CHADEMA Kasulu watimuana

Soma katiba ya Chadema ibara ya 7.4.10 (r) na (u) utapata majibu kamili. Kifungu hiki kinahusu kazi za kamati tendaji ya jimbo au wilaya.
 
Alhaji Kasisiko hapaswi kukikwepa kikombe. japo kwa sasa lazima atalipa fadhira kwa kijana wake kutokana na ufadhiri aliokuwa anaupata, akiachwa atashindwa kufanya maamuzi kwa mujibu wa katiba.

Ni "fadhila na "ufadili" na siyo fadhi(ra)a na fadhi(ri). Naomba usahihishe hilo next time unapoandika. Ni ushauri tu wa kukuongezea credibility ili uvute shavu hapo nafasi ya Zitto! :)
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilayani Kasulu mkoani Kigoma kimewavua nyadhifa viongozi wake watatu wa jimbo la Kasulu mjini kwa tuhuma za kuhujumu mkutano wa Katibu mkuu chama hicho Dr Wilbroad Slaa katia ziara yake mkoani humo

Mwenyekiti wa Chadema wilayani Kasulu Bw Rajabu Bujoro ameiambia Redio Kwizera kuwa maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha kamati ya ushauri ya chama hicho baada ya kubaini kuwa viongozi hao walichochea vurugu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kiganamo December 8 mwaka huu.

Amewataja waliovuliwa madaraka kuwa ni Bw Lukas Gervas aliyekuwa katibu, Bw Joshua Kaijage aliyekuwa katibu mwenezi pamoja na Masoud Bigangika aliyekuwa mratibu wa vijana wote kutoka jimbo la Kasulu mjini na kwamba watapewa siku 14 ili wajieleze na wakishindwa watavuliwa uanachama

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chadema Mkoani Kigoma Alhaji Jafar Kasisiko amesema kuwa maamuzi hayo yanakiuka Katiba ya Chama hicho kwa kuwa wilaya haina mamlaka ya kinidhamu kwa viongozi wa Jimbo isipokuwa baraza la Mkoa

Gogoro lingine hilooooo! Matokeo ya ziara ya Dr. Slaa huko Kigoma.
 
Alhaji Kasisiko hapaswi kukikwepa kikombe. japo kwa sasa lazima atalipa fadhira kwa kijana wake kutokana na ufadhiri aliokuwa anaupata, akiachwa atashindwa kufanya maamuzi kwa mujibu wa katiba.
Mtoi bila shaka hili zimwi ambalo limemchanganya Slaa akaamua kuja na ahadi ya kuhalalisha Gongo.
 
Karama!..????sasa karama inakuwaje kwa taarifa,iwe ni habari ya kweli ama ya uongo .

Utajiuliza sana. Lakin siku zote Mola yu pamoja na watenda haki na wakweli na abadan hawezi kuwa na wanafiki.

sasa hapo uatapata pumba na mchele.

Pole sana
 
ismael, kasulu kuna matatizo ya uongozi. Kambi ya bujoro inapenda madaraka na vivyo hivyo ata hawa akina masud ni wapenda misifa. Mgogoro ulikuwepo na ilionekana waliuzika. Kilichokuza mgogoro huu kwa nguvu ni pale ilipotolewa ratiba ya ujio wa dr slaa. Kambi ya bujoro ilisapoti dr slaa aje huku akina masud, kaijage na luka hawakutaka dr slaa aje. Awa walijiapiza kuwa ni zito damu. Hujuma zilifanywa na vijana wa ccm lakini masud & co walikuwa na mkono wao. Waliitwa kwenye kikao cha maandalizi wakagoma isipokuwa kaijage. Kilichofanyika akina masud wanakijua. Je ujio wa zito kesho si wapepanga bila kuhusisha watu wengine. Siku ya ujio wa dr slaa ata zitto alikuwa na mkono wake kwa vurugu zilizotokea Waliondaa hizi vurugu si wahuni kwamba hawakuandaliwa, bali masud and co waliandaa huu upuuzi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom