CHADEMA kimeutoa mkoa wa Tanga sadaka kwa CCM

CHADEMA kimeutoa mkoa wa Tanga sadaka kwa CCM

bennymas

Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
68
Reaction score
30
Wandugu!

Katika makosa ambayo CHADEMA itakuja kujutia ni kuufanya mkoa wa Tanga sadaka kwa CCM hasa ukizingatia CUF haijajipanga kwenye majimbo mengi ya mkoa huo.Mkoa wa Tanga una wapiga kura zaidi ya Milioni moja.

Mtonyaji wangu wa ndani amenieleza kwamba CHADEMA wamepewa majimbo ya Korogwe Mjini,Korogwe Vijijini,Mkinga,Muheza na Kilindi.Kwa wenyeji wa mkoa wa Tanga lazima watatilia shaka weledi wa timu ya kiufundi (Technical Team) ya UKAWA hasa kwa majimbo ya Kilindi na Mkinga.

1.Kilindi
Mtandao wa kiungozi na wanachama ni moja ya vigezo muhimu hasa kushinda katika uchaguzi. Jimbo la Kilindi halina uongozi wa kikatiba kuanzia ngazi ya jimbo mpaka msingi,halina mgombea anayeleweka wa CHADEMA,jimbo hili lenye kata 20 CHADEMA haina uwezo wa kusimamisha wagombea wa udiwani makini hata kwenye kata tano tu.

2.Jimbo la Mkinga
Kwa kutazama mila na desturi za jimbo husika,kwa kigezo hiki pekee CHADEMA haiwezi kufurukuta kwenye jimbo hili lililopo kwenye fukwe za babari ya hindi,jimbo lililopo njia kuu ya kuelekea Mombasa.Zaidi ya mila na desturi jimbo la Mkinga lenye kata 21 CHADEMA haina mtandao wa chama unaoeleweka na haina wagombea wa udiwani makini hata kwenye kata tano.Angalau CUF wanaweza kufurukuta kwa kuzingatia mila na desturi za wananchi wa jimbo hili wakiweka mgombea anayekubalika.CHADEMA hakina mtandao unaoeleweka.

3.Jimbo la Muheza
Ni ukweli usiopingika kwamba CHADEMA haiwezi kushinda kwenye jimbo lolote lenye mila na desturi za maeneo ya pwani.Muheza jimbo lenye kata 33 CHADEMA inakubalika kwa kiasi kwenye kata ambazo hazizidi nane kati ya 33.CUF inaweza angalau kuleta ushindani kwenye jimbo hili kutokana na kuwa na mtandao wa kichama unaoeleweka ikiwa ni pamoja na mtia nia wa ubunge mwenye ushawishi Dr.Mgaya ambaye alihama CHADEMA na kujiunga na CUF.Pamoja na jimbo hili kuwa kwa kiasi na siasa hai za upinzani kwa vyama vya CUF na CHADEMA ni ukweli usiopingika CUF ina nafasi ya kufanya vizuri kuliko CHADEMA.

4.Korogwe Mjini na Vijijini.
Sina shaka na weledi wa kamati ya ufundi ya UKAWA kuyaweka majimbo ya Korogwe Mjini na Vijijini kwenye mikono ya CHADEMA.Pamoja na ukweli kwamba CHADEMA haiwezi kushinda korogwe vijijini inaweza kufurukuta Korogwe mjini iwapo jitihada za dhati zitafanyika.Kwa kuangalia mila na desturi za watu waliopo karibu na milima ya usambara na milima ya usambara ikiwepo jimbo la Mlalo,Bumbuli na Lushoto CHADEMA kina nafasi nzuri kuliko CUF.Korogwe Mjini ni sehemu nzuri ya kimkakati na ushindi kwa CHADEMA.

Jimbo la Korogwe vijijini lenye kata 20 CHADEMA inauwezo wa kufurukuta kwenye kata 12.Jimbo la Korogwe vijijini lenye kata 8 CHADEMA inaweza kufurukuta kwenye kata 6.

