CHADEMA kufanya maandamano ya kulaani jeshi la polisi

CHADEMA kufanya maandamano ya kulaani jeshi la polisi

Rich Pol

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2013
Posts
7,877
Reaction score
5,700
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)mkoani hapa kinatarajia kufanya maandamano makubwa kesho- kulaani- jeshi la polisi kushindwa- kukitia mbaroni kikundi kinachodaiwa- kufanya-- vurugu na kuwacharanga kwa mapanga na shoka wafuasi wake- katika kampeni za uchaguzi udiwani zinaoendelea Kata ya Sombetini.

-Mpango huo ulitangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mbunge wa Arusha Mjini wa Chadema, Godbless Lema.

Lema alisema- chama hicho kimeishiwa uvumilivu kutokana na kikundi hicho kuendesha vitendo hivyo tangu kuanza kwa kampeni zake za kumnadi mgombea wao.

Alisema matukio ya kuvamiwa na kupigwa kwa wafuasi wa chama hicho yamezidi kukithiri kutokana na polisi kushindwa kuwachukulia hatua kali dhidi ya kikundi hicho.

Lema alisisitiza kuwa Chadema hakitasubiri kibali cha polisi cha kufanya maandamano,- bali kitatoa taarifa ya kuwapo kwake ili kufikisha kilio chao na kuiwezesha dunia kufahamu- kuwa Arusha bado si shwari .

''Juzi mfuasi wetu amekatwa panga kichwani na kufyekwa vidole,tumetoa taarifa polisi ,hakuna hatua zozote zilizochukuliwa,tupeleke wapi kilio chetu , tumeona bora tuandae maandamano ya amani kulaani matukio hayo,'' alisisitiza Lema.

Alisema wao kama wafuasi na wanachama wa Chadema wapo tayari kukamatwa kwa kuandamana kupinga unyanyasaji unaofanywa dhidi yao.

Kwa mujibu wa Lema,- hadi sasa zaidi ya wafuasi 50 wa Chadema- wamejeruhiwa vibaya na magari matano kuharibiwa kwa kuvunjwa vioo. Hadi juzi matukio saba yametokea tangu kampeni hizo ambazo zilianza Januari 15, mwaka huu na hakuna mtu aliyekamatwa kwa kuhusishwa nazo.

Alimtuhumu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha , Liberatus Sabas kuwa ameonyesha chuki za dhati dhidi yake na Chadema kwa sababu amekuwa hapokei simu yake anapompigia kumtaarifu matukio ya uhalifu yanayoendelea katika kampeni hizo.

Kwa upande wa Kamanda Sabas, akizungumza kwa njia ya simu na NIPASHE alikana tuhuma za kumchukia Lema na kwamba ndiye aliyetangaza kutompigia simu hata kama atavamiwa na majambazi.

''Ndugu zangu mimi simchukii mtu yoyoye- kwanza huyo kijana (Lema)aliwahi kutangaza kwamba, hatanipigia simu yangu hata kama atavaamiwa na majambazi, sasa hapo nani anamchukia mwenzake, ''alihoji Kamanda Sabas.

Akizungumzia kuhusu- vurugu za Sombetini, alisema- hajapata taarifa kamili na kusisitiza-- hakuna aliyejuu ya sheria.

Alisema iwapo kama kuna mtu ameripotiwa kwa kuhusika na- uvunjifu wa amani, atakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

CHANZO:
NIPASHE

Jana kamanda wa polisi mkoa wa Arusha amesema hana taarifa yoyote ya maandamano ya Chadema, na atakae thubutu atashughulikiwa na kuchukuliwa hatua.

MY TAKE:
Kama kuna mtu Ana ndugu jamaa na rafiki Gerezana au mpenzi wake njia rahisi ya kuonana nae kesho aandamane tu.
 
Ni wazi polisi na ccm
wanashirikiana kutesa na kuua raia Arusha. Mali za raia ziharibiwe na raia wakatwe mapanga rpc huna taarifa? Kwanini usiachie hiyo nafasi?
 
