CHADEMA jahazi lilopoteza muelekeo!

CHADEMA jahazi lilopoteza muelekeo!

Okey, Chadema ni jahazi lililopoteza muelekeo. Swali langu ni; kwanin serikari inahangaika na inatumia nguvu kupambana na jahazi lililopoteza muelekeo? Kwanin msiachane nalo ili lipoteze muelekeo vzuri? Naomba unijibu kwa hoja yenye mantiki
 
Chadema ilisha ondoka na Dr slaa.chadema yasasa ya muunganiko wa Lema, Msigwa , DJ na ma mvi ndio iwe inaongoza upinzani!! Upinzani hakuna tena. Kilasiku wanasajili mijizi tu.
Hata kipindi cha dr slaa mlisema chadema aliondokanayo juliana shonza uwongo??
 
Kweli mkuu, toka Dr Slaa ameondoka chadema imebadilika sana.
*Wameacha kuhoji kwa kutumia sera sasa ni mwendo wa matukio tu.
*Ujengaji wa hoja umeisha, sasa kelele za [HASHTAG]#lissumsaliti[/HASHTAG] ndo zinaongoza chama.
*Reasoning capacity imeshuka, sasa hivi ni mwendo wa matusi tu (angalia hapa jf).
*Hakuna kipya chochote zaidi ya kelele zile zile za siku zote.
*Ugomvi ndani ya chama: Lowassa camp vs [HASHTAG]#lissumsaliti[/HASHTAG] camp (macho yote 2020).
Too bad, hata kuiunga mkono chadema inabidi kujiuliza mara mbili mbili.
 
2020 mbali huko angalia uchaguzi mdogo tu wa madiwani.
e21dd31760af5d197460b87d5b0b7c4c.jpg
Haina tofauti na takwimu za kupikwa tuliona hizo picha 2015 na mlisema mmeibiwa!
 
Okey, Chadema ni jahazi lililopoteza muelekeo. Swali langu ni; kwanin serikari inahangaika na inatumia nguvu kupambana na jahazi lililopoteza muelekeo? Kwanin msiachane nalo ili lipoteze muelekeo vzuri? Naomba unijibu kwa hoja yenye mantiki
Serikali inapambana kwa nguvu kumkwamua mwananchi wake ili kumpatia elimu,kumtafutia madawa kwa ajili ya afya na kumletea maendeleo katika nyanja mbalimbali serikali haiwezi kupoteza muda kukaa na kujadili chadema isipokua chadema ndio inatumia nguvu kutaka kuikwamisha serikali!
 
Ki ukweli CDM sasa inapumulia mrija.
Nimefanya tathmini ya haraka haraka, nimekuta kila uchao CDM inazidi kurudi kwa speed ya ajabu.
 
Kitendo cha kuamua tu kuandika habari zinazoihusu CDM, inaonyesha ni jinsi gani CHADEMA inavyozidi kuimarika kwenye mioyo ya Watanzania wengi.
Mleta maada ckutegemea kabisa wewe kuandika habari znazoihusu cdm ila kwa thread yako hii ni dhahili kuwa Cdm inapendwa saaaaaaaana.
 
Ndio ndoto iliobaki kama ya lowassa kuingia ikulu!
 
CHADEMA ilianza rasmi Mei 28, 1992 chini ya Mwenyekiti wake Edwin Mtei mkazi wa Arusha. Katibu Mkuu wa Kwanza alikuwa Mzee Bob Makani, Msukuma wa Shinyanga. Makamu wa Mwenyekiti alikuwa Brown Ngwilupipi wa Mbeya; Katibu Mkuu Mwenezi wa kwanza alikuwa Edward Barongo kutoka Kagera.

Katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya siasa chama hiki kilisimamisha wagombea ubunge na udiwani tu katika maeneo machache; mgombea urais hakusimama. Chama kilipata wabunge wanne (4) kati ya 269 kwa wakati huo na Madiwani 42 tu nchi nzima!

Uchaguzi wa mwaka 2000 chama kiliongeza nafasi kadhaa; kilipata Wabunge watano (5) tu; Madiwani 75 na kuongoza halmashauri tatu za Kigoma, Karatu na Tarime.

Mwaka 2005, Mgombea Urais alikuwa Freeman Mbowe aliyevuna asilimia 5.88% ya kura zote akiwa mshindi wa tatu. Chama kilipata Wabunge 11 na Madiwani 103 na kiliongoza Halmashauri tatu ambazo ni Kigoma, Tarime na Karatu.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010, Mgombea Urais Dkt Slaa alipata kura asilimia 27.1% ya kura zote; Chama kilishinda nafasi kadhaa za ubunge na kupata jumla ya wabunge 48 na Madiwani 467; pia kiliongoza halmashauri saba (7).

Mwaka 2015, Mgombea Urais Edward Lowassa, alipewa na tume kura 6,072,848 ambazo ni sawa na asilimia 39.97%; chama kilipata jumla ya Wabunge wapatao sabini (70) na kuongoza Halmashauri zipatazo saba ikiwemo Jiji la Arusha, Jiji la Mbeya, Jiji la Dar es Salaam, Ubungo, Ilala nk.

Kwa taarifa hizo fupi, ni wazi tu kwamba CHADEMA ni chama ambacho kinazidi kukua pamoja na changamoto kadhaa ambazo chama hiki kinapitia.
 