5.Majimbo ya Mlalo,Bumbuli na Lushoto.
Kwa kipindi ambacho nimefanya kazi zangu za uwakala wa usambazaji wa Mbegu za mimea vijijini katika wilaya za Tanga kati ya majimbo matatu ya Lushoto ni jimbo la Lushoto Mjini pekee ambalo CHADEMA inafanya siasa hai (active politics) na kiasi majimbo ya Mlalo na Bumbuli.Mara ya mwisho nilishuhudia Mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara Prof.Abdallah Safari na kufuatiwa mikutano mfululizo ya viongozi wa jimbo ikiongozwa na viongozi wa jimbo wakishirikiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha SEKoMU.

Pamoja na CUF kushinda kata 1 mwaka 2010 viongozi wao wamezubaa sana na sijawahi kuwaona wakifanya mikutano ya hadhara na kibaya zaidi hata kata ambayo wana diwani hawakushinda hata kijiji na kitongoji kimoja.Nitatilia shaka weledi wa kamati ya ufundi ya UKAWA jimbo hili wakipewa CUF.Nimeshuhudia matukio mengi ya kisiasa ya CHADEMA jimbo la Lushoto Mjini na Muheza kuliko majimbo yote ya mkoa wa Tanga.Jimbo Lushoto ni jimbo zuri kwa CHADEMA kutokana na kuwa na mchanganyiko wa makabila mbalimbali na uwepo wa vyuo vya IJA,SEKoMU na Ustawi wa Jamii Mabughai ambapo kwa kiasi kikubwa wanaunga mkona CHADEMA.2010 CHADEMA kilifanya makosa makubwa kumuweka mwanafunzi wa mwaka wa pili wa SEKoMU anayeishi ghetto, mzaliwa na mwenyeji wa Kahama kugombea ubunge Lushoto.

Jimbo la Bumbuli CHADEMA wanaweza kufanya vizuri wakipata mgombea mzuri wa ubunge.

6.Handeni
CHADEMA haina mtandao wa kueleweka Handeni zaidi ya migogoro ambayo inadhofisha chama.CHADEMA haina chake Handeni.
 
Wagumu sana kuelewa hao watanga, ngoja cuf wahusike nao kwanza! Tupo busy na kanda ya ziwa!
 
Watasingizia wameibiwa kura na kulaumu kila kitu kura zisipotosha.
 
bennymas

Wao wanarudiarudia huko kanda ya ziwa " mnyika,salum Mwalim,, mbowe , sasa hivi nasikia tena amekuja LISSU,sijui wamegundua ni kanda ya ziwa
 
Last edited by a moderator:
Mikoa mingi ya pwani, ni shidaaaa!! kiuchumi wako hoi kweli lakini bado wanathamini magamba! !utawasaidiaje watu wenye akili za kushikiwa!! yaaani kama mkoa wa pwani hadi una wahurumia lakini wamo tu, ZAMU HII TUNAKWENDA NA WALE WANAOJITAMBUA NA KUKAMATA FULSA NA KWENDA ZETU, MAPOPOMPO TUNAYAACHA.
 
Hata mikoa ambayo CHADEMA inakubalika haishindi kwa asilimia angalau 60,sasa ukishinda kwa mfano Kagera kwa 54% halafu Tanga unashindwa kwa 86%,mikakati yako haina maana.

CHADEMA itakuja kulia isipoutilia mkoa wa Tanga maanani kwa kuamini CUF ndio imakubalika.CUF haina investment yoyote ya maana ya kisiasa mkoa wa Tanga.Matokeo ya 2010 sio kipimo kizuri kuuweka mkoa wa Tanga rehani.
 
Watu wa Tanga wenyewe wanahitaji kuhamasika na kubadilika. Kwa kifupi watu wa Tanga ni wagumu mno kusoma alama za nyakati na kukubali mabadiliko. Wamekuwa watu wazito na watu wa kufanya mambo kimazoea sana kuliko kwa kupima. Wao huchagua chama tu ( CCM) badala ya sera (hata kama mtu ni mgombea wa chama kingine. Wameikubali hali ya kuwa mawakala CCM kwa miaka nenda rudi hata kama haijawafanyia chochote cha maana.

Nakumbuka CHADEMA (M4C Operation) ilipita kila wilaya lakini watu bado hawajabadilika. Naona Walau baadhi za kata katika wilaya za Tanga mjini, Mkinga kidogo na Pangani kidogo CUF imeanza kukubalika, lakini bado kuna safari ndefu na haja kwa upinzani kuendelea kumwaga dozi.
 