Inafika mahali uvumilivu unakua mgumu hasa matendo haya ya kinyama yanapoendelea kufumbiwa macho kwaajili ya maslahi ya wachache. Huu ni ubaguzi wa waziwazi kwa upande wa pili,hivi inamaana ingekua ni ccm wanafanyiwa mambo hayo ya kikatili wangenyamaza kweli? Nina hakika wangeshashikisha watu adabu. Sasa kwanini washindwe kuzuia haya ya mambo ya ajabu yafanywayo na watu wao!! Ama ndo tuamini kwamba machafuko yanayoendlea kuna mkono wa ccm??? Haya mambo mnayoyafanya yana mwisho jamani
 
Hakuna tofauti kati ya IGP mpya na mtangulizi wake!

Anyway,anaewateua ni yule yule kwa malengo yale yale!
 
Anayeua kwa upanga naye atauwawa kwa upanga,RPC acha kujifanya umevaa miwani ya mbao hiko cheo ni dhamana uliyoapa kuwatumikia raia kuwalinda na mali zao,leo masisiem yanafanya makosa ya jinai unasema huna taarifa raia wanataka kuandamana hapo una taarifa na kupiga marufuku,aliyekuwa wazri wako nchimbi sasa hivi anaenda kutambika makaburini...time will tell,dunia ni mzunguko!!!
 
Mbona polisi ilisha laniwa siku nyingi!au labda tuongezee laana nyingine mpya.kiboko chao 2015 hasa makamanda wa mikoa.
 
Me nakwambia cku zitukiaanzisha vita tukakuwa kama somalia hapo, ipo cku uvumilivu utatushinda kbs kila mtu atabeba mapanga na marungu na mikuki, kwa uonevu huu ipo cku tu, sio kwamba nataka vita au napenda vita ila ipo cku uvumilivu utatushinda tu!!
 
Eti liberatus anamwita Lema "huyu Kijana" ! nisawa jamani. Hakuna wa kumkemea kwa huu ujinga. Mie naichukia TZ sana sasaivi.
 
Haya mandamano wanafanya kumlaani lema au kuilaani chadema mbona waajabu sana hawa watu vurugu wafanye wao halafu tena waandamane wao lema bana.
 
Inafika mahali uvumilivu unakua mgumu hasa matendo haya ya kinyama yanapoendelea kufumbiwa macho kwaajili ya maslahi ya wachache. Huu ni ubaguzi wa waziwazi kwa upande wa pili,hivi inamaana ingekua ni ccm wanafanyiwa mambo hayo ya kikatili wangenyamaza kweli? Nina hakika wangeshashikisha watu adabu. Sasa kwanini washindwe kuzuia haya ya mambo ya ajabu yafanywayo na watu wao!! Ama ndo tuamini kwamba machafuko yanayoendlea kuna mkono wa ccm??? Haya mambo mnayoyafanya yana mwisho jamani

Tena mwisho wake ni kifo cha cdm.
 
Anayeua kwa upanga naye atauwawa kwa upanga,RPC acha kujifanya umevaa miwani ya mbao hiko cheo ni dhamana uliyoapa kuwatumikia raia kuwalinda na mali zao,leo masisiem yanafanya makosa ya jinai unasema huna taarifa raia wanataka kuandamana hapo una taarifa na kupiga marufuku,aliyekuwa wazri wako nchimbi sasa hivi anaenda kutambika makaburini...time will tell,dunia ni mzunguko!!!

Basi subiri zamu yako ikuzungukie nawe umtese sabas.
 
Tungeandamana kwa wabunge kujiongezea kiinua mgongo..naona hata wanaojiita wanaharakati wamekaa kimya.
 
Ccm na polisi wao wamejaa dhuluma sana maana kuna jambazi sugu ndio kiongozi wa green guards
 
Back
Top Bottom