CHADEMA jahazi lilopoteza muelekeo!

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
14,108
15,972
CHADEMA baada ya kushindwa uchaguzi ilijaribu kuja na mbinu nyingi za kuzima yale mengi mema yafanywayo na serikali, baada ya kuona kila sehemu wamepuuzwa kwa kua hakuna jipya CHADEMA wakamua kuja na mbinu mpya ya kufanya biashara na baadhi ya media.

Ili kumzima rais pindi anapofanya matukio yake ya kizalendo nao ghafla huamua kufanya matukio yao na mengine yameelekea kugharimu maisha yao na kwa kua wameshafanya biashara na baadhi ya media na wanataka kumfunika rais na kutaka habari zao ziwe kurasa za mbele na kuandikwa sana hawajali

Hii ni mifano tu

1.Rais anapokea report ya kwanza ya makinikia ,wakaja na habari ya bomberdia imekamatwa

2.Rais anapokea report ya pili, mwanasheria wao anapigwa risasi

3.Rais anawapa vyeti wakaja na habari mwanasheria wao amewasalimia watanzania

4.Rais anafanya uteuzi wa watendaji wa serikali,nyalandu atangaza kuondoka

5,Rais alipokua mwanza kwenye shughuli za funguzi mbalimbali wakaja na taarifa mwanasheria kafanya kampeni live za udiwani

6.Rais yupo bukoba akiwatumbua wakurugenzi,wao wamekuja na nyalandu akutana na lowassa na mengineo mengi tukiyaandika yote itakua balaa.

Yote inaonyesha ni jinsi gani chama hakina maono tena na muelekeo na wanajaribu kushirikiana na baadhi ya vyombo vya habari kwa kutoyapa umuhimu matukio ya maendeleo afanyayo rais.

Angalizo CHADEMA ipo siku mtatangaza chairman au Lowassa amefariki ili kupata front page, maana kila wanalofanya huwa wanajisifu kesho tunatabiri habari hii itamfunika rais

Kifupi rais ana mengi ya maendeleo na yatabaki kumbukumbu ila CHADEMA mtawatajirisha wenye media, kama mlivyomtajirisha kubenea na habari za ufisadi wa Lowassa, rais atapimwa kwenye boksi la kura lakini si kununua media!
 
Chadema ilisha ondoka na Dr slaa.chadema yasasa ya muunganiko wa Lema, Msigwa , DJ na ma mvi ndio iwe inaongoza upinzani!! Upinzani hakuna tena. Kilasiku wanasajili mijizi tu.
 
Huwezi kusema chadema imepoteana na wakati huo chadema bado inapendwa na watu wengi.

Mleta mada ebu jiulize ni kwanini wananchi ccm wanaiona ni kama takataka. na wakati huo ccm kila kitu wanavyo mfukoni kuanzia pesa polisi mahakama bunge nk.
 
Chadema ilisha ondoka na Dr slaa.chadema yasasa ya muunganiko wa Lema, Msigwa , DJ na ma mvi ndio iwe inaongoza upinzani!! Upinzani hakuna tena. Kilasiku wanasajili mijizi tu.
Na watanyooka sana!
 
Ngoja 2020 ndio utajua kama imechokwa au upo ndotoni!
 
Naona mkuu wao wa idara ya propaganda pale ufipa amekosa mpya ndo maana wanakuja kuja tu baada ya rais kufanya au kusema lolote. Ila kiongoz umeongea fresh ila subiria matus yao maana yapo kwenye sera zao
 
Hakuna anayeiona CCM Kama takataka isipokuwa wenye Akili finyu...
CHADEMA ndio takataka kutokana na kutoeleweka na watu kazi yao
 
Hakuna anayeiona CCM Kama takataka isipokuwa wenye Akili finyu...
CHADEMA ndio takataka kutokana na kutoeleweka na watu kazi yao
Takataka lakini inasumbua akili za watu. Ukishatupa takataka Unaenda fukunyuafukunyua?!! Unaziacha hapo then gari la taka linaondoa. Wonders shall never end.
 
Naona mkuu wao wa idara ya propaganda pale ufipa amekosa mpya ndo maana wanakuja kuja tu baada ya rais kufanya au kusema lolote. Ila kiongoz umeongea fresh ila subiria matus yao maana yapo kwenye sera zao
mkuu nipo tayari kama kitako cha sufuria siogopi moto wa gesi,mkaa wa kuni au mawe na umeme wake mbele kwa mbele kabali yao
 
Wenyewe CHADEMA hawataki Kuambiwa kuwa sasa hv muelekeo wa chama umepotea...
Kimekuwa chama cha Matukio na sio chama cha Ajenda...
Msimamo wa Ajenda ulishakufa zamani na sasa ni Msimamo wa Matukio...
Litakalotokea mbeleni kwenye tukio ndio ajenda yao...

Hapo tu Hata dola hawajawahi kushika wanapoteza Ramani
CDM imepoteza dira, haya sasa baada ya nyie kufurahia mnakuja kuwashauri tena? Wenye akili tumegundua kuwa ni polojo tu.
 
Uhuru wa kuongea saa nyingine haufai kwa viumbe vingine
 
Watu wanaweka hoja ww unawaza hela tu,
Ishi kwa Akili sio kuwatabiria hela watu,
Fanya kazi naww upate Hiyo buku 7 au zaidi ya hapo
Le mutuz na lizabon wameona hicho kitengo hakilipi tena amebaki jinga lao na huyo babu yako kipara na wew unajitumbukiza humo humo ccm sasa inazama
 
Ngoja 2020 ndio utajua kama imechokwa au upo ndotoni!
2020 mbali huko angalia uchaguzi mdogo tu wa madiwani.
e21dd31760af5d197460b87d5b0b7c4c.jpg
 
Chadema ilisha ondoka na Dr slaa.chadema yasasa ya muunganiko wa Lema, Msigwa , DJ na ma mvi ndio iwe inaongoza upinzani!! Upinzani hakuna tena. Kilasiku wanasajili mijizi tu.
Muulize baba yako yohana, anaiogopa chadema mpaka amepiga marufuku miutano ya siasa.
 
Wenyewe CHADEMA hawataki Kuambiwa kuwa sasa hv muelekeo wa chama umepotea...
Kimekuwa chama cha Matukio na sio chama cha Ajenda...
Msimamo wa Ajenda ulishakufa zamani na sasa ni Msimamo wa Matukio...
Litakalotokea mbeleni kwenye tukio ndio ajenda yao...

Hapo tu Hata dola hawajawahi kushika wanapoteza Ramani
Kuna siku mlishakubali chadema wanamuelekeo??
 
Back
Top Bottom