CHADEMA: Kipaumbele cha Rais Magufuli ni kununua ndege? Hali ya Uchumi inazorota!

Tubasuburi hali iwe kama zimbabwe
Nimesoma maoni ya mkutano wa CHADEMA juu ya uchumi wetu.
Kuna mambo ambayo hayana ubishi na ni kweli.

Serikali kana ni sikivu ikubali tu na kujirekebisha.
Biashara karibia 7,000 zimefungwa( mwanzoni mwa mwaka huu kulingana na Dr Mpango ilikuwa 2,000)

Mabenki yametikisika, amana zimetetereka.

TRA makusanyo yamedidimia, ni dhahiri hilo kutokana na biashara kufungwa!

Sasa kukua huku kwa uchumi kwa 7% kwetu sisi tulio katika sekta binafsi inatutia mashaka huko tuendako.
Mi ni CCM progressive, na chama hakinilipii buku saba.

Tuzingatie ushauri ili tunaojitegemea tufaidike na nchi yetu.
 
Good for you Mr. Jidu La Mabambasi kwa hatimaye kukubaliana na mawazo ya wapinzani kuwa hali inadorora si kwa pororjo za watawala kuwa wanaolalamika ni wapigadili, bali kwa sababu ya uchumi wetu kudidimia.
 
Mkuu mimi niliyejiajiri, biahara yangu nikiifunga kutokana na hali hii ya kudoroa biashara, TRA hawataKusanya kodi, na watu wanakosa ajira.
Sasa mimi mjasiriamali na wenzangu 7,000 ni kundi kubwa hilo la kutofumbia macho.
 
- Amelaani TRA kuipiga kodi kubwa Acacia kuliko bajeti ya nchi. Kwani hiyo kodi ni ya mwaka mmoja si ni malimbikizo na interest ya miaka zaidi ya 15?

- Amesema Tanzania itasusiwa na wawekezaji. Mbona North Korea imesusiwa na dunia lakini China inafanya nao biashara?

- Kasifia awamu ya nne tulikuwa tunaenda vizuri kiuchumi. Vinavyouzwa nje ni madini, kahawa na korosho. Kama kwenye madini nchi ilikuwa haikusanyi kodi na inapata asilimia 0 ya mauzo. Na inawezekana hata katika exports nyingine za nchi mambo yalikuwa hayo hayo. Anazungumzia uchumi hewa au ni uchumi gani?

- Nchi yenye uchumi hewa inaendeshwa na misaada. Bahati mbaya wanaoiba madini sio wanaotoa misaada. Ina maana kwa mwendo iliokuwa inaenda Tanzania watoa misaada wangechoka na hapo ndio joto ya jiwe ingeonekana.

Mkuu mleta uzi huenda una hoja lakini umeharibu hapo ulipoifananisha nchi yetu na korea kaskazi. Kumbuka korea kaskazini wamefikia hatua ya kutengeneza bomu la nyuklia, wakati sisi hata kumudu chakula cha wananchi ni kazi!! Unaweza kuifananisha N.korea na hii nchi yetu ambayo bila aibu inasema imeibiwa kwa kushindwa kukusanya kodi miaka 15 na bado haina uhakika inadai kiasi gani mpaka sasa? Hili andiko lako ni kujidhalilisha tu.
 
Kwa hiyo wamarekani wakisusia dhahabu za Tanzania na wachina watazisusia?

Tulipopata shida miaka ya nyuma Tanzania haikususiwa kiuchumi. Ilinyimwa misaada kwa kukataa masharti ya IMF.

Na nyinyi mnafanya makosa kuilinganisha Tanzania na Zimbabwe. Zimbabwe kuna mahindi. Tanzania kuna rasilimali. Akilimali tu ndio kidogo ni tatizo.
 
North Korea?Bado Mnaendelea Kuzindua Mabomba Ya Maji Na Vitanda Vya Disp Na Madawati Eti Unajifananisha Na N Korea Anayetengeneza Nykulia,jipange Kijana Ndyo Urudi Hapa
 
- Amelaani TRA kuipiga kodi kubwa Acacia kuliko bajeti ya nchi. Kwani hiyo kodi ni ya mwaka mmoja si ni malimbikizo na interest ya miaka zaidi ya 15?

- Amesema Tanzania itasusiwa na wawekezaji. Mbona North Korea imesusiwa na dunia lakini China inafanya nao biashara?

- Kasifia awamu ya nne tulikuwa tunaenda vizuri kiuchumi. Vinavyouzwa nje ni madini, kahawa na korosho. Kama kwenye madini nchi ilikuwa haikusanyi kodi na inapata asilimia 0 ya mauzo. Na inawezekana hata katika exports nyingine za nchi mambo yalikuwa hayo hayo. Anazungumzia uchumi hewa au ni uchumi gani?

- Nchi yenye uchumi hewa inaendeshwa na misaada. Bahati mbaya wanaoiba madini sio wanaotoa misaada. Ina maana kwa mwendo iliokuwa inaenda Tanzania watoa misaada wangechoka na hapo ndio joto ya jiwe ingeonekana.

Piga hesabu kwa average kila mwaka tulikua tunapoteza trillion 25plus budget halisi ya Tanzania actual budget haizidi 20 trillion
 
Na msisahau wakati South Africa ilipokuwa imetengwa makampuni ya madini ya Uingereza na Marekani yaliendelea kuchimba madini.
 
Back
Top Bottom