Ni kweli kinakuwa kila mwaka, ila ili kikue zaidi kinahitaj kuwa na Sera makini hususani kukipeleka vijijin ambako baadhi ya wanakijiji bado wanasema Nyerere yupo
 
Mkuu ccm ilichokwa...na chadema haikujipanga...tegemea anguko kubwa sna la chadema kwenye uchaguzi wa mwaka 2020..
 
CHADEMA baada ya kushindwa uchaguzi ilijaribu kuja na mbinu nyingi za kuzima yale mengi mema yafanywayo na serikali, baada ya kuona kila sehemu wamepuuzwa kwa kua hakuna jipya CHADEMA wakamua kuja na mbinu mpya ya kufanya biashara na baadhi ya media.

Ili kumzima rais pindi anapofanya matukio yake ya kizalendo nao ghafla huamua kufanya matukio yao na mengine yameelekea kugharimu maisha yao na kwa kua wameshafanya biashara na baadhi ya media na wanataka kumfunika rais na kutaka habari zao ziwe kurasa za mbele na kuandikwa sana hawajali

Hii ni mifano tu

1.Rais anapokea report ya kwanza ya makinikia ,wakaja na habari ya bomberdia imekamatwa

2.Rais anapokea report ya pili, mwanasheria wao anapigwa risasi

3.Rais anawapa vyeti wakaja na habari mwanasheria wao amewasalimia watanzania

4.Rais anafanya uteuzi wa watendaji wa serikali,nyalandu atangaza kuondoka

5,Rais alipokua mwanza kwenye shughuli za funguzi mbalimbali wakaja na taarifa mwanasheria kafanya kampeni live za udiwani

6.Rais yupo bukoba akiwatumbua wakurugenzi,wao wamekuja na nyalandu akutana na lowassa na mengineo mengi tukiyaandika yote itakua balaa.

Yote inaonyesha ni jinsi gani chama hakina maono tena na muelekeo na wanajaribu kushirikiana na baadhi ya vyombo vya habari kwa kutoyapa umuhimu matukio ya maendeleo afanyayo rais.

Angalizo CHADEMA ipo siku mtatangaza chairman au Lowassa amefariki ili kupata front page, maana kila wanalofanya huwa wanajisifu kesho tunatabiri habari hii itamfunika rais

Kifupi rais ana mengi ya maendeleo na yatabaki kumbukumbu ila CHADEMA mtawatajirisha wenye media, kama mlivyomtajirisha kubenea na habari za ufisadi wa Lowassa, rais atapimwa kwenye boksi la kura lakini si kununua media!
Mku kimepoteza mwelekeo baada Katambi kuondoka sio
 
CHADEMA ilianza rasmi Mei 28, 1992 chini ya Mwenyekiti wake Edwin Mtei mkazi wa Arusha. Katibu Mkuu wa Kwanza alikuwa Mzee Bob Makani, Msukuma wa Shinyanga. Makamu wa Mwenyekiti alikuwa Brown Ngwilupipi wa Mbeya; Katibu Mkuu Mwenezi wa kwanza alikuwa Edward Barongo kutoka Kagera.

Katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya siasa chama hiki kilisimamisha wagombea ubunge na udiwani tu katika maeneo machache; mgombea urais hakusimama. Chama kilipata wabunge wanne (4) kati ya 269 kwa wakati huo na Madiwani 42 tu nchi nzima!

Uchaguzi wa mwaka 2000 chama kiliongeza nafasi kadhaa; kilipata Wabunge watano (5) tu; Madiwani 75 na kuongoza halmashauri tatu za Kigoma, Karatu na Tarime.

Mwaka 2005, Mgombea Urais alikuwa Freeman Mbowe aliyevuna asilimia 5.88% ya kura zote akiwa mshindi wa tatu. Chama kilipata Wabunge 11 na Madiwani 103 na kiliongoza Halmashauri tatu ambazo ni Kigoma, Tarime na Karatu.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010, Mgombea Urais Dkt Slaa alipata kura asilimia 27.1% ya kura zote; Chama kilishinda nafasi kadhaa za ubunge na kupata jumla ya wabunge 48 na Madiwani 467; pia kiliongoza halmashauri saba (7).

Mwaka 2015, Mgombea Urais Edward Lowassa, alipewa na tume kura 6,072,848 ambazo ni sawa na asilimia 39.97%; chama kilipata jumla ya Wabunge wapatao sabini (70) na kuongoza Halmashauri zipatazo saba ikiwemo Jiji la Arusha, Jiji la Mbeya, Jiji la Dar es Salaam, Ubungo, Ilala nk.

Kwa taarifa hizo fupi, ni wazi tu kwamba CHADEMA ni chama ambacho kinazidi kukua pamoja na changamoto kadhaa ambazo chama hiki kinapitia.
Hayo mafanikio kwa mwaka 2015 ilikua ni msingi imara na malengo yaliyoratibiwa na dr slaa!
 
Ni kweli kinakuwa kila mwaka, ila ili kikue zaidi kinahitaj kuwa na Sera makini hususani kukipeleka vijijin ambako baadhi ya wanakijiji bado wanasema Nyerere yupo

Unaendaje vijijini wakati dikteta amezuia mikutano? Unaelimishaje wakati mikutano wanafanya wao tu Ikulu mpaka katika hafla za kijeshi? Kuna haja kweli ya kuwekeza nguvu vijijini lakini kumbuka vyama vya upinzani vimezuiwa siasa wakati yeyey anafanyia siasa hadi ikulu utadhani ni chato kwake.
 
Back
Top Bottom