Mikoa mingi ya pwani, ni shidaaaa!! kiuchumi wako hoi kweli lakini bado wanathamini magamba! !utawasaidiaje watu wenye akili za kushikiwa!! yaaani kama mkoa wa pwani hadi una wahurumia lakini wamo tu, ZAMU HII TUNAKWENDA NA WALE WANAOJITAMBUA NA KUKAMATA FULSA NA KWENDA ZETU, MAPOPOMPO TUNAYAACHA.

Wewe huijui Tanga vizuri.
Tanga imegawanyika katika maeneo makuu matatu:

1.Majimbo ya Pwani
Tanga,Pangani na Mkinga.
Haya ni majimbo ya pwani na ambayo mila na desturi zao ni tofauti na maeneo mengine ya Tanga.Moja ya kabila la maeneo haya ni wadigo ambao kiasili ni watu wa Mombasa.Hawa sio rahisi kukubalina na siasa za itikadi ya CHADEMA,
Sanasana CUF. CHADEMA haina chao huko.

2.Bondei Land
Jimbo la Muheza limejaa wabondei ambao tabia zao kwa kiasi kidogo zinaendana na maisha ya watu wa pwani.Hawa ni wazito kuelewa ila kukifanyika uwekezaji mkunwa wa kisiasa ni rahisi kuelewa kuliko wadigo.

3.Zigua Land
Jimbo la Handeni na Kilindi limapatikana maeneo haya.Watu hawa wana tabia tofauti na wadigo ila wanaendana na wabondei na wasambaa.Tabia zao haziendani ma wati wa pwani.Hawa wanabadilika kukiwa na uwekezani wa kisiasa unaoeleweka.

4.Sambaa Land
Majimbo ya Korogwe Mjini,Korogwe Vijijini,Bumbuli,Lushoto na Mlalo yako kwenye eneo hili.Hili ni linapaswa kuwa haswa strategic area ya CHADEMA,huku mabadiliko yanapatikana CHADEMA ikijipanga.CUF kwenye maeneo haya unakufa kwa kasi wakati CHADEMA imejisahau.
 
Wagumu sana kuelewa hao watanga, ngoja cuf wahusike nao kwanza! Tupo busy na kanda ya ziwa!
Tehetehetehetehe! Ka wavaa balaghashia chadema hawawezi kufurukuta. Wao ni kwa wavaa rozali tu
 
Watu wa Tanga wenyewe wanahitaji kuhamasika na kubadilika. Kwa kifupi watu wa Tanga ni wagumu mno kusoma alama za nyakati na kukubali mabadiliko. Wamekuwa watu wazito na watu wa kufanya mambo kimazoea sana kuliko kwa kupima. Wao huchagua chama tu ( CCM) badala ya sera (hata kama mtu ni mgombea wa chama kingine. Wameikubali hali ya kuwa mawakala CCM kwa miaka nenda rudi hata kama haijawafanyia chochote cha maana.

Nakumbuka CHADEMA (M4C Operation) ilipita kila wilaya lakini watu bado hawajabadilika. Naona Walau baadhi za kata katika wilaya za Tanga mjini, Mkinga kidogo na Pangani kidogo CUF imeanza kukubalika, lakini bado kuna safari ndefu na haja kwa upinzani kuendelea kumwaga dozi.

Hakuna uwekezaji wa maana wa chama mkoa wa Tanga,watu wababadilika wakielimishwa...ndio maana trend ya upinzani imekuwa kutoka 2005 hadi 2014.

Kama unakumbuka 2007 CHADEMA uliwekeza sana Kanda ya Ziwa kupitia operesheni Sangara na wasukuma wakabadilika...hata wasambaa wanaweza kubadilika jitihada zikifanyika.
 
Tatizo UKAWA cdm tu ndio wanapiga kazi hao wengine wanaosha sura tu
 
Wewe huijui Tanga vizuri.
Tanga imegawanyika katika maeneo makuu matatu:

1.Majimbo ya Pwani
Tanga,Pangani na Mkinga.
Haya ni majimbo ya pwani na ambayo mila na desturi zao ni tofauti na maeneo mengine ya Tanga.Moja ya kabila la maeneo haya ni wadigo ambao kiasili ni watu wa Mombasa.Hawa sio rahisi kukubalina na siasa za itikadi ya CHADEMA,
Sanasana CUF. CHADEMA haina chao huko.

