Chadema kesho ndio matokeo ya vipimo, Mko tayari kuupokea ukweli?

Chadema kesho ndio matokeo ya vipimo, Mko tayari kuupokea ukweli?

Chris Lukosi

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
4,583
Reaction score
2,948
Ndugu zanguni,

Kama mjuavyo, kesho ndio uchaguzi wa madiwani sehemu mbali mbali nchini, sote tunajua CCM watafunika viti vyote Mbeya na sehemu nyinginezo. Lakini kuna sehemu moja tu ambayo nina uhakika matokeo yakitoka makamanda wanaweza kuzimia.

Nimefuatilia kampeni na mikutrano ya Mheshimiwa Mwigulu Nchemba na Nape na nimewaonea huruma sana makamanda kwani wameonyeshwa tofauti kati ya Chuma na plastiki.

Nawaomba watu wa msalaba mwekundu wawe standby kesho kuhakikisha wanawasaidia makamanda watakaozidiwa baada ya vipimo kutoka kwa daktari ambaye ni sanduku la kupigia kura.

CCM ushindi ni uhakika kesho 16/03/2013

JITAMBUE!
7158_500388936681602_606438292_n.jpg
 
Jifariji sana, nimepita hapa kaloleni kwa cheusi nimewaonea huruma sana CCM,
 
Pia na kipimo kizuri kwa ccm kujua watu wamewachoka .Kama wasipoiba kura ccm wataibika na wajue kuwa wananchi wanazidi kuwachukia hasa wanapoendeleza siasa zao za ubabe, utekaji na kutesa wafuasi wa upinzani
 
Jifariji sana, nimepita hapa kaloleni kwa cheusi nimewaonea huruma sana CCM,
Tusubiri Kesho.
Mimi tayari nimeishaandaa debe zima la ulanzi kwa ajili ya kusherehekea ushindi
 
Chilisosi thread zako huwa zinaboa sana maana huna chakuandika zaidi ya chafema.ukilala ukiamka ni chadema...unakuwa kama mwanaume aliyepigwa kibuti na demu wakati bado anampenda huwa haishi kumsema vibaya na kumponda.basi na wewe bado unaipenda chadema hata ukilala unaota makamanda.badilika deal na magamba yako achana na chadema.
 
Eti ndugu zanguni nani anaundugu na wewe?
 
Kwanini utangulize kama hawataiba kura?Ina maana CDM haijajipanga kwa njama za kuibiwa kura?Kwanini kila siku tuwe tunalalamika kuibiwa kura?Tujipange.Usiku mkilala huko mtaliwa.Kumbukeni hata CCM ingependa ishinde Arusha ili ipate Amani sana.bora ikashindwa kwingine kote lakini ikashinda Arusha.Kinyume chake pia kwa CDM.
 
Wewe upo mitaa ya South London sijui East halafu unashadidia ya Arusha.Subiri kesho kama umejipanga kupokea matokeo pia
Mkuu najua kuwa Arusha ndio backyard ya Chadema lakini tunawatoa kamasi kesho believe me!
 
Back
Top Bottom