CHADEMA kina wanachama wangapi?

mikutanoni huwa ni watoto tu wamekuja kuangalia chopa ila kwa ufinyu wa kung'amua mambo cdm huwa wanawahesabu watoto wale kama wapiga kura pia!
 
Huna tofauti na sokwe unashindwa kuainisha matatizo ya tz eti unahangaika na cdm, utoroshwaji wa twiga wetu kwenda nje,madini kuporwa,tembo wanaisha,mabilioni yanafichwa nje nk hayo huyaoni eti? bk7 shame on u na waliokutuma

kaka mbona umekuja juu hayo ni maono tu kutokana na hali ilivyo, kwanza unatakiwa kutambua maada inayozungumzwa,
Eti unaforce mwalimu wa kiswahili darasani afundishe math katika kipindi cha kiswahili kwakuwa wanafunzi wamefeli sana somo hilo ? chukuwa hatua tafakari
 
Wambie hao chama cha mafisi waruhusu uandikishaji wapiga kura wapya afu kutokee uchaguzi kidogo ndo mtajuta kuzaliwa nyie nyinyiem

Kwa mujibu wako, Wapiga kura wote wapya ni wana-CHADEMA...
 
Watu wanaojazana kwenye mikutano siyo kwamba wanafurahishwa na sera wengi wanakwenda kuangalia Chopa.
 
Watu wanaojazana kwenye mikutano siyo kwamba wanafurahishwa na sera wengi wanakwenda kuangalia Chopa.

aaha hapo naanza kuelewa kumbe wanaenda kushangaa DAH HILI JANGA LA TAIFA!
 
Huwezi kukaa na kutafakari matatizo ya tz yanatatuliwaje ww unahangaika na cdm why? Matatizo ya tz kwa zaidi ya 90% yamesababishwa na chama ambacho ni tusi hata kukitaja(ccm) alaf eti nkuchekee ww
 
WanaJF,

Kwa masikitiko makubwa sana nieleze tu kuwa, CHADEMA kimezidi kupoteza wanachama wake wengi hivi karibuni hali inayopelekea ku kufanya chama hicho kupoteza sifa ya kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Kwa mujibu wa viwango vya kimataifa kwenye masuala ya kisiasa, chama kikuu cha upinzani ni kile ambacho kina wanachama walau nusu ya idadi ya wanachama wa chama tawala!.

Takwimu ya idadi ya wanachama kwa mujibu wa ripoti:

...CCM hadi kufikia March 20 ilikuwa na wanachama 7,892,453.

...CHADEMA hadi kufikia March 20 ilikuwa na wanachama 456,227.

...ACT hadi kufikia March 20 ilikuwa na wanachama 124,567. Baada Zitto kuingia ACT, wanachama waliongezeka hadi kufikia 259,548 sawa na ongezeko la asilimia 100.

...Idadi ya wanachama wote wa CUF, TLP, NCCR na UDP ni sawa na idadi ya wanachama wa CHADEMA.

...Kwa mujibu wa viwango vya kimataifa, CHADEMA kwa sasa ni chama kilichounda kambi ya upinzani bungeni. Lakini hakina sifa ya kuitwa chama kikuu cha upinzani nchini.
 
Wewe kila siku unawashwa na Chadema! Punguza genye gasho.
 
Kwahiyo mwakani tutakuwa na chama kikuu cha upinzani chenye wanachama wengi kuliko chama tawala.
 

Viwango vya kimataifa...!!!! Ha ha ha haa. Acha uongo. CCM taarifa rasmi zinaonesha kuwa ina wanachama millioni 4.
 
Dada Hamida leo umekula maharage ya wapi sijui, unaropoka usubuhi yote hii,
 

Sawa dada hamida chama kikuu cha upinzani kwasasa ni act
 
Mods JF siku hizi! Halafu utaona uzi huu wa kijinga usiokuwa na ukweli wowote unaachwa tu!

Hebu mtu ajaribu kuweka uzi wenye kichwa cha habari kwa mfano: "Wasaliti wa ACT wanazidi kusambaratika kila siku" kama utadumu hata dakika moja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…