2.Bondei Land
Jimbo la Muheza limejaa wabondei ambao tabia zao kwa kiasi kidogo zinaendana na maisha ya watu wa pwani.Hawa ni wazito kuelewa ila kukifanyika uwekezaji mkunwa wa kisiasa ni rahisi kuelewa kuliko wadigo.

3.Zigua Land
Jimbo la Handeni na Kilindi limapatikana maeneo haya.Watu hawa wana tabia tofauti na wadigo ila wanaendana na wabondei na wasambaa.Tabia zao haziendani ma wati wa pwani.Hawa wanabadilika kukiwa na uwekezani wa kisiasa unaoeleweka.

4.Sambaa Land
Majimbo ya Korogwe Mjini,Korogwe Vijijini,Bumbuli,Lushoto na Mlalo yako kwenye eneo hili.Hili ni linapaswa kuwa haswa strategic area ya CHADEMA,huku mabadiliko yanapatikana CHADEMA ikijipanga.CUF kwenye maeneo haya unakufa kwa kasi wakati CHADEMA imejisahau.
Hakuna asiyejua watu wa Tanga bwana, ndio maana kwenye siasa huwezi kung'ang'ania nchi nzima ukubalike, we unachagua sehemu ambazo wanakuelewa na nguvu nyingi unawekeza huko.Hata kwa Mungu kuna wengine watabaki nyuma. Wangekuwa ni watu walio makini na wanaojitambua ingekuwa ngome kubwa ya CUF, kwani ni karibu na zanzibar kwa wenzao. Lakini bado asilimia kubwa ni ccm!!
 
Tehetehetehetehe! Ka wavaa balaghashia chadema hawawezi kufurukuta. Wao ni kwa wavaa rozali tu

Naona nowdays ritz yupo chama chake, hamy-d chake, laki si pesa chake, nawe chake kuna nn lizaboni?
 
Asante mleta mada kwa uchambuzi Safi na baadhi ya wachangiaji, ukawa inabidi kufanya feasibility study ya nguvu, na 60% ya majimbo inabidi ipewe CUF kutokana na asili, mila na desturi. Ukawa iunganishe nguvu kufanya uhamasishaji wa pamoja. Viongozi acheni kulala muda umeisha! Mpaka sasaiv ilitakiwa kuwe na time table ya kueleweka. Viongozi mnaopita humu chukulieni haya mambo serious mkayafanyie kazi!
 
CUF inakubalika maeneo ya pembezoni mwa bahari ya hindi,majimbo ya: Tanga,Pangani na Mkinga.

Inakubalika kidogo Muheza na Handeni.Kuanzia Korogwe mpaka Lushoto CUF haina nguvu.Jimbo la Lushoto walipata diwani kata moja kwa bahati nasibu kutokana na mgogoro wa kura za maoni za CCM 2010 ndio maana serikali za mitaa wakambulia 0.0% kwenye kata hiyo.

CUF haina madhara kwa CCM kuanzia Korogwe mpaka Lushoto.Ti
e will will tell.
 
Mikoa mingi ya pwani, ni shidaaaa!! kiuchumi wako hoi kweli lakini bado wanathamini magamba! !utawasaidiaje watu wenye akili za kushikiwa!! yaaani kama mkoa wa pwani hadi una wahurumia lakini wamo tu, ZAMU HII TUNAKWENDA NA WALE WANAOJITAMBUA NA KUKAMATA FULSA NA KWENDA ZETU, MAPOPOMPO TUNAYAACHA.

Kwa style hii ya nyodo na dharau ndio mtachukua nchi?
 
Watasingizia wameibiwa kura na kulaumu kila kitu kura zisipotosha.

Wewe nenda katatue kwanza gogoro ndani ya uvccm,kwani mwenyekiti wa chama chenu anasema muwache kuwa makuwadi.
 
Tehetehetehetehe! Ka wavaa balaghashia chadema hawawezi kufurukuta. Wao ni kwa wavaa rozali tu
Lizaboni rudi lumumba ukaweke mambo sawa kwani wale wagumu wanakuhitaji kukuhoji ni kwanini unakuwa ktk upande mmoja?
 
Back
Top Bottom