CHADEMA Kasulu watimuana

Mabunu

Member
Oct 17, 2012
33
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilayani Kasulu mkoani Kigoma kimewavua nyadhifa viongozi wake watatu wa jimbo la Kasulu mjini kwa tuhuma za kuhujumu mkutano wa Katibu mkuu chama hicho Dr Wilbroad Slaa katia ziara yake mkoani humo

Mwenyekiti wa Chadema wilayani Kasulu Bw Rajabu Bujoro ameiambia Redio Kwizera kuwa maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha kamati ya ushauri ya chama hicho baada ya kubaini kuwa viongozi hao walichochea vurugu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kiganamo December 8 mwaka huu.

Amewataja waliovuliwa madaraka kuwa ni Bw Lukas Gervas aliyekuwa katibu, Bw Joshua Kaijage aliyekuwa katibu mwenezi pamoja na Masoud Bigangika aliyekuwa mratibu wa vijana wote kutoka jimbo la Kasulu mjini na kwamba watapewa siku 14 ili wajieleze na wakishindwa watavuliwa uanachama

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chadema Mkoani Kigoma Alhaji Jafar Kasisiko amesema kuwa maamuzi hayo yanakiuka Katiba ya Chama hicho kwa kuwa wilaya haina mamlaka ya kinidhamu kwa viongozi wa Jimbo isipokuwa baraza la Mkoa
 
mchaichai

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
648
0
maamuzi sahihi kabisa hayo safi sana viongozi makini hufanya maamuzi makini kama hayo mungu awabariki
 
MUMBATI

Member
Dec 10, 2013
7
0
Hata Kasisiko naye anatakiwa kuwajibishwa maana ni yeye aliyetoa tahadhari kuwa Dr Slaa asikanyage Kigoma hivyo kwa kauli hiyo na yeye alichochea vurugu zile!!
 
Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
0
karama za Zito hizo. Siku zote haki inasimama na uongo, unafiki unatoweka.

tuvute tu subra tuone mengi.
 
Pagija

JF-Expert Member
Dec 6, 2013
380
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilayani Kasulu mkoani Kigoma kimewavua nyadhifa viongozi wake watatu wa jimbo la Kasulu mjini kwa tuhuma za kuhujumu mkutano wa Katibu mkuu chama hicho Dr Wilbroad Slaa katia ziara yake mkoani humo

Mwenyekiti wa Chadema wilayani Kasulu Bw Rajabu Bujoro ameiambia Redio Kwizera kuwa maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha kamati ya ushauri ya chama hicho baada ya kubaini kuwa viongozi hao walichochea vurugu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kiganamo December 8 mwaka huu.

Amewataja waliovuliwa madaraka kuwa ni Bw Lukas Gervas aliyekuwa katibu, Bw Joshua Kaijage aliyekuwa katibu mwenezi pamoja na Masoud Bigangika aliyekuwa mratibu wa vijana wote kutoka jimbo la Kasulu mjini na kwamba watapewa siku 14 ili wajieleze na wakishindwa watavuliwa uanachama

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chadema Mkoani Kigoma Alhaji Jafar Kasisiko amesema kuwa maamuzi hayo yanakiuka Katiba ya Chama hicho kwa kuwa wilaya haina mamlaka ya kinidhamu kwa viongozi wa Jimbo isipokuwa baraza la Mkoa
Khaa Slaa alituabia waliovuruga mikutano yake ni CCM.....ama kweli ongo na ukweli sio marafiki. Dah kumbe hata wilayani wanachakachuwa katiba hii ni hatareeeeeeeeeee!!
 
Pagija

JF-Expert Member
Dec 6, 2013
380
0
Sasa huyo Mwenyekiti anapingana na maazimio ya Wilaya kwa maslahi ya nani?
Mkuu mwenyeiti anasema katiba imekiukwa.........labda tujiulize pia maazimio ya kamati ya wilaya inakiuka katiba kwa maagizo na maslahi ya nani?
 
ISMAIL MKIMBIZI

Senior Member
Jan 13, 2013
192
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilayani Kasulu mkoani Kigoma kimewavua nyadhifa viongozi wake watatu wa jimbo la Kasulu mjini kwa tuhuma za kuhujumu mkutano wa Katibu mkuu chama hicho Dr Wilbroad Slaa katia ziara yake mkoani humo

Mwenyekiti wa Chadema wilayani Kasulu Bw Rajabu Bujoro ameiambia Redio Kwizera kuwa maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha kamati ya ushauri ya chama hicho baada ya kubaini kuwa viongozi hao walichochea vurugu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kiganamo December 8 mwaka huu.

