CHADEMA kidedea kijiji cha Kabiga Geita

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,599
3,220
GreatThinkers, Good news

Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwafahamisheni ya kuwa CHADEMA imeshinda ktk uchaguzi wa Serikali ya kijiji cha KABIGA kata ya KAKOLA Jimbo la Nyang’wale wilaya ya Geita.
Aliyekuwa Mwenyekiti ( CCM) aliamua kugombea Udiwani akashinda ikabidi ajivue Gamba moja, akautema Uenyekiti.
Mara ya kwanza walitangaza Uchaguzi walipogundua kuwa dalili za kushindwa ni kubwa Gafla uchaguzi uliahirishwa.
Wakajaribu kuweka Mambo sawa wakizani watarubuni wananchi matokeo yake CDM imepata kura 568 wakati CCM wameambulia 453.

Peoples……………………Power!
 
Good to go..kama tumeanza at that level then 2015 itakuwa mbaya kwa ccm..mwanzon ilikuwa ni mjin bt tumeanza kukamata mashina..
 
Bagayomba, isee basukuma dole bhaa ndhoo tahabu. Ng'wabona. Likonja elingi. Roma rocuta ausa filta.
 
ni njema,tushaur viongoz kitaifa CDM waongeze juhud shinan ili kujenga nguvu zaid ya CDM.Kwan hata ZNZ wanasubir ukomboz huo kwan wameelewa faida ya mandamano,pana wananch toka huko alimshukuru sana Lisu na alimwambia wao hawana elimu kupitia maandamano ya CDM wanapata uelewa wa mambo mbalmbal.TUONGEZE JUHUD TUTAUSHINDA USANII ULOPO TZ
 
haya hayaaaaaaaaaaaaa!!!!!! wanasema hata mbuyu ulianza kama mchicha...kwa hiyo wakinza na wenyeviti si mbaya...
 
watu wamegutuka wanataka kusilimishwa.

Sasa hayo ya kusilimishwa yametokea wapi tena? Mbona kila issue tunai-deflect kwenye udini? Halafu kina FaizaFoxy na Malaria sugu wakijibu tunawaona ndo wenye matatizo.Huu ni uchokozi wa wazi wazi.
 
Kaaazi kweli kweli!! Teh teh magamba bwana watajivua mpaka ngozi.
Mkuu tujuze jina la huyo mteule.
 
Sasa hayo ya kusilimishwa yametokea wapi tena? Mbona kila issue tunai-deflect kwenye udini? Halafu kina FaizaFoxy na Malaria sugu wakijibu tunawaona ndo wenye matatizo.Huu ni uchokozi wa wazi wazi.
Labda anamaanisha kusilimu Chama... Wataalam wa kiswahili watusaidi tujue kusilimu ni dini tu au hata chama? Unajua ukipata ujasiri wa kuhama lichama lihovu kama lile la magamba si ni sawa na kusilimu kabisa.
All in all watu wa Geita mko vizuri, napafahamu pale katoro kuna mwaka nilipita.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka kidedea ktk Uchaguzi wa serikali ya kijiji uliofanyiaka tarehe 19/6/2011 katika kijiji cha KABIGA kata ya KAKOLA Wilaya mpya ya NYANG'WALE Mkoani Geita.
Katibu Mwenezi CHADEMA Geita na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Ignas Karashani alisema kwamba waliibwaga CCM kwa tofauti ya Kura 115 ambapo CHADEMA ilipata kura 568 na CCM ikiambulia kura 453 na kufanya Ndugu Deus Charles mgombea wa CHADEMA kuibuka kidedea. Uchaguzi huo uliitishwa baada ya aliyekuwa Mwenyekiti kujiuzulu baada ya kushinda kiti cha Udiwani katika uchaguzi uliofanyika Octoba mwaka jana.
Hata hivyo uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rush
wa huku chama cha mapinduzi CCM kikiwarubuni wapiga kura kwa kugawa chumvi na pesa ambapo CHADEMA ilifanikiwa kupambana na hujuma hizo kwa kuripoti polisi na watuhumiwa kukamatwa kwa kosa hilo.
 
Back
Top Bottom