa sekretarieti ya chama katika mikoa ya Arusha, Mbeya, Kigoma, Kilimanjaro, Ruvuma, Dodoma, Pwani, Mtwara, Tabora na Morogoro.

  Alisema timu ya Mbeya, itaongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akishirikiana na Mjumbe wa CC na Mbunge wa Viti Maalum, Chiku Abwao; Mjumbe wa CC na Mbunge Viti Maalum, Naomi Kaihula; Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde; Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, Wilfred Lwakatare, na Thomas Nyimbo.

  Timu ya Tabora, itaongozwa na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, akishirikiana na Mjumbe wa CC na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Nyangaki Kilungushela; Mjumbe wa CC na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; Mbunge Viti Maalum, Lucy Owenya; Mbunge Viti Maalum, Anna Maulida Komu; Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema na Fred Mpendazoe.

  Timu ya Morogoro itaongozwa na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara ambaye pia ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi; akishirikiana na Mjumbe wa CC, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa huo na Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Kiwanga; Afisa Ulinzi na Usalama, Hemed Sabula; Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Musa Yusufu; Mbunge Viti Maalum, Mariam Msabaha; Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda; na Mbunge Viti Maalum, Christowaja Mtinda.

  Timu ya Pwani itaongozwa na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Saidi Issa Mzee; akishirikiana na Mbunge wa Mbulu, Mustapha Akunaay; Mbunge Viti Maalum, Anna MaryStella Mallac; Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Dk. Antony Mbassa; Mbunge Viti Maalum, Conchesta Rwamlaza; Mbunge Viti Maalum, Christina Lissu; na Afisa Mwandamizi Sheria na Haki za Binadamu, .

  Timu ya Arusha itaongozwa na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe; akishirikiana na Mjumbe wa CC na Mbunge Viti Maalum, Grace Kihwelu; Mwenyekiti Mkoa huo, Samson Mwigamba; Mbunge wa Ilemela, Higness Kiwia; Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbayi; Mbunge Viti Maalum, Raya Ibrahim; na Profesa Abdallah Saffar.

  Timu ya Mtwara itaongozwa na Mjumbe wa CC, Mabere Marando; wakati ya Kilimanjaro itaongozwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu; ya Kigoma itaongozwa na Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje; ya Dodoma itaongozwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema; na ya Ruvuma itaongozwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.

  Kigaila, ambaye ni Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, alisema tayari wamekwisha kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na kuwataka wananchi wa mikoa hiyo kujiandaa kwa ajili ya maandamano hayo.

  Alisema hawatakwenda katika mikoa ya Kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Kagera kwa vile wamekwisha kwenda huko, hivyo wananchi wa mikoa hiyo watajiunga nao katika maandamano ya sasa.
   
 10. g

  gwala Member

  #10
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakitoka huko waje Acity na kilimanjaro
   
 11. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hoja ya Msingi hapo ni kupinga muswada wenyewe, tunataka katiba mpya sasa kwa nini unakuja muswada wa kupitia katiba na kufanya marekebisho!?. kama ulivyosema Katiba ndio Uti wa mgongo wa Taifa lolote, ndiyo Sheria mama, sasa katiba haiwezi ikatungwa na CCM peke yake bila kushirikisha wadau wengine. Itapendelea CCM tu, huu ni wakati wa mfumo wa vyama vingi, watendaji wote wa vyama wanauzito sawa, kwa hiyo wanapaswa kushirikishwa wote kwa uwiano ulio sawa. Unaposema katibu mkuu wa CCM maana yake yupo sasa na wa NCCR, TLP, CUF, Chadema na vyama vyote vilivyosajiliwa kisheria, kiutendaji na kimamlaka. Na hawa wanawafuasi amabao ni wanachi na ndio wenye katiba! CCM acheni Jeuri, acheni kiburi zile enzi zenu zimepita na zimezikwa!.
  Zamani CCM walizoea kwa kuwa wananchi hawakuwa na uwezo wa kusema hapana kwa jambo lolote, kwao ilikuwa ndio mzee, zama hizo zimepitwa na wakati na sasa ni enzi za ukweli na uwazi, tutapinga njama hizi za kutaka kutumia mabilioni ya walipa kodi kwa njia za kuleta mabadiliko ya kiujanja ujanja usiokubalika wa CCM. Chadema leta maandamano maana ndiyo njia pekee naya haki ya wanachi kuonyesha hasira zao kwamba wamegundua janja ya CCM katika hili suala nyeti la katiba ya nchi yetu, na pia wajue hakuna aliyezaliwa na dhamana ya kuiongoza nchi hii, viongozi watatoka miongoni mwetu na sio lazima wawe CCM na hata wakitoka CCM si lazima wawe wale wale miaka nenda miaka rudi!, kila kukicha Chiligati, Zhakia, Kingunge, Makamba! No, Tupo Viongozi na wapo wengi tu hawajapewa nafasi eti kwa sababu wanapinga sera za CCM, sasa ni wakati wa kuwakomboa Wanachi kutoka katika huu unyonyaji ulipitiliza, tumenyonywa na watu wachache kwa miaka 50, sasa imetosha! wanatumia raslimali za nchi kwa manufaa yao binafsi, sasa basi imetosha. na tusimame kidete kutetea maslahi ya watoto wetu, wajukuu wetu na wote waliokandamizwa kwa kukosa huduma bora za Jamii.
   
 12. m

  msambaru JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Jamani vitu kama hivi tunavingoja kwa hamu singida, lini jamani? Dewji nae yupoyupo tu njooni tumchimbue.
   
 13. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  Dar vp?
   
 14. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dar kibali kimeshindikana na tarehe hiyo, CCM wana maandamano ya kufa mtu kumuunga Mwenyekiti wao kwa kuanzisha mjadala wa mswada wa katiba, kukubali mswada uandikwe kwa kiswahili, kuvuta subira uwasilishwaji wa mswada wa katiba bungeni na kuondoa magamba chamani. CDM mkae mkao wa kuumia!
   
 15. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  CDM wanaelekeza nini kifanyike hawawezi kuumia. CCM wanafuata ili waendelee kuwepo wepo kwenye ramani.
   
 16. n

  ngurati JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nashauri aliyekuwa mgombea ubunge arumeru mashariki, Nassari Joshua naye akajumuike na lema dodoma, vijana wamakunbali sana uwezo wake wa kujenga hoja na ukizingatia ni kijana mdogo wa miaka 24 tu na dodoma kuna vijana wengi sana wa udom . Nimeona mara nyingi wanapokuwa kwenye harakati na lema combination inakubali sana. Ni mawazo yangu tu
   
 17. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CCM ni sawa na mgonjwa anayesubiri operation lakini kwa hofu anaiahirisha. walipogundua kuwa kuna maandamano ya CDM wao wakaanzisha ya kwao, na kwa vile polisi ni waajiriwa wao lazima watatoa kipaumbele kwa CCM.
   
Loading...