CHADEMA jahazi lilopoteza muelekeo!

CHADEMA jahazi lilopoteza muelekeo!

Chadema jahazi lilipoteza muelekeo lakini wakati huo huo mnaihofia aibu ya kupotea kwenye anga za siasa nchini kwa kufanya uchaguzi huru na wa haki kupitia Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya ya rasimu ya Warioba.

Sasa inakuwaje chama kilichoimarika kinakihofia chama mfu kilichopoteza muelekeo!? Tafakari kwa kina acha kukurupuka.

CHADEMA baada ya kushindwa uchaguzi ilijaribu kuja na mbinu nyingi za kuzima yale mengi mema yafanywayo na serikali, baada ya kuona kila sehemu wamepuuzwa kwa kua hakuna jipya CHADEMA wakamua kuja na mbinu mpya ya kufanya biashara na baadhi ya media.

Ili kumzima rais pindi anapofanya matukio yake ya kizalendo nao ghafla huamua kufanya matukio yao na mengine yameelekea kugharimu maisha yao na kwa kua wameshafanya biashara na baadhi ya media na wanataka kumfunika rais na kutaka habari zao ziwe kurasa za mbele na kuandikwa sana hawajali

Hii ni mifano tu

1.Rais anapokea report ya kwanza ya makinikia ,wakaja na habari ya bomberdia imekamatwa

2.Rais anapokea report ya pili, mwanasheria wao anapigwa risasi

3.Rais anawapa vyeti wakaja na habari mwanasheria wao amewasalimia watanzania

4.Rais anafanya uteuzi wa watendaji wa serikali,nyalandu atangaza kuondoka

5,Rais alipokua mwanza kwenye shughuli za funguzi mbalimbali wakaja na taarifa mwanasheria kafanya kampeni live za udiwani

6.Rais yupo bukoba akiwatumbua wakurugenzi,wao wamekuja na nyalandu akutana na lowassa na mengineo mengi tukiyaandika yote itakua balaa.

Yote inaonyesha ni jinsi gani chama hakina maono tena na muelekeo na wanajaribu kushirikiana na baadhi ya vyombo vya habari kwa kutoyapa umuhimu matukio ya maendeleo afanyayo rais.

Angalizo CHADEMA ipo siku mtatangaza chairman au Lowassa amefariki ili kupata front page, maana kila wanalofanya huwa wanajisifu kesho tunatabiri habari hii itamfunika rais

Kifupi rais ana mengi ya maendeleo na yatabaki kumbukumbu ila CHADEMA mtawatajirisha wenye media, kama mlivyomtajirisha kubenea na habari za ufisadi wa Lowassa, rais atapimwa kwenye boksi la kura lakini si kununua media!
 
Chadema jahazi lilipoteza muelekeo lakini wakati huo huo mnaihofia aibu ya kupotea kwenye anga za siasa nchini kwa kufanya uchaguzi huru na wa haki kupitia Tume huru ya uchaguzi na katiba mpya ya rasimu ya Warioba.

Sasa inakuwaje chama kilichoimarika kinakihofia chama mfu kilichopoteza muelekeo!? Tafakari kwa kina acha kukurupuka.
La tume huru na katiba isiokidhi mmeona leo njia sahihi nendeni mahakamani au gomeni kuingia kwenye uchaguzi pigeni kura zitoshe acheni blah blah!
 
Nchi imeshamshinda huyo uchwara sasa kabaki anahaha na sera MUFILISI za kugawa rushwa ya pesa na vyeo eti anaimarisha chama!!! Na mazuzu mnashangilia!!!

Vita ni akili ametumia mbinu ya kichura chura mapigo ya mwisho mmelegea kila kiungo kocho kocho!
 
Yaaani unashindwa kuelewa alieandika kama ana akili timamu au la
mkuu nchi kwani watu wana akili waliiwaita watu majina yote mabaya ghafla wamehamia kwao , mpaka leo hii bado wanapambana kuwasafisha tu!
 
Unahitaji watu waige nini kwa cancer ya taifa!
Unamaanisha ccm sio? Kwa east Africa ndio cancer pekee inayosurvive lakini muda wake wa kuchomwa mionzi aina ya mugabe umewadia. Muda umeisha hujajenga kiwanda hata cha ugolo na bado utataka kura za hawa wanaozurura na mazao waliyolima mitaani kutafuta masoko! Hangaikeni na kusajili wachezaji wa upande wa pili mkiamini wana mbinu za ushindi wakati walishashindwa huko kwenu!
 
unaweweseka na mapigo!
 
Na wewe mwandishi una maono gani? Kwahiyo upande A au B ni nani alikuwa mpanga matukio??
 
Bado naamin CDM wako imara pamoja na kuzongwa na nguvu ya dola
 
Yepi mliyonayo? Au hayo ya kununua? Ni kawaida ya midomo zege isiyojua kushawishi kutanguliza pesa ili yakubaliwe! Oneni aibu na nunueni na viwanda basi!
Kama mnaweza kununulika kirahisi ni dhahiri uwezo wa kuongoza nchi bado,mtaweza kuikataa rushwa na kuipiga vita!
 
Back
Top Bottom