CHADEMA kuishitaki serikali ICC

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
CHADEMA kuishitaki serikali ICC


na Sitta Tumma, Geita


amka2.gif
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeelezea dhamira yake ya kutaka kuishitaki Serikali ya Rais Kikwete katika Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia Makosa ya Jinai (ICC), kutokana na kusababisha mauaji ya raia wasio na hatia yaliyofanywa hivi karibuni na Jeshi la Polisi huko mkoani Arusha.
Pia chama hicho kimepanga kuifikisha na kuishitaki serikali kwenye Jumuiya ya Ulaya, iwapo haitawajibika kumfukuza kazi iwapo atashindwa kujiuzulu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, kutokana na kashfa hiyo.
Aidha, CHADEMA ilisema ushahidi wa wazi unaonyesha mauaji hayo yalikuwa na baraka kutoka kwa viongozi wa ngazi ya juu ya serikali ambao ndio waliomshauri Kamanda Mwema kuzuia maandamano hayo muda mfupi na kusababisha ghasia na mauaji hayo.
Tamko hilo limetolewa juzi wilayani Geita, mkoani Mwanza na Mkurugenzi wa Oganizesheni wa chama hicho, Ignas Karashani, wakati akizungumza na waandishi wa habari kulaani mauaji hayo.
Alisema Januari 5, mwaka huu, Jeshi la Polisi mkoani Arusha lililazimika kuwapiga na kuwaua kwa risasi za moto waandamanaji watatu na wengine kujeruhiwa vibaya, katika maandamano yaliyoitishwa na CHADEMA.
“Tumedhamiria kuishtaki serikali kwenye Mahakama ya Kimataifa ya ICC, pia mashitaka haya tutayafikisha kwenye Jumuiya ya Ulaya iwapo Rais Jakaya Kikwete atashindwa kumfukuza kazi IGP Mwema,” alisema.
Aidha, alimuonya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, kuacha mara moja kutoa taarifa za kejeli katika masuala yanayoligusa taifa huku akimfananisha na mtu aliyezeeka ndiyo maana katika tukio la mauaji ya Arusha ameendelea kukejeli.
“CHADEMA hatuwezi kuwa na viongozi wanaochochea ghasia na kuua Watanzania wenzetu…Tunachotaka Serikali ya Rais Kikwete iwajibike kwa mauaji ya Arusha,” alisema.
 
Hii kesi ICC wataipokea na kuishughulikia haraka sana kwa sababu serikali iliyopo madarakani haina nia ya kuwakamata IGP, RC-Arusha na Waziri wa mambo ya ndani na kuwafikisha mahakamani kwa mauaji ya raia wasiyo na hatia..........................kwenye mazingira haya yanaruhusiwa kabisa na sheria za ICC ziitwazo "complementarity rules" kuingilia dhuluma ambayo CCM iliifanya hapa Arusha.................................
 
Waanze, halafu ndio wataijuwa hiyo mahakama, kuna vichwa pale. Kwanza wataangalia maandamano yaliamrishwa na nani na kwa nini? Aliyeanzisha maandamano ndie wa kwanza kujibu. Hapo patamu kweli. Waanze. Kwenda leo, mbona wanachelewa?
 
Hapa ngoma inogile,Ccm wote rumande,makamba keko,Kikwete Gwantanamo,Chitanda milembe,CHIKAWE SEGEREA.
 
Back
Top Bottom