Amewataja waliovuliwa madaraka kuwa ni Bw Lukas Gervas aliyekuwa katibu, Bw Joshua Kaijage aliyekuwa katibu mwenezi pamoja na Masoud Bigangika aliyekuwa mratibu wa vijana wote kutoka jimbo la Kasulu mjini na kwamba watapewa siku 14 ili wajieleze na wakishindwa watavuliwa uanachama

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chadema Mkoani Kigoma Alhaji Jafar Kasisiko amesema kuwa maamuzi hayo yanakiuka Katiba ya Chama hicho kwa kuwa wilaya haina mamlaka ya kinidhamu kwa viongozi wa Jimbo isipokuwa baraza la Mkoa

Nimekuwa na muda mrefu nikifuatilia siasa za Kasulu vyama mbalimbali ikiwemo CHADEMA sioni kuwa sababu hiyo ya kuwaadhibu kuwa ni ya kweli. Ingekuwa ya kweli haipaswi kuvuliwa madaraka tu, bali kukuwafukuza chamani kabisaaa! Nijuavyo mimi kumekuwa na migogoro ya kiuongozi na maadili CHADEMA KASULU jambo lililowahi kutoa taswira kama hii hii viongozi wa Jimbo Wakasimamishwa na uongozi wa wilaya Kasulu.

Hali hii iliendelea kuwa sumu kwani mwenyekiti wa CHADEMA wilaya Bw. Rajabu Bujoro na Katibu wake Bw. Kwasakwasa walijiimarisha na kuzalisha makundi chamani. Hii ilisababisha shughuli za kichama za Jimbo viongozi wa Wilaya wanasusa na za wilaya Jimbo wanasusa ikawepo taswira ya kama CHADEMA ni mbili hapa Kasulu au ni vyama viwili tofauti.

Kifupi ni kwamba hawana maelewano ya mda mrefu, hivyo vurugu zilizotokea wakati Dr Slaa akiwa Kasulu Mjini sio kweli kuwa wao ndio walioziratibu. Haiingii akilini mfano Mratibu wa Vijana Jimboni Bw. Masoud Bigangika aratibu vurugu hizo harafu wahusika wa vurugu waonekane ni wanaccm na familia za wazee wa ccm wasiwe vijana wanaoongozwa na viongozi wa jimbo yaani wasiwe wanachama wa CHADEMA.

Picha mbalimbali zikiwemo za video zinawaonesha familia ya Mzingwa na jamaa za Mzee Juma Ulimwengu wazee wa CCM zikiongoza vurugu hizo. Masoud, Kaijage na Lucas hawana uwezo wa kuingilia vijana wa CCM na kuwashawishi ni vurugu zilizoratibiwa na CCM tuwe makini na CCM na hatari kwa CHADEMA ndiyo maana wahusika wakuu kuwashughulikia kuwatoa POLISI waliokamatwa kuhusiana na vurugu hizo walikuwa viongozi wa CCM.

Hainiingii akilini vijana wa CHADEMA waratibu na kufanya Vurugu viongozi wa CCM waingilie kati kuwasaidia. Ndoa imebarikiwa kanisani baadaye wanandoa wamegombana eti shehe awapeleke msikitini kuwasuluhisha hainingii akilini.

Niaminivyo mimi kama ilivyo katika vyama vyote vya siasa Tanzania, kumekuwepo na kuminya demokrasia na ukiwa na mawazo tofauti unaitwa msaliti na wale wenye kushika mpini wanakuadhibu. Jambo hili ndilo chanzo cha makundi vyamani, na kwa wale wanaoonesha msimamo wao kumtetea ZITTO wanatungiwa kila aina ya uongo ukichanganya na ukweli kuwa wanapingana na maamuzi ya Kamati Kuu CHADEMA kumuondoa ZITTO lazima wafukuzwe kwa uongo na ukweli.
 
bujash

JF-Expert Member
Aug 9, 2013
3,468
0
Khaa Slaa alituabia waliovuruga mikutano yake ni CCM.....ama kweli ongo na ukweli sio marafiki. Dah kumbe hata wilayani wanachakachuwa katiba hii ni hatareeeeeeeeeee!!

kwa hiyo ulivyoambiwa waliovuruga ni ccm basi inatosha kusadiki kuwa hakuna wanacdm walioshirikiana na ccm kuhujumu ziara?
 
Dec 11, 2010
3,322
0
Hata Kasisiko naye anatakiwa kuwajibishwa maana ni yeye aliyetoa tahadhari kuwa Dr Slaa asikanyage Kigoma hivyo kwa kauli hiyo na yeye alichochea vurugu zile!!

Alhaji Kasisiko hapaswi kukikwepa kikombe. japo kwa sasa lazima atalipa fadhira kwa kijana wake kutokana na ufadhiri aliokuwa anaupata, akiachwa atashindwa kufanya maamuzi kwa mujibu wa katiba.
 
Mkya

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
667
0
CHADEMA haipo kigoma ipo moshi hao watulie tuuu waache ujinga wao
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom